Mafisadi CCM sasa wakalia kuti kavu; JK alikwepa mtafaruku, kupisha upepo mbaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafisadi CCM sasa wakalia kuti kavu; JK alikwepa mtafaruku, kupisha upepo mbaya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Nov 28, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  28 NOVEMBER 2011  *Mkakati wa kuwamaliza kidiplomasia yatajwa
  *JK alikwepa mtafaruku,kupisha upepo mbaya


  Na Mwandishi Wetu

  SIKU tatu baada ya kumalizika kwa vikao vya juu vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma wiki iliyopita, upepo mbaya umeanza
  kuwaelekea watuhumiwa wa ufisadia ndani ya chama hicho wanaotakiwa kujivua magamba kwa kutafakari wenyewe tuhuma zao kabla ya kuondolewa kwa nguvu.

  Hali hiyo inatokana na siri nzito kutoka ndani ya vikao hivyo kueleza kuwa mbinu iliyotumiwa na Mwenyekiti wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete, kurudisha suala hilo kuamuliwa na Kamati ya Maadili kisha kuwasilisha maamuzi yake kwa Kamati Kuu unalenga kuwamaliza kabisa watuhumiwa hao.

  Imeelezwa kuwa syahili hiyo mpya iliyotumika mjini Dodoma haikulenga kufuta mchakato wa kuwaondoa watuhumiwa haoa kama ilivyodaiwa bali ulilenga kuepusha malumbano ndani ya kikao baada ya kubainika kundi hilo kuandaa watu wao kuwatetea kwanguvu kubwa na kuwa tayari hata kuchafua hali ya hewa.

  Taarifa zilizoifikia Majira juzi na jana, vinaeleza kuwa baada ya kundi hilo kudaiwa kuwa na wafuasi wengi ndani ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), washauri wa masuala ya kisiasa ndani ya CCM walitaka Kamati ya Maadili imalize suala hilo kukwepa mjadala mzito kutokana na wahusika kuwa na kundi kubwa la kuwatetea.

  "Kilichotakiwa watu waelewe tangu mwanzo ni kwamba CCM kama chama ni wajanja kuliko kundi la mafisadi, wale jamaa walijiandaa na wana wafuasi na kundi kubwa ndani ya NEC, kuwamaliza mle ni tatizo kubwa.

  "Njia pekee wa kuwamaliza ni kuwaachia Kamati ya Maadili ambako mle kuna wajumbe wachache na wenye msimamo thabiti na wanaoijua vizuri chama, kama mnafikiri kujivua gamba imefikia mwisho subirini mtaona matokeo, Kamati inakwenda kumaliza kila kitu,"kilisema chanzo chetu.

  Taarifa hizo zilieleza kuwa Rais Kikwete baada ya kuona hali halisi na kupewa taarifa za siri za jinsi kundi hilo ilivyojipanga kupambana kufa na kupona alishauriwa na wakongwe mbalimbali wa kisiasa kumaliza suala hilo kwa njia ya diplomasia na kwamba hakuna atayelaumiwa.

  "Kamati ya Maadili ikishamaliza itawasilisha maamuzi yake ambayo kwa lugha ya diplomasia ya chama huitwa mapendekezo, Kamati Kuu itabariki maamuzi hayo na hapo ndio mwisho wa hatua hiyo watafuata wengine," kilisema chanzo chetu ndani ya CCM.

  Majira ilipomtafuta Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Bw. Nape Nnauye, kuthubitisha taarifa hizo alisema yupo kwenye kikao na kuahidi kutoa ufafanuzi baada ya kumaliza. Hata hivyo hadi tunakwenda mtamboni kiongozi huyo hakuweza kuzungumzia suala hilo kwa maeleoz kuwa bado anaendelea na kikao.

  Wajumbe wa Kamati ya Maadili ya CCM ni Mwenyekiti wa Taif Rais Jakaya Kikwete, Makamu Bara Bw. Pius Msekwa, Amani Karume, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balosi Seif Iddi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Katibu Mkuu Wilson Mukama, Naibu Katibu Mkuu Bara Bw. John Chiligati, Vuai Ali Vuai.


  Kwa mujibu wa taratibu za CCM Kamati ya Maadili inaweza kuchukua hatua moja kwa moja au kutoa mapendekezo kwa Kamati Kuu (CC) ambayo pia wajumbe wake karibu wote wanaingia pia kuyabariki.

  Katika kikao cha NEC cha wiki iliyopita Waziri Mkuu aliyejizulu Bw. Edward Lowassa, alilalamika kuchafuliwa huku Waziri Mkuu Mstaafu Bw. Frederick Sumate, alitaka majibu ya sababu zinazofanya wanaochafua Bw. Lowassa kutochukuliwa hatua kama hana kosa.

  Suala la kujivua gamba ndani ya CCM imeleta mwamko mpya wa kimtazama ndani ya CCM huku kundi moja linalojipambanua kuwa na msimamo wa kimaadili ikielezwa kuusimami na upande wa pili ukieleza kuwa ni mchakato unaokivuruga chama hicho kwa madai kuwa hakuna ushaidi wa magamba yanayotakiwa kuvuliwa.   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Nov 28, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,376
  Likes Received: 19,646
  Trophy Points: 280
  aaaaaaa, wawamalizeje? Alfu lela ulela
   
 3. h

  hsagachuma Member

  #3
  Nov 28, 2011
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Muda wa maamuzi magumu kwa chama umefika. Nadhani anaye jiona fisadi aachie ngazi mapema
   
 4. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #4
  Nov 28, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Andrew Chenge siyo mjumbe wa kamati ya maadili? Atajihukumu mwenyewe?
   
 5. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #5
  Nov 28, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  hakuna lolote hapa kiboko yao chadema tu. mwambie mtu ukweli ili umuweke huru.
   
 6. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #6
  Nov 28, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,639
  Likes Received: 1,428
  Trophy Points: 280
  Nchi hii bana.. halafu na wananchi wake wapo wapo tu!
   
 7. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #7
  Nov 28, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,157
  Trophy Points: 280
  CCM bwana, wana porojo nyingi utadhani NAZJAZ
   
 8. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #8
  Nov 28, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  What? Majira? aaaah No no no. You have to take more time n convice me.
   
 9. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #9
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hivi hii picha<ya kujivua gamba>mbona imekuwa ndefu kama isidingo?Haina mwisho?
   
 10. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #10
  Nov 28, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Nape mbona kimya, mbona hajatuletea maamuzi ya NEC ya CCM maake alisema ndiye source. au wamemvua/amejitoa/amezira
   
 11. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #11
  Nov 28, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hatua za nidhamu sasa kumgeukia Nape. EL & Chenge watasafishwa watakuwa wasafiiiiiiiiiiiiiiiii (ndani ya CCM)
  Hiyo ndio CCM, Nape simwoni sikuizi JF...

  [​IMG]
  Il Gambino.
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  Nov 28, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,791
  Trophy Points: 280
  Porojo hizi jamani zimechosha...tuanze porojo za waluguru walima viazi, wakaguru walima mahindi, wahehe walima mahindi etc
   
 13. j

  jigoku JF-Expert Member

  #13
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Hiyo ni ZE COMEDI TU,hakuna mwenye uwezo wa kumhukumu mwenzie,na mfano hai ni hivi juzi wakati kikao kikiendelea,EL amenukuliwa akimwambia JK juu ya tuhuma zake zilizotaka kuibuliwa na kina D.Mwakawago na JK kuokolewa na uncle Ben na akakumbusha kuwa aliwahi kumwambia kuvunja mkataba wa Richmond bado JK alikataa,sasa kwa hayo tuliyoyasikia na mengine ambayo bado yamefunikwa kuhusu JK na wengineo,mnadhani ni nani anaweza kuibuka na kumhukumu mwenzake?hiyo ni sawa na FUTUHI au OK(original komedi).CCM ni ya kusafishwa na wananchi pindi waliowengi watakapobaini uchafu wa chama hiki na ufisadi inaoulea kila siku bila kujali unavyoitafuna nchi katika kila sector.
   
 14. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #14
  Nov 28, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kwa style hii du Patamu,Kama Movie hii ikichezwa na vyema,na hakika CCM watajipanua kuanza kuaminika tena kuwa kumbe hakuna Mwanachama aliyejuu kuliko chama.Ili waanzie hapo kutambua kuwa Wananchi siku hizi wanjua nazi ni nazi na sio kuwa nazi ni dafu.Wasieneshe tena michezo ya kutizama upepo wa Wananchi utesemaje waendeshe chama chao kwa misingi ya HAKI NA UKWELI NA SIO MAIGIZO.

  Zama za kirusi [Putin] kwa Tanzania zimekwisha zamani,siasa za wazee wa zamani waliosoma Russia [USSR] na China,siasa za baadhi ya Watu wachache ndani ya Nchi kuunda kakindu cha Watu wachache na kujiita wao ndio Nchi na kila kitu wao ndio wanajua hayo yanafanyika huko Russia na China,na sio Tanzania.Nyerere kama Muungwana alikopi kweli baadhi ya mifumo ya uko lakini alipoona baadhi ya mikakati yake inapingana na utu wa binadamu akaachana nayo.Kama Mwalimu Nyerere angengania basi leo Tanzania angeitawala mpaka anakufa kitandani.

  CCM wafike sehemu waachane na mbinu chafu dunia imeshakuwa ndogo kwa kuwa technlojia imeshazaa upataiakanaji wa taarifa sahihi na wakati sahihi mara moja na kwa kasi ya ajabu.Hivyo kuendeleza siasa za kinafki na uongo wa ghilba kwa watu wenye taifa lenye umri wa miaka hamsini ni aibu.Sisi tulio vijana tutakopi ujinga mara dufu kuliko ujinga wenu,hivyo tutahatarisha Taifa ambalo nyie wanaccm mnaishi ninyi, mama,baba, watoto na dada zenu.
   
 15. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #15
  Nov 28, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  upepo mbaya unakwepa upepo mbaya.
   
 16. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #16
  Nov 28, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hii episode ya kuvuana magamba.....ikimalizika itakuja episode gani vile?
  Nauliza hili kwa sababu kuwatoa magamba wachache hakutamaliza tatizo la ufisadi na uozo chamani wala serikalini.
  Tunachotaka wananchi ni kumalizika kwa ufisadi wote! Tunataka haki na fursa sawa kufaidi rasilimali zetu. Haijalishi ni chama gani
  wala ni watu gani.Hivi leo tumeambiwa wabunge washajiongezea maposho kwa zaidi ya 150%! Inahuu?
   
 17. Antonov 225

  Antonov 225 JF-Expert Member

  #17
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hawa jamaa hakuna lolote ni njia ya kusahaulisha wananchi kuhusu maandamano yetu ya katiba. Huuu ujinga wao wamalize huko huko sisi tunataka ku-exercise nguvu ya umma.
   
 18. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #18
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Raisi mwoga? anaogopa mtafaruku?
   
 19. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #19
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Mimi ni msafiri bado nipo njiani....! sijui lini nitafika ooooh!, naulizia watu kule ninakokwenda......! naambiwa bado ni mbali! sijui lini nitafika oooo!
   
 20. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #20
  Nov 28, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Muda ulishafika siku nyingi. Tatizo ni kukosekana mwenyekiti makini na mwenye ujasiri wa kutoa maamuzi magumu, siyo huyu ambaye naye ananuka ufisadi kuliko hata watuhumiwa.
   
Loading...