Maendeleo ya vitu yaliyojengwa kwenye madeni

Maendeleo ya vitu yaliyojengwa kwenye madeni

Hivi ujinga utawatoka lini?

Unajua long term items zinajengwa kwa mikopo ndio maana unasikia kuna mikopo ya nyumba, kuna hire purchase nk n.

Wewe mfano rent yako ni tshs 1m kwa mwezi , ukitaka kujenga si unaweza kuchukua mkopo na badala ya kulipa kodi ya panga ukawa unalipa deni la nyumba, hivyo ktk miaka 2 ukawa na nyumba lakini unalipa deni.

Sasa wewe hutaki hilo basi endelea kupanga nyumba

Tatizo ni riba kubwa.

Pili ni aina ya investment, pesa tulizokopa zinarudi nje zaidi kuliko kubaki humuhumu ndani

Tatu ujenzi wa miundo mbinu hiyo haiendi sambamba na kuboresha sector ambazo zingefeed miundo mbinu hiyo ili kumaximize faida za miundo mbinu hiyo!
 
Hujui hata kuandika ungesema baadhi vimejengwa kwa mikopo

Pili mikopo sio shida uwezo wa kulipa upo na return ya faida Ni kubwa

Barabara nyingi nzuri hufungua uchumi hivyo mapato ya Kodi kupngezeka hujui hilo?
Mfano enei lilikuwa halina barabara ukijenga magari yataanza kuitumia na yanatumia mafuta yanayolipiwa Kodi,gari za abiria zitaanza eneo Hilo biashara ya abiria inalipiwa Kodi . biashara nyingi zitafunguliwa zinazolipa Kodi

Kujua faida chukua mkopo uliokopa toa Kodi ulizokusanya kupitia hup mradi wa barabara kupitia components zote zilizopo hiyo barabara ndio utajua faida yake

Chadema uchumi mko zero ndio maana mnaandika ujinga . Chadema mna professor mmoja tu profesa Baregu Tena naye wa siasa

CCM tunao kibao wa kutushauri
Cha ajabu mnao wengi wa kuwashauri lakini wengi wa kuwaongoza mliwanunua CMS
 
Ujenzi wa reli na bwawa la umeme si dead investment cha msingi ni projects za umma zinapaswa kuwa wazi ktk utekelezaji wake
 
CCM kaeni tu pembeni mkajitathmini upya, waachieni wenye mawazo mbadala watutoe tulipokwama! Nyerere ndiye alistahili kukopa maana hakuchimba madini lakini serikali nyingine zimefanya hiki kitabia cha kukopakopa kuwa kama sehemu ya utamaduni wa nchi yetu! Hakuna mradi wa kutekeleza bila kukopa au kudhulumu makundi ya wanyonge! Leo hii serikali inasema inajivunia kuwekeza kwenye elimu bure ndo maana Kidoto cha sita wamefanya vizuri ilihali pesa walizodhulumiwa watumishi tangu mwaka wa fedha 2015/2016 ndizo zimesomesha hao watoto hivyo shukrani nyingi zinatakiwa kuwaendea watumishi wa umma walioteseka kwa miaka yote 5 kusomesha wanafunzi hao.
 
Mkuu nchi inajengwa kwa Kodi za watu wake na si mikopo.kodi inatoka kwa individuals na siyo kwenye mikopo.Hivyo nchi kujenga uwezo wa watu wake kuzalisha zaidi ndo maendeleo zaidi.kuinvest trions of money kwenye reli huku walimu hujawalipa,huku watoto wetu wakipata elimu mbovu haina tofauti na kukopa ukajenge nyumba
Hivi kisomo chako ni cha darasa la ngapi? Maana uelewa wako , umepitiliza wa chuo kikuu, sasa kama nchi inajengwa kwa kodi how comes USA wanamadeni????
Halafu tax base ya Tz ni ndogo kwa sababu kodi inakatwa kwenye formal sector only ambayo ni ndogo.
Lakini kwa jinsi uelewa wako ulivyo pitiliza ngoja nikuache
 
Mkuu marekani ilijengwa na itaendelea kuwa juu kwa kuwa elimu ni kiupaumbele Chao Cha kwanza
Naona uelewa wako umepitiliza sasa sijui tatizo shule uliopitia au wewe , Lakini kutokana na fact kwamba wapo wenye uelewa toka shule uliosoma , hivyo naona tatizo limo kwako.
Nitaendelea
 
Tunakopa Bayport na kuzikwepa bank sijui huyu bwana anatumiaga kiungo gani kufikiri
 
Hivi kisomo chako ni cha darasa la ngapi? Maana uelewa wako , umepitiliza wa chuo kikuu, sasa kama nchi inajengwa kwa kodi how comes USA wanamadeni????
Halafu tax base ya Tz ni ndogo kwa sababu kodi inakatwa kwenye formal sector only ambayo ni ndogo.
Lakini kwa jinsi uelewa wako ulivyo pitiliza ngoja nikuache
Mnashindwa kuinvest kwenye sector ya madini mnakimbilia kukopa..huu Ni uwendawazimu watawala wengi wa kiafrika especially CCM akili mgando sana wakishhaingia madarakani akili zinajaa tope
 
Hujui hata kuandika ungesema baadhi vimejengwa kwa mikopo

Pili mikopo sio shida uwezo wa kulipa upo na return ya faida Ni kubwa

Barabara nyingi nzuri hufungua uchumi hivyo mapato ya Kodi kupngezeka hujui hilo?
Mfano enei lilikuwa halina barabara ukijenga magari yataanza kuitumia na yanatumia mafuta yanayolipiwa Kodi,gari za abiria zitaanza eneo Hilo biashara ya abiria inalipiwa Kodi . biashara nyingi zitafunguliwa zinazolipa Kodi

Kujua faida chukua mkopo uliokopa toa Kodi ulizokusanya kupitia hup mradi wa barabara kupitia components zote zilizopo hiyo barabara ndio utajua faida yake

Chadema uchumi mko zero ndio maana mnaandika ujinga . Chadema mna professor mmoja tu profesa Baregu Tena naye wa siasa

CCM tunao kibao wa kutushauri
Mibarabara bila uzalishaji Ni bure, wekeze kwa watu ili watu wawe na maarifa ya kuzalisha na kuuza nje, vinginevyo hiyo Ni white elephant projects
 
Wewe mwenyewe mtoa post umekopa tala,songesha,nipige tafu,mpawa na bado hujalipa mpaka sasa.
Marekani nchi tajiri inadaiwa pesa ndefu na China,sembuse nchi kama Tanzania!!!.
Mkuu kukopa siyo dhambi,dhambi ni unakopa ili ufanye Nini?
 
Pamoja na mbwembwe za maendeleo ya miundombinu wametuondoa uchumi wa chini kati
 
Naona uelewa wako umepitiliza sasa sijui tatizo shule uliopitia au wewe , Lakini kutokana na fact kwamba wapo wenye uelewa toka shule uliosoma , hivyo naona tatizo limo kwako.
Nitaendelea
Mkuu nakuelewa sana,you know what,ninaposema elimu wewe unadhani ni vyeti same way anavyofikiri mwenyekiti wako.Ila Mimi simaanishi vyeti bali ujuzi na maarifa.Hivi vitu viwili ndo msingi wa kuongeza productivity.
 
Tutafika huko...

Tunaanza na mega investment...

Miaka yote uliyopunjwa yatalipwa pamoja...

Tuko kwenye mkakati na uchambuzi yakinifu kwenye madai ya watumishi...

Hatua tuliyofikia ni ya kulidhisha..

Vuta subraaaaa

Kidumuuuuuu[emoji3][emoji3]
Watanzania tunataka maendeleo ya vitu na watu yaende kwa pamoja. Maendeleo ya magufuli ni changamoto kwa Watanzania tulio wengi. Haiwezekani mtu mmoja tu aamue Wafanyakazi wanyimwe stahiki zao eti kisa ananunua ndege!

Mimi kama mfanyakazi tena niliyeko kijijini huku Tanganyika Masagati au Uchindile Wilayani Kilombero, hizo ndege zitanisaidia nini!! Ila ningepandishwa daraja kwa mujibu wa taratibu za kazi, ningeweza kukopa benki na kujenga kajumba ka kunisitiri, au kununua hata kapikipiki ka kunipeleka kazini.
 
Production kwa nchi isiyopitika ni nguvu za giza mkuu
Mkuu nakuelewa sana na hii ndo akili ya magu.ila kwa mfano huo ulioutoa ,watu wenye akili wangekopa ili kuwekeza kwenye production inayoongeza hicho kipato chako Cha 1m badala ya kukopa kuwekeza kwenye dead investment
 
Hivi kisomo chako ni cha darasa la ngapi? Maana uelewa wako , umepitiliza wa chuo kikuu, sasa kama nchi inajengwa kwa kodi how comes USA wanamadeni????
Halafu tax base ya Tz ni ndogo kwa sababu kodi inakatwa kwenye formal sector only ambayo ni ndogo.
Lakini kwa jinsi uelewa wako ulivyo pitiliza ngoja nikuache
Mkuu nchi zote duniani hazijengwi kwa mikopo bali Kodi za wananchi wake,kwa hiyo Kama tax base yetu ni ndo tunapaswa kujiuliza why tax base yetu ni ndogo,je watu wetu hawana shughuli maalum zinazowaongezea kipato? Kama zipo why hazilipi Kodi na Kama hazipo ni kwanini watu wetu hawawezi kutumia fursa zilizopo kutengeneza pesa? Watu wenye akili wangejiuliza maswali hayo na mengine Ila watu utopolo Kama ninyi mnakimbilia kukopa,Tena si kwamba mnakopa muwekeze kwenye sector zinachochea production bali ninyi mnakopa na kuwekeza kwenye showoff projects.Na kuhusu USA kuwa na deni hilo nadhani tuwaachie wachumia watusaidie,but what I know ni kwamba USA wanatusaidia sana Tanzania,wanatupa mikopo bali pia wanatupa pesa za bure. Sasa wanakopa ili watusaidie au wanakopa kwa kuwa wanaupungufu wa pesa hilo silijui,lakini pia najua USA ni wachangiaji wakubwa kule WB kule tulikoenda kukopa pesa ya mwendo kazi na flyover ya ubungo,kule tulikoenda kukopa pesa ya kuendeshea elimu yetu ya secondary.Lakini pia kitu ninachojua kuhusu USA ni kwamba raia wake wanachapa kazi sana,wanauelewa mpana wa Mambo mbalimbali,wanasafiri sana duniani na productivity yao ni kubwa sana na wanamfumo mzuri wa ulipaji Kodi.Kukwepa Kodi USA ni kosa lisilosameheka
 
Sasa mtoapost analaumu serikali kutumia fedha za mkopo kuboresha miundombinu ya nchi.
Mkuu hoja ni kuwa ukikopa ujenge nyumba wakati huzalishi ni sawa tu na hujajenga nyumba,you know what I mean?
 
Back
Top Bottom