Mafundi uashi wana laana?

Unatakiwa kuhudhuria hapo, kama sio wewe basi MTU wako wa Karibu sana. Mie nipo site mpaka kinasomeka. Mifuko IPO kwenye Gari natoa mmoja mmoja, ikiisha unajua imeisha.
Gari gani??
 
hata yule mungu wa darsalama naye nasikia alikuaga fundi mwashi alafu ndo akaenda kusomea uvuvi. kumbe ndo maana naye ana laana kubwa tuuuu
 
Kila tasnia hapa bongo haikosi wababaishaji,fundi uashi nao mafisadi sijui nani wa kuaminika ulimwengu huu.
Njaa zinatuponza sana,UAMINIFU ni adimu nowdays kama bikra zilivyoadimika.
Ukiwa mwaminifu kwa jamii inayokuzunguka hakika hautalala njaa wewe na familia yako,ukitanguliza tamaa mbele huwezi thaminika na yoyote labda matapeli wenzio.
Wenye busara wana appreciate na kumvalue mtu anaetenda kwa uaminifu.
 
Amekupora ama umempa mwenyewe. Usimamizi wako sio mzuri mpaka fundi anakuibia cement.
 
Nikweli kabisa mtoa mada anachokizungumza sababu kubwa nikutaka urahisi wa bei na hofu na Mafundi wazuri, Hili ndilo lilonifanya mm km Fundi wa ujenzi kuanzia msingi mpaka ufunguo nikawa na wazo nikawashilikisha wenzangu tumeanzisha Chama tunchotarajia kukizinduwa mwakani ili kila anayetaka kujenga popote Tz atampata Fundi mwaminifu na bora kupitia chombo hicho kitakachotambulishwa mwakani na kitamsimamia Fundi kisheria hivyo mafundi wajanja wajanja hawatakuwa na nafasi kabisa.

0788606076
 
Safi naona umeamua kujitangaza kutumia nafasi hii

Ova
 
Fundí mkweli Kinyozi
Brother hata hao wengi wao m naona hawajielewi,nimefungua saloon yangu maeneo ya songea,lakini kila kijana ninayemweka anakuja kwa mbwembwe kazi anafanya lakini uongo na ubinafsi mwingi haleti pesa.sina iman na vijana hawa hasa eneo hili utafikiri walizaliwa pamoja.kazi nzuri ukiweza Fanya mwenyewe kama Mungu amekupa kipawa hicho
 
Fundi Mwashi Fundi seremala hawa sijui wana nini ni shida tu aliyewalaani wao ndiyo wanajua na ndiyo mabingwa wa kusingizia majanga utasikia anakwambia nimefiwa nimeuguliwa yaani sababu ni nyingi mno
Mwingine eti imefika siku ya marejesho eti Dada anaumwa alafu hajatokea kazini
 
Mafundi wote ndo walivyo, sitomsahau fundi nguo niliyempa oda ya suti ya harusi miezi mitatu kabla halafu nguo nikakabidhiwa siku ya tukio asubuhi, hapo baada ya mikwara ya kutosha
 
Tangu lini kinyozi akawa fundi?
Kinyozi ni fundí kunyoa.
Si kila akikabidhiwa mashine na kuwekwa salón anaweza kunyoa ule ni ujuzi. Unanipa pesa unapendezeshwa papo hapo, sawa na usual.
 
Kinyozi ni fundí kunyoa.
Si kila akikabidhiwa mashine na kuwekwa salón anaweza kunyoa ule ni ujuzi. Unanipa pesa unapendezeshwa papo hapo, sawa na usual.
Kumbe, basi hata wapaka rangi kucha ni mafundi.
 
Achaa jamaa awatie nakozi tu maana hamna namna, kibanda changu kimeishia njiani kisa hao, room tatu za kulala katumia mifuko 100 ya cement!!!
We jamaaa nishushe kimara mwisho kabla basi halijafika mbali
 
Mafundi wote ndo walivyo, sitomsahau fundi nguo niliyempa oda ya suti ya harusi miezi mitatu kabla halafu nguo nikakabidhiwa siku ya tukio asubuhi, hapo baada ya mikwara ya kutosha
Afu unaivaa inakupwaya maana alikupima mnene pilikapilika za Harusi ukapungua burudanijeeeee
 
Fundi Mwashi Fundi seremala hawa sijui wana nini ni shida tu aliyewalaani wao ndiyo wanajua na ndiyo mabingwa wa kusingizia majanga utasikia anakwambia nimefiwa nimeuguliwa yaani sababu ni nyingi mno
Ni ma free masson. Hao ni wajenzi huru kwa kuwa hawajaajiriwa na mtu. Wanabangaiza. Sasa tatizo mnalokosea, kuwaamini na kuwarundikia vifaa, ama kuwatuma kwenye manunuzi!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…