GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,866
- 11,100
Wanabodi,
Wananchi hawashibi barabara, ndege, madaraja au hospitali. Wananchi wanahitaji chakula na pesa mwaka huu 2020. Hili chama changu cha CCM ndio tunapaswa kulihubiri kwenye kampeni sasa"Maisha bora na maendeleo ya watu"
Mimi ni mwana CCM. Wakati huu wa kampeni sera ya maendeleo ya vitu inayohuburiwa na CCM imeshafeli kwa wananchi kwa sasa, watu wanahitaji pesa au hela mifukoni tu.
Sasa kila kiongozi wa CCM anajitetea na kujaribu kuunganisha kuwa ndege, barabara na madaraja ni maendeleo ya watu. Hii sio kweli wana CCM wenzangu.
Katika Economics vitu huongelea kwa pande mbili at Micro level (level ya familia au ya mtu mmoja mmoja) na Macro level (level ya kitaifa au mambo makubwa kubwa)
Sasa haya mabarabara na Mandege ni mambo makubwa ya kitaifa ambayo yameshindwa kuleta madhara kwa mtu mmoja mmoja au Familia kama ilivyotarajiwa
Wananchi wao wanahitaji mambo ya haraka haraka tu,Kwa sasa wananchi wengi maisha ni magumu kwao huo ndio uhalisia, Wanahitaji sera za maisha mazuri
Yafuatayo inabidi yafanyike na CCM mapema kuokoa jahazi:
Mosi, Kauli mbiu ya "Tunasonga Mbele Pamoja" inawakumbusha wananchi machungu ya maisha na hasira kuwa maisha yatazidi kuwa magumu zaidi. Hii kauli ibadilishwe mapema, itamkwe "Tunasonga Mbele na Maendeleo ya Watu"
Pili,Tundu lissu asijibiwe tunazidi kuharibu kabisa ,Tundu lissu ni mtu wa tactics anaanzisha jambo dogo mkijibu ndio anashambulia kwa makombora ambayo wananchi yanawakolea na kuwaingia.
Tundu lissu alichokifanya Zanzibar leo kwa kumuunga mkono Malim Seif wa ACT hili ni pigo na mtego kwa CCM. Hapa CCM ikimjibu ataleta mashambulizi wanayopenda wanzazibar kuwa zanzibar ni nchi na mambo ya serikali tatu. Akianza kuyaongelea mambo ya muungano ndio tutachakazwa kwa hoja kama Bunge la katiba na kujikuta tunatafuta hati za Muungano wakati wa JK.
Huu ndio ukweli mchungu hatuna uwezo wa kumjibu Tundu lisu kwa hoja. Tundu lissu Bunge la katiba ilifikia sehemu Waziri lukuvi alisema Tundu Lissu ana kamzizi ka ushawishi na kadawa kanakofanya watu wamsikilize.
CCM sasa muda bado tuanze kuelezea habari za maisha bora kwa wananchi kwa miaka mitano ijayo. Ajira zilizotolewa juzi za ualimu zimezima asilimia 50 ya hoja ya Lissu kuhusu elimu.