Mafundi wa Kulalamika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafundi wa Kulalamika

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Simbamwene, May 7, 2009.

 1. S

  Simbamwene JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2009
  Joined: Jun 22, 2008
  Messages: 287
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kuna tabia iliyojitokeza, katika kada mbalimbali za Ndugu zangu Watanzania, Hata taarifa za habari, magazeti na Radio habari nyingi zina tolewa na vyombo hivi za malalamiko, Kwa ufupi asilimia kubwa ya Wazalendo wengi wamekuwa ni mafundi wa kukosoa, kulalamika, kuhukumu na wengine wamefikia hatua ya kuona wanaonewa? Tuki kariri hotuba ya JFK, usiangalie nchi yako imekufanyia nini? Ila jiulize wewe umeifanyia nini nchi yako? Watanzania tuna kwenda wapi? au tumegeuka nchi ya wakiwa?
   
 2. M

  Malila JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Tumelemazwa na dhana kwamba kufaulu kwangu/au kufeli kwangu kumechangiwa na fulani/serikali.Hata kujenga choo cha shimo cha tundu moja kwa ajili ya shule tunataka wafadhili wachangie. Tumefika mahali pale Dar mtu anaweka uchafu ktk mtalo,maji yakifurika analalamika.

  Serikali ina nafasi yake na mtu mmoja mmoja ana nafasi yake ktk kusaka unafuu wa jambo lolote liwalo.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Bwana Malila...

  Hii si nchi ya wakiwa. Uonapo Malalamiko ujue wazi haki

  haikutendeka hapo.. Ujue pia kuna upungufu katika SHERIA NA

  UTAWALA BORA kwa ujumla...

  Wale wapiga kura wa Mbagala wanalalamika kuwa misaada ya

  vyakula na ya kujisetiri inatolewa ki-CCM zaidi kuliko kijamii.

  Wakiona hilo wakae kimya? Kwanini anayepeleka misaada anavaa

  kaniki ya KIJANI na NJANO??

  Huo ni mfano tu mzee...lakini kimsingi, aina ya Utawala wa nchi yetu

  ni kiwanda cha kuzalisha malalamikona inequalities za

  huduma..upo?
   
Loading...