Mafunzo ya kutengeneza mkaa wa kisasa

Status
Not open for further replies.
raw materials za kutengenezea huo mkaa ni zipi?

Pumba kapi za mpunga, maganda na unga wa mbao, mabuwa ya mahindi au mtama, vifuru vya nazi, anyone of these na ukichanganya na jothra au jina jingine m'bono ndio inakuwa kiboko.

Unahitaji kusindika hivyo vitu kwa kutumia pellet making machine au briquettes making machine. Kama huna hiyo unaweza kuunda yako mwenyeyewe kwa kutumia mbao na bomba.
 

Njia hiyo unayoiongelea ushaijaribu wewe mwenyewe au unaongelea tu basics. Njia hiyo ya kusindika inafanya mkaa wako kutoa moshi mweusi unaochafua ukuta wa jikoni kwako wakati unautumia kupikia
 
Nashukuru bwana Biashara2000 kwa elimu niliyopata kupitia kitabu chako. Kwasasa ntaanza kama wewe ulivosema ulianza. Ntafuata mfano wako. Kwa huku Moro soko la mkaa ni kubwa sana kwahiyo hii ni biashara perfect kwa wakazi wa Moro.
 
Nashukuru bwana Biashara2000 kwa elimu niliyopata kupitia kitabu chako. Kwasasa ntaanza kama wewe ulivosema ulianza. Ntafuata mfano wako. Kwa huku Moro soko la mkaa ni kubwa sana kwahiyo hii ni biashara perfect kwa wakazi wa Moro.

Nakutakia kila la heri
 
TANGAZO: Tokea nilipoanzisha hii thread kuhusu jinsi ya kutengeneza mkaa na jinsi mimi ninavyoendesha biashara hii ya mkaa, watu wengi ambao hawako interested au ambao hawana mpango wa kuanzisha biashara ya mkaa ila ni wajasiriamali, wameniomba niwape uzoefu wangu katika kuanzisha na kukuza biashara yenye mafanikio. Na hii inatokana na ukweli kwamba ukiacha kuwa mimi natengeneza mkaa ila zidi hii ni biashara kama biashara nyingine inayoongozwa kwa mfumo wa kibiashara.

Kutokana na nchi hii na duniani kwa ujumla elimu ya biashara imekuwa ikitolewa kwa mfumo wa theory tu kwa maana kuwa elimu inatolewa na watu ambao sio wao wenyewe wafanyabiashara, imefanya watu wengi wanaomaliza vyuo waliosomea biashara au watu waliojifunza biashara kupitia mtandaoni, wanaingia mtaani kuendesha biashara na kukumbana na challenges zinazowafanya wafunge biashara na kugeukia kuajiriwa ili angalau wawe na uhakika wa kupata hela ya kula. Nadhani mnafahamiana na mifano hii huko mitaani.

Kwahiyo wajasiriamali wengi wameniomba niwape elimu kutokana na uzoefu wa ufanyaji biashara ambao nimeupata kwa kufanya biashara katika mazingira ya nchini kama vile jinsi nilivyohangaika kupata vibali mbalimbali vya biashara, jinsi nilivyopata mitaji, jinsi ya kuuza bidhaa katika soko gumu la bongo, jinsi ya ku deal na wafanyakazi, jinsi ya kufikia malengo yako, kuondoa uoga ulionao kwa njia rahisi bila kutumia njia zisizofanya kazi zinazoandikwa kila mahali kwenye internet, na kadhalika wa kadhalika.

Unapoamua kujifunza kupitia mtandao unakuwa unapotea kwa kuwa 1. anayekupa hiyo elimu ni mwandishi tu wa blog ambaye si mfanyabiashara, so ni theory tu, 2. unajifunza biashara katika mazingira ya ulaya na marekani ambapo mazingira yake ni tofauti na bongo. So naandaa kitabu hiki kwa ajili ya uzoefu wangu wa kufanya biashara hapa bongo na challenges zake na solution zake. Sisemi mimi ni bingwa wa biasha ila nachofanya ni kukueleza niliyojifunza kwa kufanya biashara ninayofanya.

Kitabu nimekuwa nikikiandaa tokea nilipoanza kupigiwa simu za maombi. Kitakuwa tayari kesho ijumaa tarehe 1 mwezi wa 2. Kinapatikana kwa sh. 10,000 tu na utajifunza mambo mengi sana yakiwemo hayo niliyoyasema hapo juu. Kwa sasa kitakuwa kinapatikana katika soft copy.

Asanteni sana.
 
We jamaa hata sim hupokei. Nataka uniuzie huo kwanza niutumie ndi niamue kusuka au kunyoa

 

Ujasiriamali juu
 

kumbe ki kibaka tu,nashukuru umenishitua
 
Mie nauliza, unapotoa mafunzo ya kutengeneza mkaa, hiwa vilevile unatoa mafunzo ya kutunza mazingila, nd how does the charcoal you are advocating reduce tree cutting?
 
Mie nauliza, unapotoa mafunzo ya kutengeneza mkaa, hiwa vilevile unatoa mafunzo ya kutunza mazingila, nd how does the charcoal you are advocating reduce tree cutting?

unatunza mazingira kwa kuwa hukati miti
 
kumbe ki kibaka tu,nashukuru umenishitua

Wewe unaona kwenye mtandao kuna info kibao tu za free unazoweza jifunza, hakuna mtu anayekuzuia kujifunza huko. Au unaweza jifunza kupitia mimi. Ndo maana kuna kitu kinaitwa chaguo. Hakuna mtu anayekuzuia. Jaribu kufikiria kimaendeleo zaidi kuliko kukashifu watu. Watu humu mtandaoni wengi ni watu wanaojiheshimu na heshima zao. Kama wewe unajaribu kutafuta excuses kwa umaskini uliomo sasa basi usiambukize na wengine. Mtu mwerevu anapokuwa maskini anajiuliza ni kitu gani atafanya ili atoke kwenye dimbwi hilo la umaskini na si kutafuta visingizio kuhalalisha umaskini alionao. Watu humu wanakushauri ingia mtandaoni ujifunze bureee kabisa hakuna anayekuzuia. Heshima ni kitu cha bure.
 

Nami nataka hiki cha ujasiriamali. Ntakupigia
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…