Mafanikio hayana uchawi soma hii itakusaidia kisha shusha comments

May 20, 2020
33
26
MAFANIKIO HAYANA UCHAWI NI KUMUOMBA MUNGU NA KUZINGATIA BAADHI YA MAMBO

Leo Apostle Jonathan Kamwavah ninakuletea somo kwa ufupi Sana linalosema:

VITU SABA AU MAMBO SABA YA KUACHA ILI UFANIKIWE KATIKA JAMBO LOLOTE LILE

1: PUNGUZA AU ACHA KABISA VISINGIZIO

Hapa namaanisha Kuna watu hawawezi kufanya Jambo mpaka waanze kutafuta visingizio, utasikia watu wenyewe watanielewa kweli, kwanza huko kwenyewe mbali, mmmh Mimi mfupi bhana, kwanza Sina hata nguo nzuri na visingizio kemkem.

2: FANYA YAKO WACHA KUFATILIA YA WATU AU KUFANYA KWA KUWARIDHISHA WATU
Hapa namaanisha Kuna watu hawawezi kufanya Jambo lao na kusimamia Mambo yao kikamilifu kutwa kucha wao nikufatilia wenzao wanafanya nini na kujifanya wanawasaidia watu katika Mambo yao wakati yakwao yamesimama na hakuna wa kuwasaidia katika yao,wakati huo muda unakwenda wakati unapita yako yanakwama. Tambuwa kuwa maisha Ni karatasi ya mtihani na kila mmoja anakaratasi yake na ina maswali tofauti kabisa na mwenzako hebu tumia muda mwingi kujibu maswali yako kwanza.

3: PUNGUZA KULALAMIKA AU ACHA KABISA KULALAMIKA
Hapa namaanisha Kuna watu ambao kila kukicha wao Ni kutoa malalamiko tuuu badala ya kupambana na vikwazo vinavyo wakabili wao nikulalamika tuuu,oooooh wazazi hawakunisomesha ndiyo maana Nina maisha magumu,oooh Mimi mtaji mkubwa Sina,ooooh vyuma vimekaza,ooooh Ndugu wamenitenga.Tambuwa Mtu mwenye mafanikio au asiye na mafanikio hutambulika kwa kufungua kunywa chake yani nini anazungumza na siyo Muonekano wa nnje.

4: ACHA TABIA YA KUJISTUKIA
Hapa namaanisha Kuna watu ambao hawawezi kufanya Jambo kwa kujiamini yani wao muda wote Ni kujistukia tuuu, mmmh nitaweza, watanielewa nikidondoka jeee? watanionaje? Ila wale wasomi Sana so watanizomea.Wewe jiamini fanya kwa bidii zako zote.

5: ACHA TABIA YA KUJILINGANISHA WALA KUJIFANANISHA
Hapana namaanisha Kuna watu ambao hawawezi kufanya bila kujilinganisha au kujifananisha na watu wengine, yani mwenzio kafungua duka la nguo nawe unakurupuka kufungua duka la nguo, Kuna walio pitiliza wanajilinganisha na kujifananisha sauti mpaka baadhi ya mienendo ya maisha na watu wengine, sikatazi kuiga yaliyo mazuri Ila katika kuiga yaliyo mazuri pia nivyema kusimama wewe Kama wewe.

6: USIOGOPE KUFELI
Hapa namaanisha Kuna watu ambao Ni woga Sana wa kufeli kitendo kinacho wapeleke kushindwa kufanya baadhi ya majambo ya msingi ambayo yange wainua na kufanikiwa, watu Hawa hujawa na woga Sana na kukosa uthubutu.Nakuambia nibole uthubutu hata ukifeli utakuwa umejifunza kwa kina na ukifanya tena huto feli tena.

7: USIPOTEZE MUDA MWINGI KUSUBIRI
Hapa namaanisha Kuna watu ambao hawawezi kufanya Jambo kwa wakati utasikia ili kesho, mara kesho, tusubiri kidogo haraka ya nini tutafanya wiki ijayo.Nisikilize nikwambie wakati Ni sasa inuka fanya sasa Kama Ni msaada utakukuta umekwisha Anza na msaada wenye tija huja katikati ya mapambano na siyo mwanzo wa mapambano.

KWA LEO NIISHIE HAPO MIMI NI APOSTLE JONATHAN LUCAS KAMWAVAH

Unaweza kuwasiliana nami kwa maombi, maombezi, maswali na ushauri kwa kupitia

EMAIL ADDRESS
jonathankamwavah@yahoo.com

jonathankamwavah111@gmail.com

PHONE NUMBER

+255716283823
+255687071261

HII NI KWELI YA MUNGU KWA WATU WOTE

*MAFANIKIO HAYANA UCHAWI NI KUMUOMBA MUNGU NA KUZINGATIA BAADHI YA MAMBO*

WOTE*
IMG-20200519-WA0010.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa tumekuelewa Apostle wetu! Ila na hayo mawasiliano yako hivi umeyaweka kwa ajili ya nini vileee!!?🤔
 
Jamaa amesaka mwanamke hadi amekosa sasa ameamua kuweka namba kabisa na picha,huo mtego lazima wajinga wanase,unamaana jamaa huko mtaani kwenu hakuna mwanamke?Duuh we mzimaa kwl?
 
Apostle unanyoa nywele kwa mtindo huo. Kwa picha yako tu, macho na sura sioni kama una vifungu vya biblia kichwani. Naona kama mtu flani hivi kama daredevil, mkorofi na aliyepitia harakati ngumu sana za maisha. Sasa sijui muda wa kusoma biblia kwa miaka kadhaa na kuwa competent ulipata vipi.
 
Back
Top Bottom