Mafanikio ya nguvu ya umma haya hapa

Mafanikio ya nguvu ya umma haya hapa

Ndumule

Member
Joined
Sep 20, 2010
Posts
6
Reaction score
1
Sina shaka wengi wetu tumeanza kuona dalili za serikali kuanza kuamka kutoka usingizini. Kwanza ilianza na kuwaweka mawaziri wachapakazi kwenye wizara muhimu k.m. Magufuri, Mwekyembe n.k. Mtakumbuka kuwa awamu ya kwanza magufuri aliwekwa wizara ya kitoeo. Pia huko nyuma Rais kwa kujiamini kabisa alishawai kutangaza kuwa hataki kura za wafanyakazi. Utakumbuka vilevile 2010 Makamba aliwazuia wagombea wa CCM kushiriki kwenye midalo, sidhani 2015 CCM watakuwa na jeuri hiyo. Kwa ufupi huko nyuma serikali na chama tawala vilikuwa vinafanya vinalotaka na bila kujali.

Kinachoonekana sasa ni kuwa serikali imegundua bila kufanya kazi kwa bidii na kuwatumikia na kuwaheshimu wananchi hali yake itaendelea kuwa mbaya. Serikali imeamka kutokana na kazi kubwa ambayo Chadema wamefanya kuwaamsha Watanzania ambao wametuma salaam CCM kuwa tunataka utendaji. ili Tanzania ipige hatua tunahitaji kuwa na vyama vikubwa viwili vyenye ushindani wa kweli. Vile vile ni muhimu katiba mpya ikaruhusu kuwepo kwa ushindani wa kweli kwenye siasa.

Naamini historia mpya imeandikwa Tanzania na hapana shaka kuwa mambo hayatakuwa kama zamani tena na haya kwa maoni yangu ndio mafanikio ya nguvu ya umma na Chadema ambayo yameshaingia kwenye historia ya nchi yetu. Mungu ibariki Tanzania
 
no, inabidi watoke wao ndo wawe chama cha upinzani
 
Back
Top Bottom