Mafisadi wavamia gazeti Tanzania daima!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafisadi wavamia gazeti Tanzania daima!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by USTAADHI, Jan 31, 2012.

 1. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Nalazimika kuweka jamvini hapa kwenye fikra zenye utafiti na kwa imani pia kuwa ntawapata wahusika kujibu hoja yangu kama akina KIBANDA,NGURUMO kuhusu hii harufu inayoelekea kwenye gazeti TANZANIA DAIMA(SAUTI YA WATU) kwa wale wasomaji na wafuatiliaji wa magazeti ya kila siku yenye mlengo wa kutetea jamii likiwemo TANZANIA DAIMA mtakubaliana na mimi kuwa gazeti hili limekuwa kichomi kwa serikali ya kifisadi siku nyingi sana na kujipamabanua kuwa kimbilio la makundi mbalimbali yanayotaka habari yao ya ukweli uwekwe wazi, na hata kufikia sehemu likanyimwa matangazo na serikali na idara mbalimbali likishutumiwa kuwa gazeti la CHADEMA!!.

  Hii ilikuwa kama silaha ya mafisadi kulifanya lisifanye kazi yake,
  Tumeshuhudia pia mhariri mtendaji BW ABSALOM KIBANDA akipelekwa mahakamani kwa uchochezi!

  Tumeshuhudia pia jengo wanalofanyia kazi likiwa na misuko suko mbalimbali hata ya kutaka kutaifishwa na serikali

  LAKINI sasa kwa mbinu ya mafisadi imepata kufanya kazi kama ifuatavyo:
  kwa siku za hivi karibuni kumezuka mtindo ndani ya gazeti hili unaoratibiwa na baadhi ya wandishi kulififisha ama kulipotezea mvuto kwa wasomaji gazeti hili kwa jamii kitendo ambacho hakijulikani kama kinafanyika kwa maslahi binafsi ya mwandishi! lakini kwa ujumla wake ni kero kwa wasomaji wa gazeti hili.
  mfanono1' MGOMO WA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU(UDSM) katika sakata hili TZ DAIMA kupitia mwandishi wake HAPPINESS KATABAZI walitoka hadharani na kuwashutumu wanafunzi kuwa wanatekeleza mawazo ya watu fulani!
  Huku serikali ikipinga kuwa madai ya wanafunzi hayana msingi na kudai kuwa wameishalipwa hakuna ambaye hajalipwa hoja ya mwandishi huyu ilijikita kumtetea prof mkandala na kukandamiza wanafunzi lakini pia mwandishi aliungana na propaganda zilizokuwa zinatolewa na serikali ya CCM kuwa wanafinzi wametumwa na CHADEMA!
  MAMBO YALIBACKFIRE! kwenye kamati ya bunge ya hesabu za serikali kuwa uongozi wa vyuo unapokea mikopo kutoka bodi ya mikopo na kukaa nayo ama hata kutumia majina ya watu wasiokuwa watahiniwa ama hata kutumia majina mara 2 hapa sikuona TZ DAIMA kupitia katabazi wakitoka na kushutumu vyuo!
  Na ubadhirifu ulibumbuliwa mpaka kufikia mkuu wa chuo cha MKWAWA kuitwa kujibu hoja ambazo mpaka sasa hatujui nini kinaendelea!.hiii ilikuwa picha halisi ya kuthibitisha kuwa madai ya wanafunzi yalikuwa ya msingi kwa ujumla wao na wanafanyiwa uisadi na viongozi wa vyuo na hawakutumwa na mtu yeyote kama katabazi alivyodai! au hata kamati ya bunge nayo ilitumwa?

  2 SAKATA LA KESI YA JERRY MURO`
  wakati watanzania wengi wakiwa na masikitiko kwa jinsi mafisadi walivyojaribu kumwangamiza mwandishi mwenzao jerry muro gazeti hili pia kupitia HAPPINESS yuleyule katabazi mwandishi ambae ni mtu wa karibu sana kimahusiano na LYUMBA ,PROFESA MUKANDALA,NA BAADHI YA VIGOGO NDANI YA SERIKALI WAKIWEMO WANA USALAMA
  alimtia hatiani yeye mwenyewe jerry muro hata kabla mahakama haijafanya kazi yake lakini baada ya hukumu ya jerry muro kutoka mi sijui labda bi katabazi atakata rufaa!!!!????
  3SAKATA LA MGOMO WA MADAKTARI!!

  jana tarehe 30 jan 2012uk wa 7 TZ DAIMA tena kupitia happiness katabazi waliwalima madaktari kwa kile walichodai huku wakishutumu madaktari kuwa walijikweza sana kukataa kuonana na haji mponda waziri wa afya pia kutokujitokeza kwenye kwenye mkutano wa PINDA

  hoja za katabazi zilijikita kujenga taswira ya kuona kuwa madaktari hawakuwa na haja ya kugoma na wala kudai nyongeza yoyote ya kwa kuwa hawakufuata taratibu za kugoma na kudai eti maneno ya madaktari yalikuwa yaSHOMBO HIZI NI LUGHA ZA MTAANI NA MAGAZETI YA UDAKU! sasa inakuwaje madai ya wataalamu yaitwe shombo? ndugu zangu TZ DAIMA ! KATABAZI!

  ZAidi akaandika eti madaktari hawa hawana tofauti na jambazi anayekuwekea bunduki kichwani akitaka chako! leo madaktari kukataa night alowannce ya 10,000 NI MAJAMBAZI?! au kudai nyumba za kuishi ni ujambazi?

  , kudai alowance za kufanya kazi hatarishi kama kuhudumia waathirika wa ukimwi na mtu kupata maambukizi pasipo hiari ni ujambazi?

  kama hawa hawa madaktari ni majambazi vipi kuhusu nyie waandishi mnaoweka taaluma pembeni kuandika anachotaka lyumba au mkanadala au BLANDINA NYONI KWA malipo ya suti pale kwenye duka la MARIEDO?

  VIPI kuhusu wabunge walikubali kupewa 330,000 kila siku kwa mwezi m6.9 endapo wakiwa bungeni? achilia mbali mshahara na hata excemption zingine kama kutolipia ushuru wa magari wakiagiza ?

  vipi kuhusu waliolipa RICHMOND,EPA,........... NA mikataba ovyo chungu mzima umewahi kuwashutumu katabazi?
  vipi kuhusu swahiba wako wanaokuweka mjini waliochota hela BOT? hawa si majambazi?

  kama madaktari wanadai nyumba za kuishi tatizo liko wapi si wapewe NHC ambazo wahindi wanahodhi? au kwako wahindi ni wa mhimu sana?

  umewahi kuona DK hata 1 anatumia VX V8? hao wanaozitumia kwako ndio wa muhimu? waandishi wa aina yako wanapaswa kuwa kwenye magazeti ya uhuru,HABARI LEO,HOJA,TAZAMA TZ TUNAOMBA UTUACHIE GAZETI LETU USILIHARIBU

  NA KAMA KUNA KIONGOZI ANAKUKUMBATIA NDANI YA BODI YA WAKURUGENZI TUTAMUANIKA ILA WEWE SASA TUNAANZA KUFUATILIA USAFI WAKO

  NAWASILISHA WANAOMFAHAMU ZAIDI HUYU MCHWA ANAYEKULA GAZETI LA WATU AWEKE HAPA


   
 2. menyidyo

  menyidyo JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 1,339
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  umemchambua.
   
 3. Lyceum

  Lyceum JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Haisomeki thread yako mkuu
   
 4. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  haisomeki? kwa nini soma na utafakari
   
 5. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  font hovyoooo....
   
 6. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Nimepata tabu sana kuisoma,sijui labda ni miwani yangu.Kama inawezekana iweke vizuri ili tuipate vizuri zaidi.
   
 7. Lyceum

  Lyceum JF-Expert Member

  #7
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Font aliyotumia ni full wino mkuu. hasa paragraph 2 za mwisho
   
 8. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #8
  Jan 31, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  chukua kontenti acha kupoteza lengo la ujumbe au ndo wale kina mariedo?
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  Jan 31, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,555
  Likes Received: 18,259
  Trophy Points: 280
  Ustaadhi, tofautisha uandishi wa reporting na makala. Nadhani hayo unayo lalamikia ni makala za Happynes na sio news. Kwenye maoni ya makala, ni maoni ya mwandishi na sio maoni ya gazeti.
   
 10. MASAMBI

  MASAMBI Member

  #10
  Jan 31, 2012
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  i cant read it
   
 11. m

  mashambani kwao JF-Expert Member

  #11
  Jan 31, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  acheni uvivu wa kusoma mbona ameeleweka?
   
Loading...