Mafanikio ni kujitambua we ni nani na unatakiwa kufanya nini

Mnastar jr

Member
Dec 29, 2016
99
53
MAFANIKIO YA MAISHA SIO ELIMU TU, UTHUBUTU, KUJIAMINI NA UJASIRI WA MAAMUZI

✍Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa.

Katika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa ni wale wa "darasa la saba” au wale ambao hawakuingia darasani kabisa

Wasomi wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi na magari mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!)

Wapo wasomi wengi tu wanaoishi kimasikini, kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana

Lakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga

Hii inachangiwa na mambo mawili:-

I. Wameelimishwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli

Hata hivyo katika maisha ya kawaida hasa kwenye mchakato wa kutafuta hela, kujaribu na kukosea ni sehemu ya mafanikio

Kadiri unavyojaribu na kukosea mara nyingi ndivyo unavyojifunza na ndivyo nafasi ya kutajirika kwako inakuwa kubwa!

Wasomi wengi kwa sababu ya "mentality" ya kuogopa kukosea huwa hawapendi kujaribu biashara kwa hofu ya kushindwa kuiendesha, na huamua kufa kimasikini wakitegemea mishahara pekee kwa sababu mishahara ndio pato lao la uhakika

II. Madarasani kunahimizwa ubinafsi badala ya umoja. Angalia namna mitihani inavyofanyika. Kila mwanafunzi anafanya mtihani peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani!

Katika maisha ya kawaida hasa ya kusaka fedha, unahitajika ushirikiano mkubwa sana, baina yako na wadau, wateja, wafanyakazi wenzio, marafiki n.k. Kwa kifupi unatakiwa kuwa na Networking ya kutosha.

Huwezi kufika mbali kiuchumi kama utakuwa na "mentality" ya ubinafsi unaosisitizwa madarasani!

Simaanishi kusoma hakuna maana, isipokuwa ninakwambia: Kama ukipata nafasi ya kusoma, soma kwa bidii; lakini usibebe kila wanachokulisha madarasani; ukakileta huku mtaani

Mtaani panahitaji akili ambayo ni tofauti na hiyo iliyopimwa kupitia kukariri ya vitabuni, mwishoni wanakuzawadia makaratasi yaitwayo vyeti

Ukitaka kufanikiwa ungana na waliofanikiwa wakuelekeze

Hii habari haitaki hasira, vumilia tu na jiongeze
....hata mimi sijawa tajiri bado
 
Hapa kuna kitu kinaitwa fear of unkown, tuna hofia kisicho kuwepo na kuacha kuhofia kilichopo.

Ni kweli kwabia wasomi wengi huja kufa masikini na msomi akijitahidi sana atajenga nyumba na kununua Gari la kutembelea full stop.

Wasomi tunaogopa kijaribu, Tunaogopa kuchekwa, Tunaogopa.ndugu na jamaa watatuonaje sasa? Tunaogopa wake zetu/ waume/ wachumba watatuonaje sasa?

Tumebakia na biashara za part time za kuendesha kwa simu na unajikuta mshahara tena ndo wa kwenda kulipa shamba boy
 
Ni kweli Mkuu lazma tujulshane ukweli
Sema wat tz wavivu kusoma mkuu
Ukweli mtupu ulionena hapa. Asante kwa kuwakumbusha hao ma.......
 
Hivi kila mtu anahitaji kuwa tajiri??
Personally I don't envy extreme wealth, Napenda pesaa ndioo but sio too much
And some people js wanna have a house na gari ya kutembelea finished...
 
Hapa kuna kitu kinaitwa fear of unkown, tuna hofia kisicho kuwepo na kuacha kuhofia kilichopo.

Ni kweli kwabia wasomi wengi huja kufa masikini na msomi akijitahidi sana atajenga nyumba na kununua Gari la kutembelea full stop.

Wasomi tunaogopa kijaribu, Tunaogopa kuchekwa, Tunaogopa.ndugu na jamaa watatuonaje sasa? Tunaogopa wake zetu/ waume/ wachumba watatuonaje sasa?

Tumebakia na biashara za part time za kuendesha kwa simu na unajikuta mshahara tena ndo wa kwenda kulipa shamba boy
What if gari na hio nyumba ndo alichokuwa anataka maishani?,.hv ni kila mtu anataka utajiri?utajiri nao ni 'subjective'...tajiri wa mkoani akiletwa masaki ni average tuuu,..
 
Hapa kuna kitu kinaitwa fear of unkown, tuna hofia kisicho kuwepo na kuacha kuhofia kilichopo.

Ni kweli kwabia wasomi wengi huja kufa masikini na msomi akijitahidi sana atajenga nyumba na kununua Gari la kutembelea full stop.

Wasomi tunaogopa kijaribu, Tunaogopa kuchekwa, Tunaogopa.ndugu na jamaa watatuonaje sasa? Tunaogopa wake zetu/ waume/ wachumba watatuonaje sasa?

Tumebakia na biashara za part time za kuendesha kwa simu na unajikuta mshahara tena ndo wa kwenda kulipa shamba boy
Hii ni kweli Mkuu
 
Ni kweli wasomi wengi wanaogopa sana Asante kwa kukumbusha kutupa ujasiri mana mafanikio bila kujaribu hayaji tuu
 
Najivunia Kuwa Msomi,maana kwa Usomi wangu Matajiri wamenitafuta na Kunipa Fedha,zinazoendesha maisha yangu.Kwa shule niliyopiga Walipa Kodi wa Marekani,Uswiss na hata RSA nishawatumikia wakalipa.Wengi wetu Luna kitu hawajui,Matajiri wote miradi yao lazima walete wasomi kuisimamia.Pili hata serikali,mashirika ya Kidini,Vyama vya siasa vinawategemea wasomi kutimiza mambo yao.Ukiwa Tajiri,na Ukawa investor,kabla ya Kupata faida,wasomi wameshachukua chao mapema;kihalali,kama mishahara,posho,consulting fees nk.Hata ukipata loss,wao wana chao mfukoni.
Nimekuwa na Hisa za Mabenki kadhaa hapa Tz,ndiyo nikathibitisha kwamba kabla Bodi ya Wakurugenzi hawajavote kutupa gawio,wanajilipa kwanza!!
 
Vizuri Mkuu watu hawajui kutumia elimu zao kazi kujsifu ma degree nna PhD inakusaidiaje?
 
acha maneno mengi.. hakuna tajiri anaeshinda jamii forums

Back
Top Bottom