Mafanikio katika Maisha hayana siri

Mafanikio katika Maisha hayana siri

Watu wengi wanashindwa maisha kwa kutoijua siri moja kubwa sana.
Kukopa kusiko na manufaa yoyote kuko kwa aina nyingi na pengine mtu anaweza kujidai kwamba mimi sijawahi kukopa na mwingine anaweza kujitapa kuwa ni mkopaji mzuri lakini pia mikopo yake yote anailipa kwa wakati na hadaiwi, kumbe ndiye ana madeni makubwa yasiyolipika.

Mkopo mbaya sana ambao ndio unawadumaza wengi kwenye harakati za kujiletea maendeleo ni mkopo wa muda. Pengine swali la kujiuliza ni je mtu anakopaje muda?.

Mtu anakopa muda kwa kutofanya jambo au shughuli sahihi kwa wakati sahihi.
Mfano unakuta mtu anatakiwa asafiri leo kwa ajili ya kufuata bidhaa fulani mahali fulani kwa ajili ya matumizi au biashara zake,lakini anaamua kuahirisha safari bila sababu za msingi na kusema atasafiri kesho yake.

Tukumbuke maisha hayasimami wala hayamngoji mtu huyo. Kesho ikifika unatokea msiba kwa jirani au anapatwa na dharura nyingine mpya hivyo anashindwa kuondoka na hivyo bidhaa aliyokuwa anakusudia kuifuata anashindwa kuipita kwa muda huo na hata akiipata baadaye anakuta kuna mabadiliko mengi yametokea ndani ya muda mfupi hata kupelekea bidhaa hiyo kukosa manufaa aliyotarajia kuyapata.

Matokeo yake mtu huyo anarudi nyuma kimaisha kwa sababu tu alikopa muda.
Kimsingi jamii inatakiwa ielewe kwamba muda ni mali, hivyo kuukopa au kuupoteza bure unaweza kukusababishia kupata hasara kubwa.

Watanzania tujitahiti kutokopa muda na tuzingatie usemi usemao LINALOWEZEKANA LEO LISINGOJE KESHO .
Hii ndio siri ya mafanikio katika maisha.

Je, wewe hujawahi kukopa muda?
 
Tunatofautiana kwenye mambo mengi sana, lakini wote tunapata fursa sawa ya masaa 24, ni jukumu la kila mmoja wetu kuona anayatumia vipi hayo masaa. Jambo la msingi ni kuheshimu muda wako na muda wa wengine.
 
Habari za jioni wana JF.....
Labda Jamani niende kwenye mada
Hapa nazungumzia suala la mafanikio hususani mafanikio ya kiuchumi....

Kwa binafsi mpaka hapa nilipofikia Hali yangu kiuchumi kuna vitu niliacha kufanya mfano
- masuala ya kuhonga na starehe za ajabu mara club mara beach sijui mitoko kipindi nipo kijana miaka18-25 aisee vijana wenzangu wa rika langu kipindi kile walikua wananicheka sana na kuniona boya kijana wa kipare nilisave pesa...

God is great aisee kweli imani yako ndio itakayokuponya. .niliamini kuwa one day yes kwa kweli saivi licha ya kuwa na miaka 27 kwenda 28 lakini kwa mwezi uhakika milion 5 mpaka saba kama income yangu after tax ipo kama kawaida licha ya kupitia changamoto lukuki katika maisha...

Cha msingi weka malengo punguza matumuzi yasiyo ya lazima chapa kazi...utaona mafanikio aisee

Na sasa nina mpango wa kuongeza mashamba ya miti njombe ili after fews years Nijipatie pesa

Vijana maisha mapambano sio mchezo aisee...lazima upigike ili utoboe kama huna cha urithi Kwa baba au mama yaani family yenu

Hivyo kama na wewe una chochote kile cha kushare ili watu waone jinsi unavyoweza kufanikiwa funguka
 
Hongera mkuu..nidhamu ni muhimu
 
Hajaandika direct kwamba ndo siri ya mafanikio ila apo aliposema namna ya kujitofautisha na wengine ndo point zipo apo
Hahhaa...siri ya niniiii nini maana yake ooo...nimeelewa mzee mama

Big up sana kwa vijana wapambanaji kama mm,mtoa mada,ww mamushka wangu na wengine wengiii...1B ya Mo ilinivuruga wallah..
 
Back
Top Bottom