Mafia: Wavuvi wapoteza maisha baharini baada ya samaki aina ya Potwe kuvuta nyavu zao

Dah! Huyu samaki mkubwa sana
images%20(67).jpg
 
Habari zenu wakuu

Leo nina majonzI sana baada ya wavuvi watatu kupoteza maisha kisiwani Mafia ambao katika bandari ya Tumbuju, wavuvi hao walikuwa kwenye boti wakielekea kuvua kwa kutumia nyavu za kupingia.

Baada ya kufika bahari wakatosa nyavu zao na baadhi wakateremka ili kupingia samaki waweze ingia kwenye nyavu sasa kwa bahati mbaya ndani ya nyavu aliingia samaki mkubwa na baadhi ya wavuvi ndio walishikilia nyavu samaki alipoona kazongwa na nyavu ndo akaamua atumie nguvu ili kijihami kuelekea bahari kuu ndipo akaondoka kwa nguvu sana.

Akaondoka na nyavu pamoja na wavuvi watatu ambao walizingirwa na nyavu ila baadae walionekana baada ya kutafutwa na wote washazikwa tayari, samaki anaitwa Potwe.

Kilindoni, dongo, ndagoni, tumbuju, kirongwe, jojo, Benjamin na beni bila kusahau Kanga
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom