Mafundi magari acheni ushamba, kuweni updated

100 others

JF-Expert Member
Aug 5, 2017
3,615
12,040
Kwa mafundi magari wote, mafundi mnaniangusha, kwa nini mko nyuma sana hasa kwenye urekebishaji wa hizi gari za mkoloni?, nyie kila siku ni japanese tu,ndugu zangu dunia ipo kasi sana.

Nitolee mfano kwa mafundi wenzenu wa hizi tv na radio, mafundi walio kuwa wakali wa kurekebisha tv za chogo kama hawakuwa updated hivi sasa imekula kwao na wengine wamefunga ofisi wanafuga kuku, sasa kila mtu ana flat, nani anataka chogo? sasa hivi chogo wanatumia wauza kahawa kwenye vibanda vyao... na muuza kahawa nyumbani kwake ana flat.

Ndugu zangu mkiingia kwenye field za kiteknolojia lazima muwe updated, wanaoanzisha trend mara nyingi ni hizi kampuni kubwa kubwa mfano kwenye simu unakuta iphone, samsung, nokia, huawei n.k... hawa wakianzishaga trend tu, haipiti muda akina itel, tecno, infinix n.k nao wapo nyuma kwa kasi wakifuata mbio za mwenge.

Mfano iphone walipokuja na notch kwenye kioo, iphone ni kampuni kubwa na simu zilikuwa za gharama, sasa hivi infinix na itel na zenyewe zina notch...aseee.

Internal battery, internal memory fingerprint n.k vyote hivyo kampuni za kichina huwa zinakuja kubuni na kuweka hizo features japo si quality kama za hao vendor wakubwa lakini wenye kipato cha chini wanakimbilia kununua nao wasiwe mbali na trend tena kwa gharama nafuu... sasa hizi kampuni kubwa zikiona akina itel na tecno wanakimbiza, wanarudi tena na wao wanatengeneza simu affordable zenye latest features kupambania kombe angalia J series za Samsung.

Sasa kwa hio mifano , kama mna akili tayari mmekwisha jua namna ya kusoma nyakati hasa kwenye hii field, zamani push to start ilikuwa inaonekana dili sana,sasa hivi porte zina push to start.

NI kwamba hizi features kwenye hizi bmw, benz n.k tunapoelekea na kuanzia sasa zinakuja kwa kasi kwenye hii mitumba ya kijapani(toyota), toyota sasa wanakuja na gari zao zina sensor kama zote, umeme kama upo tanesco, and all that, tusiwazungumzie wenzetu huko USA, wao wapo na Tesla huko gari ina injini kwenye matairi.

Muda si mrefu hizo toolbox mtakwenda kupima vyuma nipo hapa.

Hakuna kampuni hasa kwenye hii field ya tech wanataka kuwa nyuma.

Haihitaji urudi shule kujifunza mautundu, maujuzi, unahitaji smartphone na bundle tu... mambo yapo mtandaoni na advantage tayari mna basics za ufundi hakuna kinachoshindikana.

Mimi nimefungua generator la diesel lilikuwa haliwaki, nimepeleka kwa fundi kiswahili kikawa kirefu... nikarudi home... nikalifungua looote! vifaa vyote nikaweka kwenye mkeka chini. Kwa kutumia youtube na sources mbali mbali... nikalisafisha fresh... nikagundua tatizo.. nikanunua steel wire safisha fresh, nikalifunga looote. Kuna mzee amenikuta akasema we kijana mbona umeharibu hilo generator... nimelirudisha nikapiga kiki 1 tu ngoma ikaita. Na hapo mechanics sijui... ni ujanja tu...

Ndugu zangu someni nyakati... mnaendelea kusema bmw na benz hazina deal wakati toyota upepo unampeleka huko huko...

Niseme kwamba... someni alama za nyakati... vijana hivi sasa hawataki vipando vya kizembe... Hybrid zimekuwa nyingi hii inamaanisha dunia inahama kutoka kwenye utumiaji wa mafuta kuelekea kwenye umeme thats why gari ina vyote viwili... nakumbuka kipindi SATA hard disk za computer zinaingia huku IDE ilikuwa sokoni kwa muda, ziliingia mashine nyingi sana zikiwa na SATA na IDE hapo hapo, kumbe ile ilikuwa ni kama message kwamba IDE ndio mwisho wake.

Hata kipindi floppy disk zinatoka na CD zinaingia, ziliingia cpu nyingi zina floppy na CD , lakini sasa kuna CPU zinakuja na floppy? kuna CPU Zzina hard disk za IDE?

Wanaofahamu masuala ya Computer wamenielewa.

Teknolojia ni kama mafuriko, tengeneza njia maji yapite ukitaka kuyazuia utaumia.
 
umesema kweli mkuu, siku hizi mambo ni Mechanical and Electonics, iko course mmoja inaitwa MechaTronics.........ndio mpango mzima, magari siku hizi ni Computer Box ama ECU, alafu mengine chuma.

Computer iki goma, gari halisongi hata hatua mmoja!
Mechatronics imecombine Mechanics, computer, electronics systems and control system.
 
Mimi nimefungua generator la diesel lilikuwa haliwaki, nimepeleka kwa fundi kiswahili kikawa kirefu... nikarudi home... nikalifungua looote! vifaa vyote nikaweka kwenye mkeka chini. Kwa kutumia youtube na sources mbali mbali... nikalisafisha fresh... nikagundua tatizo.. nikanunua steel wire safisha fresh, nikalifunga looote. Kuna mzee amenikuta akasema we kijana mbona umeharibu hilo generator... nimelirudisha nikapiga kiki 1 tu ngoma ikaita. Na hapo mechanics sijui... ni ujanja tu....

Hii inaitwa DIY, safi sana...

So kwenye hiyo generator uligundua tatizo lilikuwa wapi?
 
Mechatronics imecombine Mechanics, computer, electronics systems and control system.
Nadhani kuna fani zingekuwa zinawekwa kwenye level ya upili wa digrii kuleta umaana mzuri, mfano;

1. Mechatronics ingekuwa kwenye level ya masters baada ya kusoma bachelor ya mechanical.

2. Electromechanical ingekuwa ni masters inayochukuliwa na wenye B.eng

3. Architects/Quantity survey ingekuwa masters kwa wenye civil engineers

Na kadhalika.
 
Ni kweli kabisa usemayo,sasaivi teknolojia imebadilika sana,mfano mdogo tu mwingine kwa madreva teksi wale wa zamani wanasema sasaivi kazi ngumu kumbe wameshindwa kugundua sasaivi teknolojia nayo imebadilika sasa ni mwendo ukitaka mteja basi lazima utumie smartphone ndio upate mteja mambo ya uber,taxify,bolt
 
Mkuu somo zuri sana. Ukiwa addicted kutumia mtandao hasa katika kujifunza, utaongeza skills nyingi sana ndani ya muda mfupi.

Ulimwengu unabadilika sana lazima na lazima tu-update maarifa tuliyonayo.
 
Nadhani kuna fani zingekuwa zinawekwa kwenye level ya upili wa digrii kuleta umaana mzuri, mfano;

1. Mechatronics ingekuwa kwenye level ya masters baada ya kusoma bachelor ya mechanical.

2. Electromechanical ingekuwa ni masters inayochukuliwa na wenye B.eng

3. Architects/Quantity survey ingekuwa masters kwa wenye civil engineers

Na kadhalika.
Mkuu wazo zuri sana...
 
Ni kweli kabisa usemayo,sasaivi teknolojia imebadilika sana,mfano mdogo tu mwingine kwa madreva teksi wale wa zamani wanasema sasaivi kazi ngumu kumbe wameshindwa kugundua sasaivi teknolojia nayo imebadilika sasa ni mwendo ukitaka mteja basi lazima utumie smartphone ndio upate mteja mambo ya uber,taxify,bolt
Hivi wapiga picha zile za karatasi siku hizi wana dili kama zamani kweli? zamani walikula maisha sana,
 
Mkuu somo zuri sana. Ukiwa addicted kutumia mtandao hasa katika kujifunza, utaongeza skills nyingi sana ndani ya muda mfupi.

Ulimwengu unabadilika sana lazima na lazima tu-update maarifa tuliyonayo.
Mkuu huwezi amini nilipika pilau, shemeji yako hakuamini, nimeshamwambia kabisa mimi suala la kupika ni moto wa kuotea mbali, kuna day alikuta andazi na chapati, amenyoosha mikono anajiuliza mwanaume gani anapika hv, kumbe ni youtube... nikiwa na ipad nimeweka pale... nafuata hatua moja hadi nyengine...
 
Back
Top Bottom