Moto wa mabadiliko ndio nini?
ni harakati za kuelimisha wananchi wazifahamu haki zao na kuzisimamia na kutekeleza wajibu wao kama watanzania katika taifa lao kwa ajili ya maendeleoMoto wa mabadiliko ndio nini?
Kwa niaba ya M/kiti wa CDM Wilaya ya Njombe (mkoa mpya wa Njombe) napenda kuwafahamisha wapenda mabadiliko wote hasa wapenzi, wanachama, mashabiki wa CDM na wananchi kwa ujumla kwamba tunaendelea vizuri na kazi ya kusambaza moto wa mabadliko kama yalivyoasisiwa na Mh Thomas Nyimbo.
Wale wenye kumbukumbu mtakumbuka kuna siku nilileta hapa mada inayoeleza jinsi Mh. Nyimbo alivyojitolea kwa hali na mali kuwasha moto wa mabadiliko. Kwa hakika tumefanikiwa sana kwa ngazi ya jimbo la Njombe Magharibi na sasa tumeunganisha juhudi na Majimbo mengine ya Njombe kusin na Kaskazini. Kuanzia mwezi wa pili (Februari) tunatarajia kuwasha moto kuelekea LUDEWA na MAKETE kwa msaada mkubwa wa Mh. Nyimbo ili hatimaye mkoa wa Njombe uwe na nguvu kama ile ya Mwanza, Mbeya, Iringa, Arusha na Kilimanjaro.
OMBI MAALUM
Kama yupo mwanaJF anaweza kutusaidia contacts za mtu yeyote wa Makete na Ludewa tunaomba tafadhali sana atusaidie kabla ya Jumapili ya wiki hii ili tuwasiliane naye mapema iwezekanavyo. Tumefikia hatua hii baada ya jitihada zetu kuelekea kukwama. Tafadhali kama unayo namba ya mtu au watu au wewe mwenyewe tujulishe kupitia 0789149165 (M/Kiti CDM Njombe (W) au mgosa81@yahoo.com.
Tunawashukuru sana kwa support yenu
Hakuna kulala.........
Posted by Kiongozi
....kwanza nimefurahi sana kwa harakati hizo ambazo mpenda maendeleo yeyote yule lazima akubali jitihada mnazofanya kuwa zina maana kwa taifa hili! Nilisikitika sana sana eti kuona Mh.Mkinda na Deo Filikunjombe wanapita bila kupingwa? wapi Demokrasia mkoa wa Njombe? Yes, wananchi wetu Njombe wanahitaji elimu ya kutosha juu ya Demokrasia ya kweli!
Juu ya ombi lako, hapo niliopohighlight, je, unahitaji contact za mtu YEYOTE yule? hata akiwa ni adui yenu? au unataka contact za mwanaharakati wa maeneo hayo? Kuna vijana hapa kama Fidel & Teamo wanaweza saidia sana hapa....!
Hujui? endelea kusoma post utaelewa tu usijifanye mtoto wa nurseryMoto wa mabadiliko ndio nini?
ni harakati za kuelimisha wananchi wazifahamu haki zao na kuzisimamia na kutekeleza wajibu wao kama watanzania katika taifa lao kwa ajili ya maendeleo
Nafikiri anahitaji wanaharakati hao, sasa Fidel na Teamo contact zao angepewa kama wazijua ili awasiliane nao,au vije GERARD????
....kwanza nimefurahi sana kwa harakati hizo ambazo mpenda maendeleo yeyote yule lazima akubali jitihada mnazofanya kuwa zina maana kwa taifa hili! Nilisikitika sana sana eti kuona Mh.Mkinda na Deo Filikunjombe wanapita bila kupingwa? wapi Demokrasia mkoa wa Njombe? Yes, wananchi wetu Njombe wanahitaji elimu ya kutosha juu ya Demokrasia ya kweli!
Juu ya ombi lako, hapo niliopohighlight, je, unahitaji contact za mtu YEYOTE yule? hata akiwa ni adui yenu? au unataka contact za mwanaharakati wa maeneo hayo? Kuna vijana hapa kama Fidel & Teamo wanaweza saidia sana hapa....!
.....ok ngoja niwa-PM hawa vijana hapa!
Nafikiri anahitaji wanaharakati hao, sasa Fidel na Teamo contact zao angepewa kama wazijua ili awasiliane nao,au vije GERARD????
Nipo mkuu ila Makete nina maza angu mdogo kanywa maji ya bendera ya kijani mpaka shuka anazo lalia rangi hiyo hiyo duh
Nashukuru sana. Kwa mujibu wa katiba ya CDM M/kiti wa Wilaya ni mjumbe wa baraza la uongozi la mkoa. Kwa hiyo wakati wa uchaguzi wa ndani ya chama wa mwaka 2009 wilaya za Ludewa na Makete zilihesabiwa kuwa hazikuwa na uongozi rasmi. Ndivyo inavyojulikana hadi makao makuu. Hata hivyo tunatambua uwepo wa wakereketwa ambao walijitolea na wanaendelea kujitolea ikiwa ni pamoja na waliogombea Ubunge. Ushahidi wa hili ni kilichotokea Ludewa wakati wa uchaguzi mkuu.Hata hivyo mpango wetu ni kutengeneza uongozi rasmi utakaochaguliwa kikatiba toka ngazi ya chini mpaka mkoani ukihusisha wilaya zetu zote nne yaani wanging'ombe, Makete, Ludewa na NjNjombe. Tunaomba mawazo zaidi MkuuThanks mdau kwa juhudi mnazofanya kwa mkoa wetu mpya wa njombe. Ninachofahamu mie ni kuwa wilaya hizi zina uongozi kamili ambao kwa hakika contacts zao zipo cdm hq. Mkipata contacts mtaanzia hapo kuendeleza mapambano.
Mkuu makao makuu wanatoa support ingawa sisi tumeamua kuanza wenyewe ili mako makuu watakapokuja watukutuke tukiwa tunatembea sio tunatambaa. Kumbuka wametoa kadi zaidi ya 4000 na bendra zaidi ya 100 kitu ambacho ni kinatusaidia sana hasa kwa kuanzia. Kuhusu Mkoa wa Iringa mimi na M/kiti wangu wote kikatiba tulikuwa viongozi wa mkoa wa Iringa (Wajumbe wa baraza la uongozi wamkoa) tatizo ni kwamba Wilaya hizo mbili pamoja na Jimbo la Njombe magh yalikuwa ni maeneo ambayo yalikuwa inactive kwa miaka mingi. HATA HIVYO HABARI NJEMA NI KWAMBA JANA MARA YA KUPOST MADA HII TULIPATA CONTACTS ZA WATU WA MAKETE BADO LUDEWA HATUJAPATA KABISAHongereni.
Concern yangu hapa ni kama hatujaona mchango wa CDM makao makuu katika hizi jitihada. Naamini kama hizo contacts si ajabu ingekuwa rahisi kuzipata kwa ushirikiano na na uratibu kutoka makao makuu mpaka ngazi ya mkoa in this case nadhani mngehitaji kushirikiana na viongozi wa mkoa wa iringa kwani ndio mkoa wenu wa njombe ulipotokea.
Nawatakia kila la kheri
Aisee mkuu upo juu. Ulembwe na Makoga ni baadhi ya vijiji ambavyo watu wake wanasupport sana mabadilikoNimesha msoma moto wa mabadiliko unaanzia Ruhuji, Ramadhani, Ulembwe, Usalule, Makoga-Ikonda- Makete