maelfu wamiminika DUCE.

usihofu kuhusu mimi,nimeshalitumikia taifa vya kutosha..hivi sasa tunasaidia kujenga uchumi kwa vitendo,nchi hii watu tukibweteka kwenye vipupwe na kusahau uzalishaji..hatutofika popote.
nashukuru kusikia unalitumikia taifa! jitahidi basi kuwashauri mawazo chanya wana jf hasa wanaosaka ajira
 
Duh, JWTZ wanaajiliwa kwa kutoa rushwa? Nchi kwa kweli imefika pabaya. Mtu atakayeniambia CCM iendelee kutawala namwona kama mchawi.
 
nashukuru kusikia unalitumikia taifa! jitahidi basi kuwashauri mawazo chanya wana jf hasa wanaosaka ajira

ebu anza kutoa ushauri wako mgeni..maana hawa madogo sio kwamba ni wajinga,wavivu, wasiofikiri na hawajitumi kama mnavyotaka kutuaminisha..mazingira ya wao kujiajiri ndio magumu..wengi ukikaa nao wana idea nzuri tu,ila wataanzaje ndio ishu.
Mie kitu ambacho nnakipinga ni wasomi wetu tuliowasomesha kwa pesa kibao wakawe wachuuzi..wauze urembo,chupi,sidiria,yeboyebo,singirendi..hawa wasomi wetu wakatumike kwenye uzalishaji mdogo na mkubwa ndio tutaona matunda yao kuanzia family level hadi taifa kwa ujumla..nani sasa wa kuwawekea mazingira ya kujiajiri au kuajiriwa???
1. Serikali
2. Sisi jamii
3. Wao wenyewe

ushauri wangu kwa sasa nitautoa kwa jamii yani sisi,tuache tu kuwalaumu wakati atufanyi chochote kuwasaidia..mie nachoshauri sisi jamii tuwasaidie kuwapa mitaji,yani tutumie njia tunazotumia kuwezesha harusi zifanyike kwa mafanikio..tuwachangie kwenye family zetu na jamii kwa ujumla..serikali nayo ina mengi inayotakiwa kuyafanya.
 
Duh, JWTZ wanaajiliwa kwa kutoa rushwa? Nchi kwa kweli imefika pabaya. Mtu atakayeniambia CCM iendelee kutawala namwona kama mchawi.

Kwakweli ajira kwa sasa ni tatizo kubwa,ni watu wachache ambao wametokea maisha ambayo hawawezi elewa shida wanayopata vijana.Mimi bila kumung'unya maneno.Tumebakiza miaka miwili tu,ya kufanya maamuzi magumu.Lazima tuelewe kuwa Ndani ya chama tawala kwa sasa hakuna mtu anayehangaika kutatua matatizo ya taifa hili,kila mtu anafikiria kujilimbikizia mali yake na familia yake.Na wengine kuwa ma tycoon.Kwani kwa sasa pesa ndiyo yenye thamani na ndiyo inayofanya mtu aheshimike, no matter ilipatikana kwa njia haramu au haki.

CCM must go...
 

Sawa bibie mimi ni kuruta.Sasa panga siku uje hapa upanga(ngome) tuonane,alafu tuone kama utakuja kusema tena maneno hayo.Tatizo la mliomaliza shule juzi,mnaona kama hakuna wasomi wenye shahada za uzamilivu,waliohitimu kuanzia miaka ya 2000 kushuka chini.Watu wana shahada za uzamivu na wanatupigia saluti,itakuwa wewe na kishahada chako cha kwanza.Jeshini kuna wasomi wengi kuliko unavyofikiria binti.
 

Unasumbuliwa na ugonjwa unaoitwa CCMPHOBIA
 
Nani kakuambia Jeshi linaajiri kila mwaka,au unahisi tu kuwa kila bajeti jeshi lazima liajiri hata kama halina mahitaji, ???That would wrong line of resoning.
 

Ninakuelewa vizuri sana binti,hacha kujificha nyuma ya vivuli vya wenzako.Wewe mwenyewe ni muhanga mkubwa wa tatizo la ajira,ndiyo maana mdomo wako unavuja maneno ya ghadhabu.Nakukumbuka vizuri sana bibie.wewe umri huo bado unataka watu wakuletee mchanganuo wa biashara ya kufanya,tena kwa manufaa yako? Ndiyo maana usiku hamlali,mnahangaika tu,mara corner bar,ambiance au kwa macheni.
 

mimi ushauri nilionao unabase katika hao watu watatu uliowataja!
serikali kwanza waweke mazingira ya graduate wote kujiajiri kwa kurekebisha sera zake na sheria mfano wawe wanapewa masomo ya ujasiriamali kama intensive course for last semester ili anapotoka ajue pakuanzania niwapi! then wakiwa likizo wasiwe wanabaki tu nyumbani serikali iwaambie waajiri wawapokee wanafunzi wote ili waweze kupata practical training experience

jamii inatakiwa ibadilike ,wasomi wengi wanakuwa wanauoga kuchekwa na jamii kwa hiyo wanataka kuishi ilikuipendeza jamii mfano msomi nilazima uwe na gari ,uvae suti,nyumba bora ndani ya kipindi kifupi .lakini hawataki kukubali kuwa hali ya sasa imebadilika sio kama zamani.hii inawafanya wahitimu wengi kuchagua kazi taasisi fulani kama EWURA TRA,BOT,PENSION FUNDS,TPA,TANAPA,SUMATRA Lakini wanasahau kuwa kunasehemu nyingi tu za kufanya kazi tena wana maslahi mazuri kushinda huko wanapo tarajia! Mfano Nilikuwa nafanya kazi ofisi mmoja kati ya hizi nilizo zitaja nafasi ikitangazwa application ni zaidi ya 7000 alafu wanahoitajika ni 5,kinacho fanyika hapo nikuwapick watuwanaofahamika ili kupunguza recruitment cost,mpaka tukawa tunajiuliza why many applicatants ! tukagundua jamii ina mawazo mabaya kuwa ukifanya kazi huku unatoka kimaisha ,wakati si kweli maisha ni kujipanga mkuu

kitu cha mwisho ambacho wengi wahatakubaliana na mimi ni kwamba wahitimu wenyewe hawa play thier part kwenye game la ajira ,utakuta mtu kamaliza chuo alafu ajitumi kutafuta ajira anaisubiri nyumbani kama vile kasomea zile course za afya na ualimu ambao wao wanapangiwa tu ajira na serikali wakiwanaisubiria nyumbani,utamkuta dogo maskani anakwambia brother nitafutie kazi!ukimuuliza wewe usafanya maombi sehemu ngapi anakwambia toka mwezi watano anasubiri post alizo tuma tume ya ajira au anaogopa kuapplay kazi kwa sabaubu siku hizi ajira ni za kujuana

mwisho mm nafikiri kila mtu hapo serikali,mhitimu na jamii wote wananafasi ya kupunguza tatizo la ajira

 
hahahahah kumbe wengi tulihudhuria december conference!!!
 

wewe kuruta ata ujui mambo ya ndani ya jeshi,nani atakupigia saluti ??..ujui chochote kuhusu jeshi unachojua ni kufungulia wageni geti na kung'arisha viatu vya wakubwa..mnakula bure kila kitu bure mnalemaa siku izi mnapigwa ata na wananchi..njoo mtaani uku uone watu tunavyolijenga taifa wanajeshi wa ukweli,sio unakaa na wasiwasi ukisikia wasomi wanakuja jeshini..njoo mtaani uku tutengeneze taifa la wazarishaji,sio unajifanya mwalimu wa ujasiriamali wakati unasubiria kuuziwa soda sh mia tatu alafu unawatukana madogo wasio na ajira.
 

unatamani niwe ivyo unavyosema..sema tu ndio ivyo haiwezekani tena,ndege ikipaa haina rivas.
 
ndugu hebu tuone hili. serikali imeshindwa kuajiri watu, sekta binafsi nako hakuna ajira. watu wengi wanasema serikali iliyopo ikiondoka madarakani ndo suluhisho hata mi naona kwa sehemu hilo ni suluhisho lakini hata kikiingia chama pinzani kinaweza ajiri watu wote?. mtu atasema kinatakiwa kitengeneze mazingira ya mtu kuweza kujiajili je kisipoingia madarakani inamaana mtu huyu atasubiri miaka mingine mitano na pengine kumi aje kutengenezewa mazingira ya kujiajiri! mi suluhisho la haraka kwa hii hali naona ni vijana waliomaliza shule kukaa pamoja wawili watatu kupanga mpango na kuhakikisha wanachukua hatua (kinachosumbua sana ni kuchukua hatua). we unafikiri suluhisho la haraka la hii hali ni lipi?
 


Huo ndo ukilaza mkuu, computer umewagawia wewe bure eti? Nani kwambia vijana wanacomputer kama yako?

Watu wanashinda njaa mitaani wewe unaongelea laki tatu! are you seriously? Think before you present something to other people.
 
mimi sihitaji kufuga chochote nataka kukufuga wewe, mke wako na dada zako..nataka nimlime binti yako na shangazi zako..

Siku nyengine usimfundishe samaki kuogelea..waulize Ilovo wanatutambua.muulize Mo anatutambua.
kwi kwi kwi kwi matumbo u have completed my afternoon! wanadhani ni rahisi?? mbona wao hawafugi panya wakawauze mtwara??
 
Last edited by a moderator:

Kaka/dada nasikitika sipendi nikuvunjie heshima

1. Nani kakwambia serikari imeshindwa kuajiri na kwanini iajiri serikali? 2. nani kwambia kuna serikali dunian imeajiri watu wake wote? toa mfano

Nyinyi watu ndo mnatufanya wakenya watudharau watanzania kila siku kwa mawazo mgando ya ovyo kama haya yako.


Kazi ya serikali ni kujenga mazingira mazuri ya vijana kuajiriwa na kujiajiri (sifa kubwa kwa viongozi wenye maono na upeo)

- Serikali lazima iwe na mikakati ya wazi kuwekeza kwenye nyanja za kupanua ajira

Mfano
Serikali haikupaswa kuuza mashirika na viwanda mbalimbali vya uzalishaji, kwa maana huko ajira ingepatikana

Viwanda vyote vya nguo ni mahututi, ni watanzania wangapi wangeajiriwa na kuongeza mzunguuko wa fedha kuwafikia machinga, mama lishe na wakulima....... Tafakali. Vijana wote hao wangefaidika kwa uwepo wa ufanisi wa viwanada vya nguo tu - isitoshe soko la pamba la uhakika lingepatina, kama huna cha kuchangia kaa kimya.


Ukienda tanga, Kulikuwa na Kiwanda cha mbolea, kiwanda cha chuma, kiwanda cha plastic ambon, bandari wakati huo, vyote hivi vingeendeshwa kwa ufanisi watanzania wangapi wapepata ajira na kuingiza mzunguuko wa fedha kama nilivoanisha hapo juu!!!! kwa ujinga na uwezo mdogo wa viongozi chini ya chama cha ccm tumeuwa kila kitu.

Mifano iko mingi naachana nayo inatosha hiyo ukiacha kiwira, chai, kahawa, mkonge, Tumbaku, madini, kiparapara na hasari tumeuwa kilimo -kumbuka vyama vya ushirika vikuwa na nguvu sana lakini vikauwawa kimtindo kwa nini nk

Tunataka serikali ijenge mazingira ya kufufuliwa viwanda vilivokufa na pia kufanya juhudi za makusudi kuingia ubia na makampuni ya inje viwanda vingine vianzishwe kwa usimamizi wa serikali siyo kuwaachia wageni 100% na kutesa ndugu zetu wakitanzania. Serikali iwabane mafisadi ili fedha itakayopatikana wakopeshwe vijana kwa misingi ya kuwawezesha- unataka sasahivi waunganishe nguvu, nguvu gani hawana fedha au wajifunge yokes shingoni wavute plau walime jamani hawana fedha watajiunga kufanya nini? wanahitaji kukopeshwa ili wakalime!!!!!!!!!!!!!!!!!

Hata ujerumani na marekani wapo wasiokuwa na kazi, lakini sio kama ilivyo kwa tanzania. hakuna serikali duniani inayoweza kuajiri raia wake wote. Moja ya sifa za viongozi katika nchi za ujerumani na marekani ni uwezo wa kuongeza ajira na kupunguza mfumko wa bei sio kama viongozi wako wanao toa taarifa hewa kila siku na kuvaa mashati ya kijani na kuhonga wafia njaa pilau, unaweza kuhonga pilau na kofia marekani wewe? hii inathibitisha vijana wamepigika ndo maana wakocheap kiasi hicho - Acheni siasa tunapojadili mambo ya msingi jamani.

Kusema kwa sababu hujawahi safiri na basi jipwa, ni bora kuendela na lazamani kwa sababu hutambui umadhubuti wa lile geni, ni ufinye wa mawazo chanya. kwahiyo kwenu CCM ndio kila kitu, vipi nchi zingine wanakobadili vyama na watawala kila siku wamegeuka mawe? mfano kenya, Zambia, malawi, Ghana nk. Mnaongelea kuthubutu, vijana hawathubutu kuanzisha miradi mbona nyinyi mnashinndwa kuthubutu kukiingiza chama kingine madarakani na kusingizia hamna uhakika na wageni!Kuweni jasiri wa kufanya maamuzi sahihi. CCM imechoka tuingize chama kingine iwe CUF, Chadema au NCCR ni sawatu.
 
Huo ndo ukilaza mkuu, computer umewagawia wewe bure eti? Nani kwambia vijana wanacomputer kama yako?

Watu wanashinda njaa mitaani wewe unaongelea laki tatu! are you seriously? Think before you present something to other people.

Basi vuteni subira Dr slaa au Lowasa aje awape hizo ajira 2015.Usisahau umri nao unakwenda sambamba na Jinsi miaka inavyokwenda.Nawahakikishia msipochukua hatua,mtatubu mpaka siku ya mazishi yenu..Serikali ikupe wewe ajira alafu watoto wa makamba,kikwete,lowasa, nk.wapewe nini?nchi imekwisha hii,we unabaki unasubiri tu hadi leo.
 

Kwa taaifa yako nina ajira nzuri kwa elimu yangu. Lakini siwezi kusahau nilikotoka kijijini wala kuongea siasa nikijuwa wazi vijana na watanzania wanateseka kwa ujinga wa watawala na hasa wa ccm.

Watu kama wewe mnaojifanya vipofu ili kuchangia michango isioendana na ukweli/uhalisia wa maisha ndio mnaiuwa tanzania.

Anya way hujatuambia uliwagawia vijana wangapi computer ili wauze wapate mtaji wa kujiajiri? hili ndio swali langua la msingi kwako.
 
Mimi nadhani wengi sana wangependa kufanya kitu fulani cha kuwaingizia kipato. Lakini pengine changamoto kubwa ni mtaji. Ambacho serikali ingeweza kufanya hata kama si kuwaajiri vijana wote ingeform parastatal ambazo zingeweza kuwakopesha wajasiriamali kwa mfano wa ukopeshaji wa bodi ya mikopo.

Ujasiriamali hauhitaji mtaji mkubwa. kwa hiyo vijana wangekuwa wanaandika project proposal zinazoonyesha aina biashara wanayotaka kufanya na mtaji wanaohitaji. Hizi zingeweza kuwa ni joint project or indvidual projects. Parastatal husika zingezichambua hizi project proposals na kutoa mitaji kulingana na ukubwa wa project.

Kwa mfano tukiweka maximam ya mtaji wa up to one milioni kwa kila mkopaji! Ambao pengine anatakiwa aanze kurudisha after six months, huoni kama tungekuwa tumewasaidia vijana wengi sana? Na si ajabu tungekuwa na maenterprises makubwa tu hapa nchini ambayo yangekuwa yamechipukia kutoka kwenye hivi vimitaji vya milioni moja au laki tano!

Just imagine yale mabilioni ya JK, yangelenga kuwa saidia vijana katika mfumo huu, leo hii tungekuwa wapi? Ulishawahi kujiuliza hadi hivi leo yale mabilioni yako wapi? Tatizo viongozi wa CCM ni vichwa vya panzi au wana ubongo kama wa samaki (Karume, 2012). Ubunifu ziro!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…