Mafisadi kutumia Bunge kumtisha Dr.hosea

sulphadoxine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,257
644
Nimkakati wa kuzuia kesi nzito za rushwa kuchunguzwa.

MKAKATI mzito unaandaliwa kumtisha Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hoseah, kwa nia ya kuzuia ukamilishwaji wa kesi nzito za ufisadi zinazochunguzwa na taasisi hiyo, baadhi ya mikakati hiyo ikielezwa kutumia vikao vya Bunge, imefahamika.

Habari kutoka
Dodoma na Dar es Salaam zimeeleza kwamba tayari
watuhumiwa wakuu wa ufisadi wamekwishaandaa watu maalumu kutumia vikao vya Bunge vinavyoendelea mjini
Dodoma
kuwasilisha ujumbe utakaommaliza ama kumtisha Dk. Hoseah kwa nia ya kumpunguzia kasi ya kushughulikia majalada ya ufisadi.

Dk. Hoseah ambaye watuhumiwa wa ufisadi wamemuelezea kama mtu asiyetabirika, amekataa kuzungumzia mikakati hiyo alipohojiwa na Kulikoni hivi karibuni akielezea kwamba amezoea kukabiliana na
changamoto nyingi katika kazi zake na kwamba anachojitahidi ni kutenda haki bila kujali mamlaka na dhamana ya mtu kisiasa.

“Sina taarifa za mikakati ya kunichafua, lakini nafahamu kwamba watu wanaojijua kuwa si wasafi wamechanganyikiwa na hakuna ajabu kusikia kwamba wanaingia gharama kunichafua. Ninachoweza kuwahakikishia Watanzania wenzangu ni kwamba nitawatumikia kwa uadilifu na nitatenda haki bila kujali nafasi ya mtu katika jamii,” anasema Hoseah.


Source:Gazeti la kulikoni la leo tarehe 1-7 july 2011
 
Ninachoweza kuwahakikishia Watanzania wenzangu ni kwamba nitawatumikia kwa uadilifu na nitatenda haki bila kujali nafasi ya mtu katika jamii,” anasema Hoseah.

... namforwardia Liyumba nipate comments zake kuhusu hili.
 
Simwamini sana Hosea. mkikumbuka suala la RichLowasa, oh no I mean Richmond, itakuwia vigumu kumuamini mtu huyu. Aidha, fuatilia yaliyomwangwa na Wikileaks kumhusu kamanda huyu wa PCCB
 
Dr.Hosea ni moja ya watendaji wa serikali ambao siwahamini hata kidogo +DPP
 
Duuuh waheshimiwa hawachelewi kumwekea Hosea zile sumu zao za Dodoma kama ilivyowatokea baadhi ya waheshimiwa wapambanaji wa ufisadi...Mungu alilinde jembe letu, Hosea kama unanisoma chapa kazi na hakikisha kila sisimizi aliyekula rushwa unampeleka kwa pilato...wakanyee madebe segerea...kaza buti
 
Hosea ni gamba anachofanya sasa ni kutuaminisha kuwa all of his failures are result of poor system. Mabwepande wamejipanga vizuri, kila kona wamo.
 
Gangsterrone inaonekana we Ni Mtetezi mzuri wa huyo jamaa ebu tupe mazuri take japo na sisi tuyaone kama unavyoyaona manake umekuwa ukimtetea hata pale ambapo hapastahili,Kama vita ya rushwa jamaa kafelli tukiongea kuishindwa kwake munasema sisi CDM
 
Back
Top Bottom