Maendeleo kinyumenyume | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maendeleo kinyumenyume

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mweongo, Aug 23, 2010.

 1. m

  mweongo Member

  #1
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 23, 2010
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu Watanzania, napenda kungia kwenye jukwaa hili kwa kujiuza hivi Taifa letu linaendelea kweli au tunarudi nyuma bila kujijua?

  Kwanza kabisa najiuza Tunajenga miji ya aina gani? Inasikitisha ukiangalia hali ilivyo katika Jiji la DSM, Arusha na mingine. Hivi viongozi wetu hali hii hawakeri? Viongozi hawa akiwemo mkuu wanchi, wanasafiri nje kila kukicha, hivi hawaoni miji ya wenzao ikoje wakaiga. wataalamu wa mipango miji wakowapi sheria ziko wapi tatizo linazidi kukua na linaachiwa liendele.Tufike mahali tuseme inatosha, sheria ziwepo na zisimamiwe. Nchi inaendeshwa kihunihuni kila mtu anafanya anavyotaka. Kwa mfano hapa Arusha watu wanatabia ya kukata viwanja kwenye mashamba yao kwa kipimo cha 'room' ukitaka room 1 au 2 unakatiwa sehemu inayolingana na unachotaka kujenga au uwezo wako. Barabara hakuna hata njia ya mguu ni shida. Tukiendelea na hali hii baada ya miaka 50 au 100 nchi itakuaje? Utashanga sehemu walizojenga wazungu tangu enzi za ukoloni ndio nzuri; Upanga, Oysterbay nk. Hata kuiga na kuendeleza walichofanya wazungu tumeshindwa!! Angalia Manzese Buguruni, Gongolamboto Kimara Sinza. Viongozi wetu wanajua wanaona lakini hawachukui hatua.

  Kwa upande mwingine naona watanzania hawaheshimu fedha zao. Mfano mtu anajenga kwenye hifadhi ya barabara baada ya muda anabomolewa au mtu anajenga nyumba ya mamilioni sehemu ya ajabu hata akitaka kuza hawezi kurudisha hata nusu ya gharama alizotumia. Je huu si ni ufisadi.

  Kitu kingine kinacho nikera ni Swala la elimu. Naona viongozi hawatendei haki watoto wetu na hasa wale wanaosoma shule za Kayumba. Wameazisha utitiri wa shule, hazina walimu hazina vifaa, hata wakiwepo walimu hawana taaluma ya kutosha kuwapa woto. kinachotokea ni mzunguko wa ujinga. Kwanini shule zisingejengwa kwa amwamu kulingana na uwezo zikato wahitimu wachache lakini bora, kuliko ilivyo sasa. Mtoto anamaliza Kidato cha 4 hawezi kuandika barua. Hivi tunajenga Taifa la namna gani? lakini sishangai maana wabunge wanapitisha bajeti ya elimu ya kayumba pale bungeni wakati watoto wao hawasomi huko, hivyo hawana uchungu! nasema 'this is a time bomb'.

  Nataka kumaliza lakini nina machungu mengi. Kweli miaka 50 tangu tupate uhuru wakina mama wanaojifungua wanalala wawili wawili kitandani au chini. hivi hatuwezi kununua vitanda au kujenga wodi za kutosha? Mbona magari ya kifari tunaweza kununua!

  Miondo mbinu: Mjerumani aliweza kujenga reli miaka hiyo sisi tumeshindwa hata kuisimamia licha ya kushindwa kujenga reli mpya. Usafiri wa reli ndio wa uhakika na salama zaidi kuliko barabara. tungelenga kuwa na mtandao wa reli nchi nzima.

  Hivi kuna haja gani ya kuanzisha mikoa na wilaya mpya na majimbo ya uchaguzi. vitu hivi vina mnufasha nani? swala la kugawa nchi lingesimamiwa na bunge tofauti na ilivyo sasa ambapo wakubwa wanafutia kazi jamaa zao kwa kuanzisha wilaya mpya. kwani hiyo fedha isitumike Kuhudumia mashule na hospitali? Lingine kunasababu gani ya kujaza bunge kwa wabunge wa viti maalum. fedha inoyotumika kuwalipa engeelekezwa kenye mashule na hospitali.

  Tufike mahali tuwe na mjadala wa kitaifa, tuangalie mambo ambayo ni ya msingi kwa taifa letu kuliko ilivyo sasa.

  Hivi nikweli watanzania hawahawa wanaolala chini hospitali watoto wao wanapewa elimu isiyo elemu ndio wanashabikia na kuitukuza CCM!?
   
 2. Homo Habilis

  Homo Habilis Senior Member

  #2
  Aug 23, 2010
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 189
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0


  Exactly ndio wenyewe mkuu.! wala usitafute mchawi.
   
 3. Xuma

  Xuma JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 631
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Hivi kwa nini watanzania hatujifunzi jamani kutokana hali halisi? Inasikiisha kusikia kuwa kuna watu eti wana imani na serikari ya JMK
   
Loading...