Wanaotajwa kwa urais
Ndani ya CCM, kinyanganyiro cha urais kinawahusisha wanasiasa vijana ambao umri wao ni kati ya miaka 40 na 50, wanasiasa wenye umri kati ya miaka 50 na 60 na kundi la wazee wenye umri zaidi ya miaka 60 ambao wametumikia nchi tangu uhuru.
Wanasiasa vijana wanaotajwa ni pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Emmanuel Nchimbi, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu, Mbunge wa Bumbuli, January Makamba na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye.
Katika kundi la umri wa kati wapo Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya, Waziri Mkuu aliyejiuzulu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk Asha-Rose Migiro.
Kundi hilo pia linawajumuisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe.
Katika kundi la wenye umri zaidi ya miaka 60 wanaotajwa ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta.
source:mwananchi