maelfu wamiminika DUCE.

kwi kwi kwi kwi matumbo u have completed my afternoon! wanadhani ni rahisi?? mbona wao hawafugi panya wakawauze mtwara??
cacico we unatunzwa na kulishwa na bwana wako unamdanganya mwenzako azeke na bahasha ya kaki mkononi.
 
Last edited by a moderator:
mkuu hujanisoma ukanimaliza au hujanielewa kwanza sijasema serikali inaajiri watu wote, pili nimesema kwamba serikali inatakiwa itengeneze mazingira tatu nimesema mimi napenda serikali iliyopo madarakani iomdoke. wewe sijui kwa kutojua au kwa makusudi umepotosha hoja yangu. kama watu hamchukui hatua zinazofaa muda huu serikali mpya ikiingia madarakani mtaanza kuishambulia isipomaliza hata mwaka. chukulia serikali ivunje mikataba ya halali iliyowekwa na hao wenye viwanda wahisani wakituwekea vikwazo kama zimbabwe itakuwaje. mi ntajichukulia jembe naingia zako chimbo kulima viazi mviringo na ndizi tena kisomi. wewe uliezoea kublame watu utaanza campain serikali ya zamani irudi. halafu kabla ya huo mwaka 2015 au 2020 ambao unahisi serikali nzuri itakuja hapa katikati tunafanyaje tunakaa tu au tunachukua hatua? ni hatua gani hizo mbali na za kuelimisha watu kuhusu ubaya wa hii serikali kwani hilo haliwezi kutulisha wala kutuvisha
 
Tunazidi kupanua vyuo vya elimu ya juu, wahitimu ni wengi kwa mfumo ule ule wa kazi za kuairiwa!!! Ni lini tutaamua rasmi kufanya somo la ujasiriamali kuwa compulsory kuanzia shule za msingi? Iwekwe wazi kazi za ajira zina ukomo!!! Tubadilishe utashi (mindset) vinginevyo bomu litalipuka kushinda lile la Hiroshima na Nagasaki. Imagine post 2 lakini waombaji wenye sifa 5,000!!! Hao 4998 wataenda wapi? Wakijiunga pamoja hawa!!!! Ni hatari!1
 

By Red Giant

ndugu hebu tuone hili. serikali imeshindwa kuajiri watu, sekta binafsi nako hakuna ajira. watu wengi wanasema serikali iliyopo ikiondoka madarakani ndo suluhisho hata mi naona kwa sehemu hilo ni suluhisho lakini hata kikiingia chama pinzani kinaweza ajiri watu wote?. mtu atasema kinatakiwa kitengeneze mazingira ya mtu kuweza kujiajili je kisipoingia madarakani inamaana mtu huyu atasubiri miaka mingine mitano na pengine kumi aje kutengenezewa mazingira ya kujiajiri! mi suluhisho la haraka kwa hii hali naona ni vijana waliomaliza shule kukaa pamoja wawili watatu kupanga mpango na kuhakikisha wanachukua hatua (kinachosumbua sana ni kuchukua hatua). we unafikiri suluhisho la haraka la hii hali ni lipi?

Mkuu
Hizi post zote mbili za kwako, soma halaf kanusha kwamba kwenye red sio wewe ulieandika.
 
umejengo hoja yako vizuri. lakini kuna mapungufu. kwanza waliosoma sio kwamba ni watu special sana hadi serikali iwaundie chombo kwaajili ya kuwakopesha wao tu ukishamaliza chuo unatakiwa ukapambane na dunia kama ambao hawakusoma so kama kukopa wote muende benki muende benki. bodi ya mikopo yenyewe huwa inakosa pesa ya kuwapatia wanafunzi na mahospitali pia hakuna dawa sasa hizo za kukopesha wanafunzi waliomaliza shule sijui zitatoka wapi? hoja yako ni nzuri kinadharia lakini kipractical imekaa vibaya. hivi hawa watu wakipewa milioni moja utawashauri wakafanye biashara gani? mi bado ningewambia wakalime na kufuga kitu ambacho najua wakikaa vizuri bila hata hiyo milioni moja ya serikali wanaweza kukifanya. wanafunzi wengi wakitoka chuo huwa hawaoni mambo kiuhalisia anaweza pewa milioni moja ataenda fungua kibanda cha Mpesa halafu anajiri mtu! kisa anaona kufagia kibanda na shughuli za pale sio hadhi yake. tuacheni kujiona special aliesoma na asiyesoma kwa serikali ni watu sawa dawa ni kufight tu tena wasomi wanaadvantage ya elimu.
 

umeongea kitu cha maana sana mkuu,nimeipenda komenti yako.

Kwa mkulima wa Tanzania aliambiwa zile pesa za EPA zilizorudishwa zitafunguliwa akaunti maalumu TIB kwa ajili ya kukopesha wakulima..ukienda pale mkulima uliyetoka kinyanambo ni kwamba haukopesheki wanakopesheka ni wale wale wenye mitaji mikubwa..sasa hii serikali isiyojali hali halisi ya wananchi wake sijui inasubiri nini..mkulima wa nanjilinji unamuomba documents inayoonyesha alivyolipa kodi ya mradi wake kwa miaka miwili si utani uo!!
 
Mkuu sijasema popote kwamba hizo parastatal zianzishwe kwaajili ya wanafunzi wanaomaliza chuo kikuu. Nimesema kama sehemu ya kukabiliana na tatizo la ajira. Piga hesabu yale mabilioni ya Kikwete yaliyotafunwa na watu wachache tu yalikuwa kiasi gani? Kama angeyaweka kwenye parastatal wakulima na wafanyabiashara wakayakopa na kujiendeleza ingekuwaje, kuliko alivyoyapelekwa benk na kuishia kuchukuliwa na matajiri?

Ninasikitika kwamba katika hoja zako nimegundua kwamba wewe huna experience yoyote na maisha yoyote ya ujasiriamali zaidi ya hayo ya ajira ambayo unayaishi. kwahiyo hata unapoongelea ujasiriamali wewe mwenyewe huujui. Na sijui unatoa wapi ujasiri wa kuwashauri wenzako wakajiajiri wakati wewe unategemea ajira.

Hivi unawezaje kusema waende wakalime au kufuga wakati hujasema wanatoa wapi hiyo ardhi ya kulima? Au unadhani kila mtu ana ardhi? Na pili mbona husemi huko anakoenda kulima atapanda nini? Mawe? Bila huo mtaji wa angalau milioni moja au laki tano, hizo mbegu bora na mbolea atanunuaje? Na hizo eka tatu au nne atakazotaka kulima atazilimaje? Kwa mikono? Ulishawahi kulima wewe au unapiga story tu hapa ndugu?

Unasema wakafuge, watafuga nini? Bata mzinga? Unataka waende porini wakawinde swala ndiyo wafuge? Hivi unaweza kufuga kuku au hata simbilisi bila kuwa na hela ya kununulia hao kuku au simbilisi wa kuanzia kufuga? Ukitaka kufuga kuku wa nyama 200 let say unahitaji mtaji usiopungua laki sita, sasa ukimwambia mtu nenda kafuge tu unafikiri atakwenda kuanzaje? Hatuwezi kutatua tatizo la ajira kwa vijana wa Tanzania, kwa mitizamo kama hii yako ya kuamini kwamba vitu vitafanyika tu bila ya kuwa na means ya kuvifanya. Ni lazima tuandae mazingira mazuri ya kuwawezesha watanzania kujiajiri na si kusema tu wakajiajiri ilihali mazingira ya kujiari ni mabovu.
 
matumbo, kama kuna blanda ambayo huwa naona Kikwete aliicheza hadi hivi sasa ni yale mabilioni ya Kikwete. hivi hadi leo yamerudisha faida kiasi gani? Yaliishia kugawanywa kwa wafanyabiashara wakubwa na matajiri tu. Kwa hakika safu ya uongozi ya Kikwete imekosa kabisa wabunifu wa kuweza kutatua matatizo ya watanzania. hivi sasa nchi ina matatizo kibao yakiwemo ya kushuka kwa thamani ya shilingi, kupanda kwa mfumuko wa bei, kuongezeka kwa vitendo vya rushwa na tatizo kubwa linaloibuka hivi sasa ni hili la ukosefu wa ajira. lakini nafikiri jitihada zinazofanyika kuyatatua haya kwa kweli si za kuridhisha. inawezekana kuna nia ya dhati ya serikali kuyakabili, lakini inawezekana wamekosa watu wanaoweza kuumiza vichwa vyao kutafuta suluhu la matatizo ya watanzania.
 

Eti una ajira nzuri?kupitia ajira yako nzuri,umewasaidia vijana wangapi kupata ajira kama yako?alafu kwanini unitwishe majukumu ya wazazi wa hao vijana ambao wanalalamika hawapati ajira,eti niwape kompyuta!we toka uzaliwe ulishawahi kupewa kompyuta bure,tena na mtu usiyemjua?
 
By Mwakitobile

Mtaji siyo lazima upate kutoka benki,kwa mfano unamiliki simu au kompyuta ya thamani ya 300,000/= uza upate mtaji mdogo ambao mnaweza kuunganisha watu wawili au zaidi na kubuni biashara ndogo,ambayo mkiisimamia vizuri inaweza kuleta faida kubwa baadaye.Ndugu zangu kuweni na uthubutu,siku zinakwenda sana,serikali haina kabisa mpango na nyinyi.Kama unabisha jiulize strategic human resource planning katika government parastatals au organizations katika kuzalisha ajira mpya ni implicable katika real world.Take care.....




Hapa ndipo nilipo kuuliza swali hili hapa chin soma post yako hapo penye red, watu wanaongea facts nyinyi mnaleta utoto na mifano ya kufikirika kanusha tena si wewe ulieandika hapo.

Huo ndo ukilaza mkuu, computer umewagawia wewe bure eti? Nani kwambia vijana wanacomputer kama yako?

Watu wanashinda njaa mitaani wewe unaongelea laki tatu! are you seriously? Think before you present something to other people.


Ninakazi nzuri - yangu si yakuweza kuwasaidia au kuwaandalia vijana mamilion ajira, Jukumu hilo ni la serikali upo,

shughurisha kichwa chako
. mkuu.
 
Dada adolay.Unajisifu kuwa na kazi nzuri ya kuajiliwa!kazi nzuri ni ile uliyoitengeneza mwenyewe na inakuletea faida ya kutosha,kama ukiachishwa kazi,bado utajisifia kuwa ulikuwa na kazi nzuri.Hao mabwana zenu wanaihujumu serikali ndiyo wametufikisha hapa,usiwapotoshe wenzako wasubiri,wakati wewe ni kimada wa kigogo mkubwa serikalini.
 
Yaani humu ni malumbano tuu! Lakini ukweli ni kwamba wale hasa wanaoteseka kwa kutokuwa na kipato ni hii ajira mnayoisema hata kuiona hii jf hawawezi, wote humu wengi wenu mna ajira au mna uhakika wa maisha/kula. Ujumbe haufiki kwa walengwa.... Mnachosha tu
 
trueeeee, bwanangu pia anaweza kukulisha hata wewe! karibu tushee kulishwa!
TUONGEE UKWELI cacico kama bwana wako amekusaposti katika hoja kama hii lazima atakua na elementi za kishoga! we unasemaje? halafu cacico kama bwana wako anamawazo kama wewe lazima kutakuwa kuna mtu anawalisha we chunguza vizuri.
 
Last edited by a moderator:
mkuu Lukolo tusifanye ubishi ukawa mkubwa na usiwafaidishe watanzania je wewe unafikiri waliokosa ajira wasubiri waajiriwe au waanze kujiajiri kidogokidogo?
 
Last edited by a moderator:
mkuu Lukolo tusifanye ubishi ukawa mkubwa na usiwafaidishe watanzania je wewe unafikiri waliokosa ajira wasubiri waajiriwe au waanze kujiajiri kidogokidogo?
Red Giant, sasa umekuja kwenye hoja. Tofauti na pale mwanzoni ambapo ulikuwa unatoa mapendekezo ambayo hayatekelezeki. Kwa hakika wasio na ajira wanatakiwa kutafuta namna mbalimbali za kujikomboa. Na inaweza isiwe busara kuendelea kusubiri ajira za serikali kwa kuwa zinaweza kuchelewa hata kwa miaka kumi. So kila mmoja aangalie opportunities anazoweza kuzipata kupitia kwa ndugu, marafiki na watu wa karibu ili kujikomboa na hili jinamizi la ajira.

Nakumbuka mimi baada ya kushindwa biashara ya umachinga, niliwatafuta jamaa zangu fulani ambao walikuwa wana twisheni center niakenda kuungana nao. Kwa hiyo nikaanza angalau kupata hela ya chakula. Mimi sina tatizo juu ya suala zima la kujiajiri, lakini nilikuwa sikubaliani na mapendekezo yenu mliyokuwa mnayatoa ya mara watu wakauze simu wapate mtaji. mara wakalime nk. Nafikiri kila mtu ajaribu kuexplore opportunity iliyo karibu yake ili kuweza kurahisisha maisha.

Lakini ijulikane kwamba hii ni short term solution ya tatizo kubwa la ajira inayolikabili taifa hivi sasa. Longterm solution ni kama ile niliyosema awali ya kuanzisha parastatal ambayo itawakopesha watu mitaji. Akina Bhahressa walianza na biashara ya mgahawa tu, hivi sasa wanamiliki mabilioni. Kwa hakika milioni moja inatosha kufungua kiosk au kuanzisha biashara ya baba ntilie na inaweza kuja kuwatoa vijana wetu wakaachana na utegemezi wa ajira za serikali. So nafikiri tufike mahali fulani tuwe na long term plan za kulimaliza tatizo la ajira nchini.
 
umeongea vema sana mkuu hata kama hukubaliani na hoja zetu kwamba watu wakauze simu lakini unakubaliana kwamba vijana wanatakiwa wa do something. hata kama we unaichukulia ni short term solution(kwa mtazamo wako) vijana wanatakiwa watumie nguvu zote na kuona hiyo kama ndiyo solution yao kuliko kukaa na kuisubiria serikali kuja na hicho kitu unaita long term plan
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…