Maelfu Wampokea Sugu, Wamwita Mfalme

nilikuwepo kwenye mkutano wa mheshimiwa SUGU alifanya vizuri sana ingawa ilifanyika kijijini sana lakini huwezi amini watu walivokuwa wengi mimi nana picha yake ya video watu walirudisha kadi za ccm watu walijiunga na cdm.lakin tulivokuwa tunatoka huko kwenye mkutano sehem ya ilolo tulivamiwa na vijana wa ccm waliokuwa wameshika sepetu sururu fimbo na mawe na kujeruhi baadhi wa watu na kwa maonezi zaidi pia walikamatwa watu watano waliopigwa uvamizi huo uliongozwa na mwenyekiti wa vijana wilaya ccm Michael Mwangosi
 
hao waliofika vyuo vikuu wakawa maproffesor wamefanya nini dada au unakariri elimu darasa na elimu dunia....
 
Radhia Sugu is a psycopathy, anafurahisha watu wa vijiweni tu na wala hayuko makini na maendeleo ya jimbo lake. Najua CDM mkoa wana andaa mtu mwingine kwa vile ukiongea na watu makini hapa Mbeya wana regret kwa hasira zao walizompigia kura za chuki mbunge wa zamani kutoka CCM Mpesya.

Wewe ni mkazi wa Mby kweli? siamini mi naishi Mbeya labda hao magamba wa Mbeya ndo wenye maoni hayo, Sugu bado anakubalika sana ndo mana alimaliza fujo ambazo hata jeshi lao la Itende walishindwa, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni
 
issue hapa ni kuwa SUGU kafanya mambo wasiyotarajia wengi zaidi wasomi wamekuwa waoga au wabinafsi kujitoa kushughulikia matatizo ya wananchi.
Mpeni hongera alikotoka mpaka alipofikia zaidi soma kitabu chake uta-mu-appreciate.

chukua mfano wa RAISI WA MADAGASCAR why not SUGU?
 
Anaweza kuwa alichaguliwa kwa bahati mbaya pia.

Hao waliochaguliwa kwa bahati nzuri si ndo wezi wa rasilimali za nchi hii? Wasira, lowasa, chenge, makinda, nchemba na wengine wengi tu ndani ya ccm. na sidhani kama katika kiswahili kuna kitu kinaitwa bahati mbaya
 
Kazi yangu inanilipa mshahara mzuri kwanini nijiangaishe kwa kimshahara cha mil 3 sijui 4?

Mwanadamu amezaliwa alete mguso chanya duniani na ndicho anachofanya Sugu, wewe kwa uchoyo wako au kukosa uwezo unaridhika na mshahara, unafikiri maisha ni kupata mshahara mzuri tu?? Polee :thinking:
 
Mbunge Sugu ametishia uhai wa CCM huko Kiwira alipoenda kumpigia kampeni mgombea udiwani wa Chadema. Watu kwa maelfu walimpokea na kumshangia mfalme, mfalme. Sugu ameapa kuwa CCM haitapata hata jimbo moja Mbeya 2015. Source. Mwananchi uk 14

tupe more up date za huko KIWIRA mkuu
 
Wewe ni mkazi wa Mby kweli? siamini mi naishi Mbeya labda hao magamba wa Mbeya ndo wenye maoni hayo, Sugu bado anakubalika sana ndo mana alimaliza fujo ambazo hata jeshi lao la Itende walishindwa, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni

mweleze mkuu watu wa mby ndiyo tunao fahamu ni kizuri alicho kifanya sugu kulinganishs na wote walio pita labda kama hupo mbeya na ana negative response na kamanda
 
Radhia Sugu is a psycopathy, anafurahisha watu wa vijiweni tu na wala hayuko makini na maendeleo ya jimbo lake. Najua CDM mkoa wana andaa mtu mwingine kwa vile ukiongea na watu makini hapa Mbeya wana regret kwa hasira zao walizompigia kura za chuki mbunge wa zamani kutoka CCM Mpesya.
'Jambo usilolijua"
Hiyo ni kujifurahisha tu.
lazima ujue kuwa sugu anakubalika sana,na ni miongoni mwa wabunge wachache sana nchi hii waliopita kwa haki na jasho lao.Mbunge mmoja wa upinzani kushinda uchaguzi ni sawa na wabunge 30 wa Magamba.Ni kama vile ngamia kupenya kwenye tundu la sindano,jinsi CCM wanavyotumia vibaya madaraka.
lakini pia wewe utakua mgeni wa mby,siasa za mbeya ni ngumu sana,huwa kura zinapigwa kwa makabila(wasafwa na wanyakyusa) lakni Sugu Mkinga kupewa ubunge mbeya ni kama vile Obama kushinda Marekani.
mwisho kabisa nataka ufahamu kuwa huyo Mpesya unayemsema,sie wengine alikua mwl wetu mzuri sana,lakini Ubunge alituangusha.miaka yote aliyokaa bungeni ,pamoja na kuwa meya ,bado aliishia kuwajengea wasafwa wenzie Vilabu vya pombe za Kienyeji.Kimoja kule juu milimani"Iziwa" na kingine kule alikokuwa anaishi"Isanga -Iganzo"wakati huohuo akaenda kujenga shule Dodoma.Hiyo ni akili kweli?ina maana wanchi wake hawastahili kupata Elimu,wanatakiwa kunywa mataputapu(pombe za kienyeji,yaani "Kyindi na Komoni" ila wadodoma ndio wanastahili kupata Elimu.
Usiongee mambo usiyoyajua,kaa kimya watu tuna hasira sana.
 
Radhia unasema Sugu anaungwa mkono na wahuni, ni kweli nakubaliana na hoja yako. Hana tofauti na CCM inayoungwa mkono na wajinga. Kwangu ni afadhali mtu mhuni kuliko mjinga
 
Back
Top Bottom