Maembe ya Kwetu Matamu - Yakidondoka Yenyewe!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,345
38,995
MAEMBE YA KWETU MATAMU, YAKIDONDOKA YENYEWE!
308225_10150300847911156_687191155_8581980_1131354866_a.jpg

Maembe yalodondoka yenyewe


Maembe yetu matamu, matamu yanipa hamu

Ladha yake ni adimu, yana vigezo muhimu,
Si machachu kama ndimu, yanataka utaalamu,
Maembe kweli matamu, yakidondoka yenyewe!

Hayahitaji vurugu, hayapopolewi mawe,
Ya Kisarawe na pugu, hata ya kule Kongowe,
Hata pwaguzi na pwagu, wanavyopata kiwewe
Maembe kweli matamu, yakidondoka yenyewe!

Si maembe ya kizungu, ni maembe ya kikwetu,
Utaapia kwa Mungu, ukila roho i kwatu,
Ni radhi nitiwe pingu, matamu madodo yetu,
Maembe kweli matamu, yakidondoka yenyewe!

Yanapokuwa mtini, mabichi yanavutia,
Yanini purukushani, kuiva yataivia,
Yabadilika rangi tawini, na harufu yavutia
Maembe kweli matamu, yakidondoka yenyewe!

Yatapigwa na upepo, kuringisha doli doli,
Yakining’inia kama popo, yapendeza kwelikweli,
Kisebu na kiroho papo, kitakupata kwa kweli
Maembe kweli matmu, yakidondoka yenyewe!

Subira yavuta kheri, yanapopoka yenyewe,
Wala hayataki shari, usiyarushie mawe,
Iwe shambani au pori, shika kikapu na wewe,
Maembe kweli matamu, yakidondoka yenyewe!

Anza kuyaokoteza, embe moja baada ya moja,
Ukipata la kupendeza, kwenye mamia ni moja,
Hilo siyo la kuuza, hilo ni embe la haja,
Maembe kweli matamu, yakidondoka yenyewe!

Nililosema nimesema, ya kwetu kweli matamu,
Hivyo kutama natama, nimezidiwa na hamu,
Moyo umeshanituma, nalila kama wazimu,
Maembe kweli matamu, yakidondoka yenyewe

M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji a.k.a Vuvuzela Matata)
 

The Finest

JF-Expert Member
Jul 14, 2010
21,615
5,966
MM Ngoja niangalie haya maembe ya huku mjini kwetu kama yanadondoka yenyewe baada ya kuiva au ndio hadi mtu ukatingishe mti ili yadondoke pamoja na kuwa yameiva
 

Globu

JF-Expert Member
Jan 12, 2011
8,376
1,792
Aahh unanikumbusha mbali. Maembe matamu yakidondoka yenyewe.
 

M-bongotz

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,729
387
Mwanakijiji umenena, tuseme nini tena
Embe kweli ni tamu, na haliishi hamu
iwe dodo, sindano, bolibo au ng'ong'o
Mradi limejiivia mtini, si kuvundikwa darini
Maembe kweli matamu,yakidondoka yenyewe
 

Mtalingolo

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
2,182
408
Hata mie nahamu, nipate japo sindano.
Yanantia wazimu, nilapo kwa mkono.
Maembe kweli matamu, yalo dondoka yenyewe
 

Mkwaruzo

JF-Expert Member
Feb 21, 2011
566
97
Beti zangu naweka, kuliponda embe vuru.
Juu mpaka chini ladondoka, likawa vuru vuru.
Na siku sijaiweka, ya kulitia kinywani.

Kinywa changu nafunga, kuingia embe hili.
Ni bora la kuvundika, kwangu lina thamani.
Mtini lapevuka, likaivia ghalani.
Sehemu mwanana huwekwa, liive pasi na kurupushani.

Halikumbani na viroja, likaingia tabuni.
Likahesabiwa siku, kama komba na la mtini.
Likisalimika kuliwa, basi ladondokea chini.

Chini kutu la ng'ombe, yawa yake mafikio.
Hadi vizuri ukalikoshe, na jiki kama si liwa.
Kisha ujiuze, eti li salama kuliwa.
Bure sijiti mashaka, kupenda yakudondoka.
 

Habdavi

JF-Expert Member
Mar 5, 2011
618
417
chachu ya embe bichi, nayo yafaa kwa achali na pilipili
kweli embe la kwetu tamu, likiiva ladondoka lenyewe,
 

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
46,981
63,944
Embe hili hili embe au embe gani hilo? sijaliona mie embe la hivyo
 

brazakaka

Senior Member
Mar 3, 2010
116
14
Embe hili hili embe au embe gani hilo? sijaliona mie embe la hivyo
Whatever the case Mkuu, tatizo langu siku hizi si vijijini au mijini watu hawana subira ya kungoja yaanguke yenyewe ni kulazimisha mtindo mmoja tu.
 

Kwamex

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
378
95
Enzi zangu nakumbuka,mabichi tulipopoa, kwenye majivu ya moto, kwa muda tulifukia, twasubiri likiwiva, kisha kwa mbali kubondabonda, sijui ni kubonda? Ama kulibonyabonya, subiri lilainike, kama ya kigoli maziwa, kisha kwa juu toboa, na kuanza kulinyonya, hakika utaenjoy, na...........dah! mi mkali aisee.
 

jacjaz

JF-Expert Member
Sep 7, 2011
440
203
mimi nimezaliwa town jamani,cjui km yalidondoka yenyewe au yaliangushwa,mim nanunua na kula tu huku town....Yote naona ladha zafanana tu.....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

5 Reactions
Reply
Top Bottom