Dingswayo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 4,019
- 2,932
Nimemona kwenye TV Rais akifunga mafunzo ya JKT kwa wabunge ambayo yalichukua wiki tatu tu.
Nilishapitia jeshini na mafunzo yetu yalichukua mwaka mmoja. Kwa muda wa mwaka mmoja tuliweza kujifunza mengi lakini hata hivyo kwa mawazo yangu niliona kuwa hatukujifunza mengi ya kutosha.
Huu muda wa wiki tatu ni muda mdogo sana kumfundisha mtu ukakamavu wa kijeshi na kumtoa uraia, kujua mbinu za kivita, ikiwa ni pamoja na uzoefu na ujuzi wa kutumia silaha mbalimbali na kubadilisha mawazo na kuleta hisia za uzalendo.
Binafsi naona kama vile walikwenda kwenye ziara ya kujua JKT wanafanya nini.