Mafisadi wa DARUSO waumbuka

Mafisadi wa DARUSO waumbuka

miss confidence

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2016
Posts
393
Reaction score
273
Heshima zenu wana JF.

Katika harakati za kuendelea kukomesha tabia ya ubadhilifu wa Mali za umma mnamo tarehe 13 mwezi wa sita katika Bunge la serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha dar es salaam (DARUSO- Mlimani campus) mbunge wa viti maalumu kutoka ndaki ya insia / College of Humanities (COHU) mwaka wa kwanza Mh Halima Juma John aliwasilisha hoja binafsi kuhusu ubadhilifu wa fedha za DARUSO katika serikali iliyopita 2016/2017 na hoja hiyo iliungwa mkono na wabunge wote wa bunge la DARUSO chini ya spika wa bunge hilo Mh Deogratius Mahinyila na kwa pamoja kama bunge waliadhimia uundwaji wa kamati maalumu ya kufuatilia ubadhilifu huo kama ulivyo bainishwa na Mh Halima Juma John katika hoja yake Bungeni.

Kamati ilipewa wiki mbili kwaajili ya kukamilisha majukumu yake ya kufuatilia mapato na matumizi ya DARUSO kwa mwaka wa masomo 2016/2018 ambapo kamati ilibaini ufisadi mkubwa sana uliofanywa na viongozi wa serikali ya DARUSO ya mwaka 2016/2017 iliuokuwa chini ya rais Leon Erasim... Baadhi ya mawaziri waliokumbwa na hatia katika ripoti ya kamati hiyo ni aliyekuwa waziri wa katiba na sheria DARUSO ndugu Boniventure Erick, aliyekuwa waziri mkuu wa DARUSO ndugu Boniphace Emmanuel, waziri wa fedha ndugu Gamba na aliyekuwa kaimu wa wizara ya mikopo Ndugu Makupa..

Ripoti imebainisha watu hawa wameiba zaidi ya milioni 20 za wana DARUSO kitu ambacho ni kinyume cha katiba ya DARUSO na katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Naambatanisha na ripoti hiyo hapa chini wana JF muone jinsi gani mafisadi ya nchi hii tunavyokuwa nayo tangu huku chini na panapo fikia ngazi ya juu yanakuwa majizi yaliyokubuhu.
 
university bwana? Ukiona hoja hizi ujue UE wamemaliza.
 
Je, hakuna utaratibu wa Rais (DARUSO) kuwasilisha bungeni ripoti ya Mapato na Matumizi kila baada ya miezi mitatu?

Kisha bunge kuijadili na kuipitisha kama wameafikiana Nayo?
 
Huu utaratibu haupo mkuu... Utaratibu uliopo Mara baada ya bajeti kupita majukumu ya kiserikali huendelea kama kawaida na habari ya kusomeana mapato na matumizi hufanywa ktk ile siku ya kuvunja bunge ambapo ripoti husomwa na ofisi ya waziri mkuu kuhusu utendaji kazi wa kipindi chote kwa kila wizara na serikali kwa ujumla.
 
Mkuu hujaambatanisha ripoti uliyosema
 
Back
Top Bottom