Maelfu ya wanawake, watoto waikimbia Sudan Kusini

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,569
9,429
Sudan. Maelfu ya wanawake na watoto kutoka Sudan Kusini wamevuka mpaka kuingia nchini Sudan tangu kuanza kwa mwaka huu, wakikimbia ghasia na tishio la njaa.

Kwa mujibu wa Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR)Wasudan Kusini 1, 37,000 wameingia Sudan tangu Januari mosi, huku wengine zaidi ya 131,000 wakiwa tayari wamewasili nchini humo tangu mwaka 2016.

Wafanyakazi wa misaada wanaarifu kuwa wengi ya watu hao wanaowasili sasa ni wanawake na watoto.

Mkurugenzi wa Shirika la Msalaba mwekundu, kanda ya Afrika Dk, Faroumata Nafo-Traore amesema wengi wa wanawake na watoto hao wamedhoofika kiafya na wamekuwa na msongo wa mawazo kutokana na hali iliyowatokea huko wanakotoka.

Tangu Desemba 2013 jumla ya wakimbizi 471,000 wa Sudan Kusini waliingia nchini Sudan. Wengi wao wako katika kambi zilizokuwa Mashariki na Kusini mwa Darfur na magharibi na Kusini mwa Kordofan.


SOURCE; MWANANCHI
 
Back
Top Bottom