Katika hili mimi msimamo wangu upo clear
.kimsingi unategemea sana na FACTS zinazotengeneza sakata hili! Kwa bahati mbaya kabisa, hakuna ambae ametamka bayana kuhusu hivyo viwango vya 2012 na vya miaka ya nyuma!
Naamini umenifuatilia kwenye posts zangu nyingi kwenye sakata hili. Mara kwa mara nimekuwa niki-refer taarifa ambayo ipo kwenye page ya facebook ambayo inadai ni official page ya NECTA ingawaje ukiangalia vizuri unakuta ni kama vile official page ya HakiElimu or someone else! Taarifa ile inadai kwamba Serikali imetoa viwango vipya ambavyo vitaanza kutumika 2013 ambapo, badala ya F kuanzia 0-20, kuanzia 2013 F itaanzia 0-34! Aidha, badala ya D kuanzia 21-40, mitihani kuanzia 2013 D itaanzia 35-44! Aidha, kwa mujibu wa Raia Mwema, wao wanadai viwango hivyo vipya ni kama ifuatavyo:
A = 85%-100% ....B = 65%-84% ....C = 50%-64% ....D = 35%-49% ....F = 0%-34%
Wakati viwango vya zamani ni hivi hapa chini:
A = 81%-100% ....B = 61%-80% ...C = 41%-60% ....D = 21%-40% ....F = 0%-20%.
Hapa chini, ni baadhi ya aya za habari hiyo kutoka gazeti la Raia Mwema.
Ni katika mazingira hayo taarifa ya mabadiliko katika utaratibu wa muda mrefu wa gredi za ushindi inakuwa habari kubwa. Alama zinazofahamika kwa muda mrefu ni A- alama 81 hadi 100; B- alama 61 hadi 80; C-alama 41 hadi 60; D- alama 21 hadi 40 na F- alama 0 hadi 20.
Kwamba alama hizo zimekuwa zikibadilishwa na Baraza la Mitihani (NECTA) katika kile kinachojulikana kuwa ni standardisation ni taarifa iliyowatisha wengi. Ni hali iliyowaathiri kwa aina ya pekee watahiniwa wa mwaka 2012, hata kama kwa miaka karibu mitano ya nyuma matokeo ya kidato cha nne, na hata ya kidato cha sita, yamekuwa yakionyesha kuserereka kuelekea chini.
Vyanzo kadhaa vya habari vinasema alama hizo sasa ziko katika makundi ya A-alama 85 hadi 100; B-alama 65 hadi 84; C-alama 50 hadi 64; D-alama 35 hadi 49 na F alama 0 hadi 34
Hivyo basi, mimi hoja yangu inasimama pale pale kwamba...ikiwa ni kweli kwamba viwango vipya vilipaswa kutumika 2013 na badala yake Baraza wakavitumia 2012; hili jambo si sahihi na haijalishi ni wakati gani Wizara walifahamu jambo hilo!
Hapa chini, ni kauli kuhusu Mkuu wa Shule wa Azania kutoka kwenye gazeti hilo hilo la Raia Mwema!
Mkuu wa Shule ya Sekondari Azania, Dar es Saalam, Bernard Ngozye, anasema matokeo hayo mabaya yaliwashangaza wadau wa elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam kiasi cha wao kukutana na kuhoji Baraza la Mitihani kujua chanzo ni nini. Anasema Machi mwaka huu walikutana na maofisa wa Baraza la Mitihani na ndipo hapo walipoambiwa kwamba Baraza lilirekebisha gredi, taarifa hiyo wakiisikia kwa mara ya kwanza.
Anasema Machi mwaka huu walikutana na maofisa wa Baraza la Mitihani na ndipo hapo walipoambiwa kwamba Baraza lilirekebisha gredi, taarifa hiyo wakiisikia kwa mara ya kwanza.
Aidha, gazeti lilimuhoji Mwalimu mwingine wa Shule ya Sekondari Kiteketeke iliyopo Newala. Hii ndo kauli ya Mwalimu huyo(Mkuu wa Shule):
Walikuja hapa wenzenu. Niliwaambia haya haya. Mmoja baadaye akaniuliza kama nilikuwa ninajua kwamba gredi za Baraza ziko juu, nikasema hapana, anasema Fredy John, Mkuu wa Shule ya Sekondari Chitekete, Newala, Mtwara, ambayo ni kati ya shule 10 zilizofanya vibaya zaidi kitaifa.
Hao hao Raia Mwema wakiongea na Mkuu wa Shule mwingine, Mkuu huyo anasema:
"Hapana. Hatujui kama kuna mabadiliko hayo ya alama za madaraja ya ufaulu. Wakibadili si lazima walimu na wanafunzi wawe na taarifa? Haya mabadiliko hayapo," alisema Magesa, ambae ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Mukituntu; Ukerewe Mwanza!
Hapa maana yake ni nini? Kumbe mabadiliko muhimu kama hayo ni lazima shule zifahamu na bila shaka ndio maana Mr. Magese ame-conclude kwamba no such changes coz hawana taarifa yoyote kama hiyo!
Kwamba shule zetu zina matatizo ya Waalimu, si jambo geni hata kidogo! Hoja kwamba shule zetu hazina maabala; kwangu si hoja coz masomo ya Art na Biashara hayahitaji Maabara na bado ufaulu wao ni mdogo! Kwamba shule za serikali zina matatizo lukuki; ni chizi tu ambae anaweza kukataa ukweli huo! Hata hivyo, ngoja tuone kauli ya Mwalimu mwingine ambae alihojiwa na Raia Mwema:
Nami matokeo haya yamenishangaza sana. Shule yangu haina matatizo ya walimu, maabara wala maktaba, lakini imefanya vibaya tofauti na matarajio yetu, anasema Sid Moir, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Katoke Lweru, Muleba, Kagera.
For more, link hii hapa:
Raia Mwema - Siri ya waliofeli kidato cha nne 2012 nje nje
So what was so special in 2012? Anyway, ngoja tuchukue baadhi ya shule za mfano ambazo wadau wengi wanazifahamu.....kimsingi, nimeangalia zile maarufu na zenye kufaulisha kulingana na kundi husika!
Ukitaka kufanya Statistical/Mathematical Analysis, matokeo hayo yatakuwa kama ifuatavyo. Matokeo haya ni for three consecutive years, 2012, 2011 and 2010:
| Div I | Div II | Div III | Div IV | FLD | TOTAL | PSD(I,II,III) | Div IV+FLD | %PSD | %FLD |
Marian Girls | 42 | 36 | 8 | 2 | 0 | 88 | 86 | 2 | 97.7 | 2.3 |
| 73 | 30 | 10 | 1 | 0 | 114 | 113 | 1 | 99.1 | 0.9 |
| 75 | 4 | 2 | 0 | 0 | 101 | 101 | 0 | 100 | 0.0 |
| | | | | | | | | | |
Feza Boys | 48 | 12 | 8 | 1 | 0 | 69 | 68 | 1 | 98.6 | 1.4 |
| 44 | 8 | 4 | 0 | 0 | 56 | 56 | 0 | 100 | 0.0 |
| 60 | 16 | 7 | 1 | 0 | 84 | 83 | 1 | 98.8 | 1.2 |
| | | | | | | | | | |
St Anthonys | 10 | 36 | 60 | 126 | 1 | 233 | 106 | 127 | 45.5 | 54.5 |
| 21 | 50 | 78 | 85 | 0 | 234 | 149 | 85 | 63.7 | 36.3 |
| 49 | 71 | 88 | 33 | 0 | 241 | 208 | 33 | 86.3 | 13.7 |
| | | | | | | | | | |
Kirinjiko | 2 | 20 | 62 | 45 | 0 | 129 | 84 | 45 | 65.1 | 34.9 |
| 8 | 25 | 33 | 49 | 0 | 115 | 66 | 49 | 57.4 | 42.6 |
| 11 | 36 | 59 | 45 | 1 | 152 | 106 | 46 | 69.7 | 30.3 |
| | | | | | | | | | |
Mzumbe | 32 | 35 | 16 | 16 | 3 | 102 | 83 | 19 | 81.4 | 18.6 |
| 63 | 28 | 14 | 6 | 0 | 111 | 105 | 6 | 94.6 | 5.4 |
| 60 | 20 | 10 | 11 | 1 | 102 | 90 | 12 | 88.2 | 11.8 |
| | | | | | | | | | |
Ilboru Sec. | 20 | 38 | 30 | 27 | 0 | 115 | 88 | 27 | 76.5 | 23.5 |
| 40 | 23 | 24 | 14 | 1 | 102 | 87 | 15 | 85.3 | 14.7 |
| 48 | 12 | 19 | 11 | 0 | 90 | 79 | 11 | 87.8 | 12.2 |
| | | | | | | | | | |
Azania | 14 | 47 | 57 | 137 | 180 | 435 | 118 | 317 | 27.1 | 72.9 |
| 48 | 34 | 66 | 138 | 71 | 357 | 148 | 209 | 41.5 | 58.5 |
| 56 | 62 | 122 | 207 | 159 | 606 | 240 | 366 | 39.6 | 60.4 |
| | | | | | | | | | |
Kibaha | 26 | 41 | 25 | 13 | 2 | 107 | 92 | 15 | 86.0 | 14.0 |
| 59 | 22 | 15 | 8 | 0 | 104 | 96 | 8 | 92.3 | 7.7 |
| 53 | 18 | 21 | 14 | 0 | 106 | 92 | 14 | 86.8 | 13.2 |
KEY: PSD = PASSED
FLD = FAILED
FIRST ROW for each School= 2012 RESULTS
SECOND ROW for each School= 2011 RESULTS
THIRD ROW For each School = 2010 RESULTS
Aidha, kwenye mchanganuo huo hapo juu, Division IV na Zero zote kwangu ni FAILURE tu!
Kimsingi nimeamua kuyaweka kwa staili hiyo ili kujibu yale madai kwamba matokeo yamekuwa yakishuka mwaka hadi mwaka! Ukiangalia takwimu hizo, jibu ni KWELI matokeo yamekuwa yakishuka mwaka hadi mwaka. Lakini hata hivyo, hatuna budi kuangalia ushukaji huo umekaaje! UKichukua wakali wa serikali hapo juu, utakuta the theory prove TRUE only for ILBORU ambao mwaka 2010 walifeli 12.2% na mwaka 2011 walifeli 14.7%. Hata hivyo, pakatokea STEEP GRAPHICAL FAILURE in 2012 tofauti na ile ya 2011 taking 2010 as a benchmark! Hali kadhalika, Kibaha, Azania na Mzumbe kulikuwa na improvement ukiangalia matokeo ya 2011 kwa kulinganisha na yale ya 2010. Pamoja na yote hayo, bado nako pakatoea STEEP GRAPHICAL FAILURE kwa mwaka 2012 kuliko mwaka wowote ule huku kukiwa na almost DOUBLING kwenye failure ukichukua takwimu za 2011 na zile za 2012! WHY? Uhaba wa Walimu? Madawati? Mahabara? Nini hasa? Kama hizo ndizo sababu; ina maana uhaba huo umeibuka 2012?!
Turudi kwa shule za binafsi.
Ukiondoa Kirinjiko ambao wanaonekana wame-improve 2012 as compared to 2011; wengine wote wanaonekana wameharibu zaidi! Feza Boys from 0.0% to 1.4% wakati Marian Girls from 0.9% to 2.3%! S.t Anthony's Sec hali ndio mbaya zaidi! Percentage Failure ime-shoot from 36.3% in 2011 to 54.5% in 2012! What's wrong na kwenye hizi shule? Nako kuna uhaba wa Walimu? Madawati?Mahabara? Tatizo nini?!
Do these two categories share COMMON problems/challenges?! If not, what type of agent that drove all these categories to the current position (in 2012) as compared to years before?!
Generally speaking, hapa KUNA KITU! Suala la kujiuliza, ni nini hasa hicho kitu?! Ikiwa uhaba nilioutaja hapo juu do not seem to prove TRUE to both categories, so kwanini nisishawishike kwamba tatizo la msingi la 2012 sio lile tulilozoea kulisikia year after year? Ikiwa 2012 watu wamezungumzia suala la Madaraja Mapya, nina sababu gani za msingi za kutokubali hoja hiyo?! It's only GRADE RANGES ndiyo inayoonekana ku-prove TRUE in both categories na kinyume chake ni kuleta ILLOGICAL ASSUMPTIONS!
Na kwa hakika, matokeo haya yana-reflect madai ya kwamba viwango vilivyotumika sio vile vilivyozoeleka! With EXCEPTION of Feza Boys, shule zote hapo juu ufaulu wa Daraja la Kwanza umeshuka sana almost by half kwa kila shule! Did it happen by CONCIDENCE? No, I Don't Think so!
Sasa turudi kujichunguza wenyewe!! Nashawishika kuamini kwamba ni idadi ndogo sana ya wale watoto waliomaliza kidato cha nne mwaka jana ambao wanaingia sehemu kama JF! Hata hivyo, sina shaka hata kidogo kwamba humu jamvini kuna Wanafunzi wengi sana wa elimu ya juu!
Mathalani, wakati nipo SUA, grade zetu zilikuwa hivi:
71-100=A, 65-69=B+, 60-64=B, 50-59=C, 40-49=D, 0-39= E
Kwavile inasemekana kwamba Baraza walitumia viwango vipya bila wadau kufahamu; tu-assume SUA nao wanaamua kutumia viwango vipya bila wanafunzi kufahamu na kuwa kama ifuatavyo!
75-100=A, 70-74=B+, 64-69=B, 55-63=C, 46-54=D, 0-45=E
Tuseme paper imekuja, mwisho wa siku umepata 52! Hapo unapumua na kujiona umepata C (50-59)! Matokeo yanatoka kwenye notice board, unakuta umewekewa D (46-54)! Ukihoji, unaambiwa madaraja yamebadilishwa!! Tuwe wakweli, hivi huko vyuoni kweli kungekalika?! Yaani uambiwe from nowhere kwamba Madaraja yamebadilika; ya mwaka huu ni tofauti na ya mwaka jana!! The same situation iwe pia kwenye vyuo vyote nchini!
Let's be sincere here! Hivi kama ni kweli madaraja yaliyotumika ni tofauti na yale ya kila mwaka; halafu tu-assume the same SCANERIO inatokea upande wa Elimu ya Juu halafu utafiti ufanyike na kugundua kwamba tatizo ni viwango vipya ambavyo vilitumika kinyemela kisha serikali ikaamua viwango vya zamani vitumike hadi pale wadau watakapokuwa well informed.....hivi criticism hizi tunazoziona leo hii hapa bado zingekuwepo? Au kwavile wale watoto hawana wa kuwasemea ndio maana tunakata shauri la kuwala nyama mbichi kwa uzembe wa Baraza na Wizara? NO, tuache ubinafsi wa kujiona kwavile tumeshavuka mto, basi haya hayatuhusu! Hakika, tutafute pengine pa kuisulubu serikali lakini hapa sio pahala muafaka!
Aidha, lazima tukumbuke kwamba hawa madogo ndo kwanza wameanza safari! Matokeo haya ndiyo ambayo kesho na keshokutwa yatakayotumika ku-determine their future! Ni matokeo haya haya ambayo wengine yatatumika kama Competitive Edge/ Leverage katika ku-apply international Scholarships!! Tuseme mtu amepata 83; hii maana yake ni kwamba, kwa viwango vya kawaida, huyu mtu angekuwa na "A" lakini kwa viwango hivyo vipya, atakuwa amepata "B" na hivyo ku-minimize his/her competitive edge!!
What do I say about hivyo viwango vipya? Binafsi, sina tatizo na viwango vipya hata kidogo! And in fact, ilikuwa ni utani kwenye elimu kudai kwamba aliyepata 22% nae amefaulu! Haya yalikuwa masihara kwenye mustakabali wa elimu! Hata hivyo, ninachopinga mimi ni utumikaji wa viwango vipya kinyemela(kama ni kweli).Hili kwa hakika halikubaliki! Tutafute pa kuisurubu serikali lakini sio katika hili la kuamuru kutumika kwa viwango vya zamani PROVIDED ni kweli viwango vilivyotumika ni vipya! Nitakuja hapa kuungana na wote wanaopinga STANDARDIZATION IF and only IF itakuja kuthibitika kwamba madai ya kutumika kwa viwango vipya 2012 yalikuwa ni MADAI YA UONGO! Kinyume chake, matokeo lazima yarekebishwe na wahusika waliofanya mambo sensitive kama haya kinyemela wanapaswa kuondoka na si lazima wasubiri kuondoshwa!
c.c
Kichuguu