Maendeleo kwa vijana wa taifa hili

Imphuvyi

JF-Expert Member
Aug 6, 2018
224
151
Habari wananzengo,,
Naomba kwa wenye uwezo wa kufikisha taarifa kwa wahusika wawaambie waliangalie upya swala la maendeleo kwa vijana wa taifa hili. Unakuta kijana Ana taaluma nzuri tu, lakini hana mtaji.

Akienda kutaka msaada kwenye asasi za mikopo kigezo namba moja ni Awe na Mali isiyohamishika hapo inazungumziwa nyumba.

Sasa jamani kijana ndio kwanza ametoka shule, shule yenyewe alisoma kwa mkopo, hiyo nyumba anaitoa wapi??

Wenye sauti tusaidieni kuwasilisha hoja.
 
Hii ya Halimashauri
Halimashauri haiwezi kufanya chochote bila serikali kuu kuamua.

Wangeweka utaratibu kwa hizi tasisi za kifedha zinazoendeshwa na serikali, wakaweka namna rafiki kwa vinaja wasiyo na dhamana kuweza kukopesheka, ili wajiendeleze kuliko kutuacha tukizagaa mtaani, huku tukingojea ajira ambazo hazipo.
 
Niseme tu hujanielewa
 
Anyway, anaejua taasisi inayokopesha bila kigezo cha dhamana ya nyumba au kiwanja anitonye.
 
Maisha ni vita, na maisha ni ya kwako; nachoweza kukushauri, kama una wazo la biashara ambalo lina tija, unaweza kukutana na muajiriwa yeyote mwenye sifa ya kukopesheka, yeye akawekeza fedha, na wewe ukawekeza muda ili mwisho wa siku muweze kugawana faida (2/3 kwa 1/3).​
 
Back
Top Bottom