Maendeleo bila ya Haki na Sheria siyo maendeleo

Sijali

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
2,589
1,679
Habari Wanajamvi,

Ili maendeleo yadumu, yaheshimiwe na yathaminiwe, ni lazima yaambatane na uadilifu, Sheria na Haki.

Maendeleo yeyote yanayofikiwa kwa ukiukaji mkubwa wa haki za raia, ni rahisi sana kubomolewa, na mwenyewe aliyeyaleta kusahauliwa katika jaa la historia.

Ipo mifano mingi duniani, lakini ninaoufikiria karibu ni ule wa Iran na Iraq. Watawala wa nchi zote hizi, Shah Pahlavi na Saddam Hussein, walishindana katika nyakati tofauti kuleta maendeleo makubwa na ya haraka katika nchi zao.

Maendeleo ya vitu. Isipokuwa maendeleo hayo yaliambatana na ukiukwaji mkubwa wa aki za binadamu; mauaji, ukatili, mateso, wapinzani kupotezwa, kutoheshimu desturi, mila na dini.

Siku zote wakubwa hao walikuwa wakiwaambia raia kuwa lengo ni kuleta maendeleo! Matokeo yake, kwa Iran, ilifika wakati raia wakachoka wakaamua 'kuingia barabarani'. Kwa thamani kubwa ya uhai wao, wakajitolea hadi wakamwondoa Shah.

Naam, pamoja na maendeleo yake ama Iraq, Mtu wa nje alipojitokeza tu kuwasaidia kuondoa dhuluma, maelfu kwa maelfu ya Wairaq wakahiari kujiunga na mgeni huyo, badala ya kusimama kuipigania nchi yao. Kiasi kwamba walidiriki kumruhusu mgeni huyo kumkamata na kumchinja kiongozi wao aliyekuwa akiwaletea maendeleo.

Funzo katika hayo:

1- Maendeleo ni ya watu kwanza, si vitu
2- Maendeleo ni yale wayatakayo watu
3- Maendeleo yanayodumu lazima yaendane na uadilifu na haki
4- Ni kiongozi mwadilifu pekee ndiye anayeacha nyuma ukumbusho (legacy). Wengine, watasahauliwa.
5- Two wrongs do not make a right!
 
Back
Top Bottom