Mafanikio ya EWURA katika kushusha bei za mafuta

K

kalulukalunde

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Messages
1,056
Likes
1,067
Points
280
K

kalulukalunde

JF-Expert Member
Joined May 27, 2016
1,056 1,067 280
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ilianza kazi zake za udhibiti mwaka 2006 ikiwa na jukumu kubwa la kusimamia kikamilifu sekta za nishati na maji ambapo katika kipindi cha miaka 10 mamlaka hiyo imewezesha kuwepo mafanikio makubwa katika sekta ya mafuta.

Hata hivyo miongoni mwa mafanikio makubwa ya EWURA ni kuweza kudhibiti bei ya mafuta nchini ambapo ndicho kilikuwa kilio kikubwa cha watumiaji wa huduma hiyo ambayo inagusa moja kwa moja maisha ya wananchi wa hali ya chini. Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo, anasema mafanikio yaliyopatikana kwenye sekta ya mafuta ni pamoja na mamlaka hiyo kufanikiwa kudhibiti bei ya mafuta nchini, ambapo anasema Tanzania ni moja kati ya nchi zinazoagiza nishati ya mafuta yaliyosafishwa kutoka nje.

Hivyo udhibiti wa bei za mafuta nchini ni moja ya jukumu la EWURA ambalo walianza kulitekeleza rasmi mwaka 2009. Sababu za kuanza kudhibiti bei ni ile hali ya kushindwa kwa nguvu za soko kudhibiti bei katika mazingira ya soko huria iliyotokea mwaka 2008, ambapo bei za mafuta katika soko la dunia zilipanda ghafla hadi kufikia wastani wa dola za Kimarekani 140 kwa pipa la mafuta ghafi. Wakati bei ya mafuta ilipokuwa ikipanda katika soko la dunia na bei ya mafuta hapa nchini ilikuwa ikipanda pia.

Anasema kuanzia Septemba, 2008 bei ya mafuta katika soko la dunia zilianza kushuka na kufikia wastani wa dola za Kimarekani 40 kwa pipa la mafuta, lakini kampuni za mafuta nchini hazikushusha bei za mafuta kwa wepesi na uwiano ule ule wa bei za soko la dunia. EWURA kwa kuliona hilo iliingilia kati na kuandaa kanuni ya ukokotoaji wa bei za mafuta nchini mwaka 2009. Lengo kuu la kanuni hii ilikuwa ni kudhibiti bei za mafuta nchini.

“Hivi tulipanga bei kwa mara ya kwanza ikashuka kutoka Sh 2,200 kwa Dar es Salaam hadi kufikia Sh 1,140. Hiyo ilikuwa Januari 6, 2009.” Kimsingi, tangu EWURA iingilie kati mwaka 2009, bei haijawahi kufikia ile iliyokuwepo Desemba 2008 wakati wafanyabiashara walipokuwa wakibadilisha bei kwa kuangalia kwenye mtandao na bei zilikuwa zikibadilika mara tatu hadi nne kwa siku moja kana kwamba ni maduka ya kubadilishia fedha.

Kuhusu udhibiti wa ubora wa mafuta anasema takwimu zinaonesha kuwa kiwango cha uchakachuaji wa mafuta kimepungua kutoka asilimia 78 mwaka 2007 hadi kufikia chini ya asilimia 4 kipindi cha mwisho cha mwaka wa fedha 2015/16. EWURA inaendelea na jukumu la kusimamia na kudhibiti ubora wa bidhaa za mafuta ya petroli yanayouzwa nchini kwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara na wa kushtukiza nchi nzima kuhakikisha kuwa tatizo la uchakachuaji linapungua sana, kama siyo kuisha kabisa.

Kaguo anasema mafuta yasiyokidhi viwango stahiki huleta athari kiafya, uharibifu wa mazingira na husababisha ushindani usio sawa miongoni mwa wafanyabiashara ambapo EWURA huchukua sampuli za mafuta kutoka miundombinu mbalimbali ya mafuta ambayo ni pamoja na maghala ya kuhifadhia mafuta, malori ya kusafirishia mafuta na vituo vya mafuta ili kupima ubora wa sampuli hizo.

Aidha, EWURA inatumia teknolojia ya kisasa ya kuweka vinasaba ili kudhibiti uchakachuaji na uuzwaji wa mafuta yasiyolipiwa kodi, mafuta yanayoweza kuingizwa kutoka nchi jirani kwa magendo na yale yanayosafirishwa kwenda nchi za jirani kupitia hapa nchini ili yasiuzwe katika soko la hapa nchini, hali ambayo ikiachwa huweza kuikosesha serikali mapato, kudidimiza uchumi na kuwa na ushindani usio sawa katika soko.

Anasema wafanyabiashara wanaokutwa wakiuza mafuta yasiyokidhi viwango stahiki huchukuliwa hatua stahiki za kisheria ikiwemo; kufungiwa miundombinu husika, kuwatoza faini na kuitaarifu Mamlaka ya Mapato (TRA) ili walipe kodi stahiki kwa wale wanaobainika kukwepa kodi. Kuhusu mafanikio ya kuanzishwa kwa mfumo wa uletaji mafuta kwa pamoja ambao Ewura iliuanzisha, Kaguo anasema ulianza Januari 2012 baada ya waziri mwenye dhamana ya masuala ya mafuta nchini kutoa kanuni za usimamizi wa uagizaji mafuta kwa pamoja.

Hatua hiyo ilikuja baada ya EWURA kumpatia kazi mshauri mwelekezi ambaye alifanya utafiti na kupendekeza utaratibu huu, baada ya kuonekana kuna msongamano mkubwa wa meli katika Bandari ya Dar es Salaam ambao ulisababisha kuongezeka kwa gharama za bei za mafuta nchini kutokana na ucheleweshaji wa meli kushusha mafuta.

Anasema kwa mujibu wa sheria ya petroli na kanuni, mafuta yote kwa ajili ya mahitaji ya soko la ndani ni lazima yaagizwe kwa kufuata mfumo huu wa uagizaji na kwa mafuta ya nje nao wanaruhusiwa kutumia mfumo huo, lakini si lazima, hivyo kuruhusiwa kuagiza nje ya mfumo. Mara tu mfumo huu ulipoanza faida moja kubwa iliyoonekana mara moja ni kupungua kwa gharama za ucheleweshaji wa meli bandarini kutoka wastani wa siku 45 meli kusubiri kushusha mafuta hadi kufikia wastani wa siku tatu.

Hii ina uhusiano wa moja kwa moja na bei za mafuta nchini, kwani gharama hizi za ucheleweshaji wa meli huwekwa kwenye kanuni ya kukokotoa bei za mafuta. Suala lingine ni gharama ya meli moja kuchelewa kushusha ni dola za Kimarekani 20,000 kwa tani kwa siku kwa meli zinazoshusha kwenye gati la Kurasini (KOJ) na dola za Kimarekani 23,000 kwa tani moja kwa siku kwa meli zinazoshusha kwenye boya kubwa la Kigamboni (SBM).

Pia mfumo huo wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja hutumia ushindani wa kimataifa ili kumpata mshindi wa uletaji mafuta nchini. Kampuni hushindana kwa gharama za usafirishaji na ‘premium’ kwa kila zabuni. Faida ambayo imeonekana kwenye utaratibu huu ni kupungua kwa gharama za usafirishaji na ‘premium’. Gharama hizi huwa zina uhusiano wa moja kwa moja na bei za mafuta nchini. Aidha kupungua kwa gharama hizi husababisha kupungua kwa bei za mafuta katika soko la ndani.

Zabuni zilizokwishatangazwa za uletaji mafuta tangu ianze ni zabuni 56 hadi kufikia Septemba 2016. Kati ya hizo zabuni, gharama za usafirishaji na ‘premium’ zimepungua kwa mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa. Pia kupitia mfumo huu, ubora wa mafuta unadhibitiwa kiurahisi zaidi ikilinganishwa na hapo awali kwani mafuta huagizwa kutoka sehemu moja ikilinganishwa na kipindi cha nyuma ambapo kila kampuni iliweza kuagiza mafuta yake yenyewe kutoka sehemu tofauti tofauti.

Hii ilisababisha udhibiti wa ubora wa mafuta kuwa mgumu. Kwa sasa kila meli yenye shehena ya mafuta inapowasili nchini, mafuta yote yanapimwa ubora ili kuhakiki kama yanakidhi viwango vya ubora vilivyopitishwa na Shirika la Viwango la Taifa (TBS), kama yanakidhi viwango basi meli huruhusiwa kupakua shehena hiyo ya mafuta.
 
IamHumble

IamHumble

Senior Member
Joined
Dec 4, 2016
Messages
137
Likes
41
Points
45
IamHumble

IamHumble

Senior Member
Joined Dec 4, 2016
137 41 45
Ewura japo ina ufisadi kiasi, ni moja ya Taasisi zinajojitahidi kutekeleza majukumu yake ya kila siku.
 
C

CHAZA

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Messages
7,147
Likes
2,705
Points
280
C

CHAZA

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2012
7,147 2,705 280
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) ilianza kazi zake za udhibiti mwaka 2006 ikiwa na jukumu kubwa la kusimamia kikamilifu sekta za nishati na maji ambapo katika kipindi cha miaka 10 mamlaka hiyo imewezesha kuwepo mafanikio makubwa katika sekta ya mafuta.

Hata hivyo miongoni mwa mafanikio makubwa ya Ewura ni kuweza kudhibiti bei ya mafuta nchini ambapo ndicho kilikuwa kilio kikubwa cha watumiaji wa huduma hiyo ambayo inagusa moja kwa moja maisha ya wananchi wa hali ya chini. Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo, anasema mafanikio yaliyopatikana kwenye sekta ya mafuta ni pamoja na mamlaka hiyo kufanikiwa kudhibiti bei ya mafuta nchini, ambapo anasema Tanzania ni moja kati ya nchi zinazoagiza nishati ya mafuta yaliyosafishwa kutoka nje.

Hivyo udhibiti wa bei za mafuta nchini ni moja ya jukumu la Ewura ambalo walianza kulitekeleza rasmi mwaka 2009. Sababu za kuanza kudhibiti bei ni ile hali ya kushindwa kwa nguvu za soko kudhibiti bei katika mazingira ya soko huria iliyotokea mwaka 2008, ambapo bei za mafuta katika soko la dunia zilipanda ghafla hadi kufikia wastani wa dola za Kimarekani 140 kwa pipa la mafuta ghafi. Wakati bei ya mafuta ilipokuwa ikipanda katika soko la dunia na bei ya mafuta hapa nchini ilikuwa ikipanda pia.

Anasema kuanzia Septemba, 2008 bei ya mafuta katika soko la dunia zilianza kushuka na kufikia wastani wa dola za Kimarekani 40 kwa pipa la mafuta, lakini kampuni za mafuta nchini hazikushusha bei za mafuta kwa wepesi na uwiano ule ule wa bei za soko la dunia. Ewura kwa kuliona hilo iliingilia kati na kuandaa kanuni ya ukokotoaji wa bei za mafuta nchini mwaka 2009. Lengo kuu la kanuni hii ilikuwa ni kudhibiti bei za mafuta nchini.

“Hivi tulipanga bei kwa mara ya kwanza ikashuka kutoka Sh 2,200 kwa Dar es Salaam hadi kufikia Sh 1,140. Hiyo ilikuwa Januari 6, 2009.” Kimsingi, tangu Ewura iingilie kati mwaka 2009, bei haijawahi kufikia ile iliyokuwepo Desemba 2008 wakati wafanyabiashara walipokuwa wakibadilisha bei kwa kuangalia kwenye mtandao na bei zilikuwa zikibadilika mara tatu hadi nne kwa siku moja kana kwamba ni maduka ya kubadilishia fedha.

Kuhusu udhibiti wa ubora wa mafuta anasema takwimu zinaonesha kuwa kiwango cha uchakachuaji wa mafuta kimepungua kutoka asilimia 78 mwaka 2007 hadi kufikia chini ya asilimia 4 kipindi cha mwisho cha mwaka wa fedha 2015/16. Ewura inaendelea na jukumu la kusimamia na kudhibiti ubora wa bidhaa za mafuta ya petroli yanayouzwa nchini kwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara na wa kushtukiza nchi nzima kuhakikisha kuwa tatizo la uchakachuaji linapungua sana, kama siyo kuisha kabisa.

Kaguo anasema mafuta yasiyokidhi viwango stahiki huleta athari kiafya, uharibifu wa mazingira na husababisha ushindani usio sawa miongoni mwa wafanyabiashara ambapo ewura huchukua sampuli za mafuta kutoka miundombinu mbalimbali ya mafuta ambayo ni pamoja na maghala ya kuhifadhia mafuta, malori ya kusafirishia mafuta na vituo vya mafuta ili kupima ubora wa sampuli hizo.

Aidha, Ewura inatumia teknolojia ya kisasa ya kuweka vinasaba ili kudhibiti uchakachuaji na uuzwaji wa mafuta yasiyolipiwa kodi, mafuta yanayoweza kuingizwa kutoka nchi jirani kwa magendo na yale yanayosafirishwa kwenda nchi za jirani kupitia hapa nchini ili yasiuzwe katika soko la hapa nchini, hali ambayo ikiachwa huweza kuikosesha serikali mapato, kudidimiza uchumi na kuwa na ushindani usio sawa katika soko.

Anasema wafanyabiashara wanaokutwa wakiuza mafuta yasiyokidhi viwango stahiki huchukuliwa hatua stahiki za kisheria ikiwemo; kufungiwa miundombinu husika, kuwatoza faini na kuitaarifu Mamlaka ya Mapato (TRA) ili walipe kodi stahiki kwa wale wanaobainika kukwepa kodi. Kuhusu mafanikio ya kuanzishwa kwa mfumo wa uletaji mafuta kwa pamoja ambao Ewura iliuanzisha, Kaguo anasema ulianza Januari 2012 baada ya waziri mwenye dhamana ya masuala ya mafuta nchini kutoa kanuni za usimamizi wa uagizaji mafuta kwa pamoja.

Hatua hiyo ilikuja baada ya Ewura kumpatia kazi mshauri mwelekezi ambaye alifanya utafiti na kupendekeza utaratibu huu, baada ya kuonekana kuna msongamano mkubwa wa meli katika Bandari ya Dar es Salaam ambao ulisababisha kuongezeka kwa gharama za bei za mafuta nchini kutokana na ucheleweshaji wa meli kushusha mafuta.

Anasema kwa mujibu wa sheria ya petroli na kanuni, mafuta yote kwa ajili ya mahitaji ya soko la ndani ni lazima yaagizwe kwa kufuata mfumo huu wa uagizaji na kwa mafuta ya nje nao wanaruhusiwa kutumia mfumo huo, lakini si lazima, hivyo kuruhusiwa kuagiza nje ya mfumo. Mara tu mfumo huu ulipoanza faida moja kubwa iliyoonekana mara moja ni kupungua kwa gharama za ucheleweshaji wa meli bandarini kutoka wastani wa siku 45 meli kusubiri kushusha mafuta hadi kufikia wastani wa siku tatu.

Hii ina uhusiano wa moja kwa moja na bei za mafuta nchini, kwani gharama hizi za ucheleweshaji wa meli huwekwa kwenye kanuni ya kukokotoa bei za mafuta. Suala lingine ni gharama ya meli moja kuchelewa kushusha ni dola za Kimarekani 20,000 kwa tani kwa siku kwa meli zinazoshusha kwenye gati la Kurasini (KOJ) na dola za Kimarekani 23,000 kwa tani moja kwa siku kwa meli zinazoshusha kwenye boya kubwa la Kigamboni (SBM).

Pia mfumo huo wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja hutumia ushindani wa kimataifa ili kumpata mshindi wa uletaji mafuta nchini. Kampuni hushindana kwa gharama za usafirishaji na ‘premium’ kwa kila zabuni. Faida ambayo imeonekana kwenye utaratibu huu ni kupungua kwa gharama za usafirishaji na ‘premium’. Gharama hizi huwa zina uhusiano wa moja kwa moja na bei za mafuta nchini. Aidha kupungua kwa gharama hizi husababisha kupungua kwa bei za mafuta katika soko la ndani.

Zabuni zilizokwishatangazwa za uletaji mafuta tangu ianze ni zabuni 56 hadi kufikia Septemba 2016. Kati ya hizo zabuni, gharama za usafirishaji na ‘premium’ zimepungua kwa mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa. Pia kupitia mfumo huu, ubora wa mafuta unadhibitiwa kiurahisi zaidi ikilinganishwa na hapo awali kwani mafuta huagizwa kutoka sehemu moja ikilinganishwa na kipindi cha nyuma ambapo kila kampuni iliweza kuagiza mafuta yake yenyewe kutoka sehemu tofauti tofauti.

Hii ilisababisha udhibiti wa ubora wa mafuta kuwa mgumu. Kwa sasa kila meli yenye shehena ya mafuta inapowasili nchini, mafuta yote yanapimwa ubora ili kuhakiki kama yanakidhi viwango vya ubora vilivyopitishwa na Shirika la Viwango la Taifa (TBS), kama yanakidhi viwango basi meli huruhusiwa kupakua shehena hiyo ya mafuta.
Nami kipekee niwapongeze EWURA kwa jitihada zao. Kwenye kila jambo la binadam lazima liwe na mapungufu, lakini kwa hapa lazima niwape hongera EWURA kwanza kwa kupunguza upandaji holela na pia kwa kupunguza uchakachazi hasa kwa mafuta yasiyokizi Vigezo
 
rushanju

rushanju

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2011
Messages
2,575
Likes
1,777
Points
280
Age
53
rushanju

rushanju

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2011
2,575 1,777 280
Kwa hayo maneno yooote hapo juu naona mnataka kuharalisha kupanda kwa bei keshokutwa..
 
M

massaiboi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2016
Messages
800
Likes
808
Points
180
Age
49
M

massaiboi

JF-Expert Member
Joined Jan 4, 2016
800 808 180
Mafuta yameshuka duniani kote sio issue ya ewura, ni soko la dunia lilivyo. Lakini pia hiyo ndio kazi yao so mtu hapongezwi kwa kutimiza wajibu wake ila kwa kufanya kitu cha ziada
 
Forum statistics

Threads 1,273,525
Members 490,428
Posts 30,484,172