Mafunzo ya JKT ya Wiki Tatu


Mkuu umenikumbusha mbali sana, hawa makuruta hata kufungua na kufunga SMG sidhani kama wemefanya, LMG ndiyo kabisaaaaaaaaaaa, kwanza angalia kwenye magazeti uone picha aliyopigwa zitto angalia anavyotupa mkono haujanyooka kama wa askari aliyeiva.Gooze match inaonyesha askari alivyoiva.Anyways ikitokea vita tayari tunao askari wa kutanguliza mstari wa mbele kwa ajili ya kutest zari.Nadhani umenipata
 
Kizazi cha kuigiza! Maigizo hayakuanzia hapa, yamehalalishwa hata kwenye ELIMU na mambo mengine!

Ni bahati mbaya sana hata wabunge wa upinzani tuliowaamini nao sasa wameungana na wasanii.Ndiyo maana namkubali Mnyika maana yeye hana unafiki, eti watu wanamlaumu dogo janja ku-jongo JKT ya kisanii, dogo janja kweli kweli alibaini mapema ule ni usanii
 
Niliona Wabunge walipewa mavazi maalumu........wakati wetu haya mambo hayakuwepo....pamoja na muda mfupi huo jamaa wamenyooka...muone Zitto



 
Siasa imeharibu sekta zote muhimu kuanzia elimu mpaka afya, sasa ni zamu ya majeshi. Hawa walienda kuwadhihaki wenzao na ni kejeli kwa sie tuliokaa huko mwaka. Mi nadhani hawakwenda mafunzo bali semina ya Jkt. Sasa Vodafasta mpaka wanajeshi!
 
Niliwaona mahali wanaadaa pass out parade, you could easily see kwamba ni usanii mtupu.

Halafu tulionge na boss mmoja aliyeshiriki kuwafundisha, maelezo yake hali kuwa ni ushahidi kwamba hawa jamaa wamefanya usanii wa kiwango cha juu sana.
 

Wanasiasa mko fiti si mchezo kwani mmeweza kuchakachua hata Jeshi!! nimeona hata kwata yenu ilivyo feki mpaka basi !!
 
Sasa hapo wakijiita makamanda wa akina Halima Mdee nitawaelewa!! Japo kuwa ni wiki 3 tu lakini inaonekana shuruba wameipata yaani Ester Bulaya nilifikiri ni dada muuza vitumbua huku kwetu Tandale kwa tumbo kwa jinsi alivyochakaa!!
 
Unajua Nchi hii mambo mengi tia maji tia maji
 
JKT ina hatua zake:-

Mzalendo = Pit short & Tshirt
Kuruta = Pit short & Tshirt pamoja &Kombati
Service Man/Girl

Mzalendo huwa muda wote anatakiwa kukimbia& si kutembea.

Kuruta nae pia mpaka atakapo Pass out ndiyo anatembe na kuruhusiwa kupiga saluti

Service Man/Girl
Ina maana kuna hatua nyingi muhimu hawajapitia. Huwezi kwenda kuchimba Handaki
bila kusoma aina za Mahandaki

Silaha za msaada zinatakiwa kukaa Handaki la namna gani. Yaani hii ni danganya kubwa wazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…