Huko ni kujiaminisha tu.
Ukanunue vifaa wewe fundi, mimi nina uboss gani kushindwa kwenda madukani kununua kwa kufuata mkadirio wako?
Nani asiyejua unaponunua mzigo mkubwa kwenye maduka kuna disscount kubwa pia?
Hiyo disscount unapotoka manunuzi unaweza kuja kunipa taarifa?
Halafu nisipokusimamia, unaweza kufuata taratibu za uchanganyaji wa ratio inayotakiwa?
Mimi nadhani kusimamiana ni jambo la heri sana katika suala zima la ujenzi.
Kama hauna hila kwanini usipende kusimamiwa ili kuondoa majungu?
Mimi siyo local fundi, Mimi ni contractor, civil engineer as well as building materials supplier.Kuna aina mbili za kufanya kazi , forced account ile ambayo unamnunulia mjenzi wako materials yote alafu yeye anakufanyia kazi as per your estimation hivo vifaa vikiisha itamlazimu kukusubiria wewe mwenye kazi ukampatie.
Aina nyingine ni full contract hapa wewe ni kumpa Fundi mchoro na kukubaliana bei afu yeye anakukabidhi jengo lako, ila hapa lazima uwe na consultant Wa kusimamia na kuhakikisha kuwa kazi inafanyika as per agreed specifications.Na hii ni njia wanatumia watu wenye pesa zao na wale ambao kidogo wanaona mbali.
Turudi kwako, wewe kama siyo mhandisi knowledge ya kusimamia standards za jengo huna, hivo hata kama ukiwa site zaidi utakua unasimamia usiibiwe materials.
Mtizamo wangu katika hili.
1.Watu wanipenda wajenge nyumba kubwa na za thamani kwa kutumia bei ndogo i.e kutumia mafundi wasoeleweka ilimradi tu wabane gharama ilihali ana project kubwa in hand, matokeo yake ni kucheleweshewa kazi, kucheleweshewa muda,kubadili mafundi kila Mara , pengine hata kuharibiwa kazi. Hapa Nina mfano hai, Nina client wangu mmoja anataka nimjengee ghorofa bila kutumia ramani, bila michoro ya Chuma, bila vibali vya manispaa eti anataka asevu cost, hili binafsi nimelikataa .
Kuna tendency ya watu kuogopa Ku hire expertise mfano engineer ,technician au architect kwa kukariri eti wana gharama without even consulting one.
N.B Honesty is an expensive thing ,do not expect it from cheap things.