Maelfu wamzika Sheikh Yahya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maelfu wamzika Sheikh Yahya

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, May 23, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Rais Kikwete aliongoza maelfu ya wananchi
  [​IMG] Wananchi walijipanga barabarani kumuaga  [​IMG]
  Maelfu ya wakazi wa Dar es Salaam na vitongoji vyake wakiwa wamebeba jeneza la Sheikh Yahya Hussein gwiji wa utabiri Afrika Mashariki kuelekea msikiti wa Manyema ambako aliswaliwa.


  Rais Jakaya Kikwete, wanasiasa na wananchi walikuwa miongoni mwa maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwenye mazishi ya Mtabiri maarufu Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahaya Hussen, aliyefariki juzi kwa ugonjwa wa moyo.
  Kwenye mazishi hayo viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa walitoa wito wa kudumishwa kwa amani, umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania.
  Viongozi waliopata nafasi ya kuzungumza ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na John Cheyo Mwenyekiti wa UDP. Safari ya kwenda katika nyumba ya milele kwa marehemu Sheikh Yahaya Hussein ilianza nyumbani kwake Magomeni Mikumi, majira ya saa 7:15 mchana, ambapo mwili ulipitishwa katika barabara ya Morogoro, Lumumba, Umoja wa Mataifa, kabla ya kuhitimishwa katika makaburi ya Tambaza ambako alizikwa.
  Katika hali ya inaliyoonekana watu wengi wameguswa na kifo hicho, wakazi wengi wa jiji la Dar es Salaam walijitokeza barabarani kuaga mwili wa Sheikh Yahaya, huku vilio vikitawala.
  Aidha, jeneza lilohifadhiwa mwili wa marehemu halikubebwa katika gari maalum kama ilivyopangwa awali, baada ya wananchi na waumini wa dini ya Kislaam kupinga hatua hiyo na badala yake waliamua kubeba mikononi.
  Kabla ya mazishi, mwili huo ulipelekwa katika Msikiti wa Manyema kwa ajili ya kuswaliwa na baadaye ulifikishwa katika makaburi ya Tambaza, ambako Rais Kikwete na mamia ya wananchi wengine walishuhudia shughuli za maziko.
  Aidha katika maziko hayo, pia walihudhuria mawaziri kadhaa, wabunge na viongozi wa dini ya Kiislam kutoka Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) na wanasiasa.
  KAULI ZA VIONGOZI WA VYAMA
  MNAUYE
  Katibu wa Itikadi na Uhamasishaji wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Mnauye, alisema CCM imempoteza mtu muhimu ambaye katika maisha yake aliamini mazungumzo ni jambo zuri kutatua migogoro ya kisiasa.
  Alisema hata katika kazi yake ya utabiri alionyesha dhahiri kuguswa na jambo la umoja na kuweka mbele Utanzania.
  "Sheikh Yahaya ndiye mtu wa kwanza kutabiri Serikali ya Umoja wa Kitaifa wa Zanzibar, jambo hilo likatokea na hivi sasa kule wanaishi kwa amani na utulivu," alisema Mnauye.
  Aliwahimiza Watanzania kumuenzi kwa kudumisha amani na utulivu kwa kukataa kutumiwa katika mambo mbalimbali yatakayovuruga amani.
  LIPUMBA
  Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Ibrahim Lipumba, alisema kwa niaba ya chama chake, ametoa salamu za rambirambi kwa wafiwa pamoja na Watanzania.
  Alisema marehemu atakumbukwa kwa mambo mengi kutokana na elimu aliyokuwa nayo ya utabiri, lakini pia Waislamu watamkumbuka kama kiongozi wao.
  "Mimi binafsi nilianza kumsikia Sheikh Yahya wakati nilipokuwa mtoto mkoani Tabora, hivyo naamini elimu yake ya usomaji wa Quran tukufu ninaifananisha na ile ya Sheikh Abdul Zamadu", alisema Lipumba.
  Mwenyekiti huyo wa CUF, alishauri kuwepo na kumbukumbu muhimu kwa marehemu ili vizazi vijavyo viweze kumsikia na kumjua.
  Alisema katika kumuenzi, wanasiasa waachane na siasa za ubaguzi wa dini, kabila na eneo.
  Hata hivyo, Lipumba aliwaasa wanasiasa kuepusha kutenganisha umoja wa Watanzania na kwamba siasa ambazo zinajenga amani na utulivu nchini ndizo zinazotakiwa.
  MBOWE
  Mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema), Freeman Mbowe, alisema chama chake kimeshtushwa na kifo cha Sheikh Yahaya na akawataka familia ya marehemu kuwa na subira na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
  Alisema, marehemu Sheikh Yahaya, wakati wa uhai wake ametoa fundisho kwa Watanzania kupendana, kusaidiana pamoja na moyo wa kupenda maridhiano.
  CHEYO
  Mwenyekiti wa Chama cha UDP, John Cheyo, alisema kifo cha Sheikh Yahaya kiwakumbushe Watanzania kupenda amani kama mwenyewe alivyopigania wakati wa uhai wake.
  Alisema endapo hali hiyo haitadumishwa amani na utulivu hautakuwepo na watakaoumia ni wananchi wa kawaida na sio viongozi wa kisiasa.
  "Tukumbuke Amani ni jambo zuri, Watanzania ni wamoja wanapenda kusaidiana, sasa tuepukane na vitendo vya kuvunja amani kwani wengi tutateseka", alisema.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
Loading...