Maelezo ya Wizara ya Elimu kuhusu mchakato wa kurekebisha matokeo ya Kidato cha 4 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maelezo ya Wizara ya Elimu kuhusu mchakato wa kurekebisha matokeo ya Kidato cha 4

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by oduko, May 10, 2013.

 1. o

  oduko Senior Member

  #1
  May 10, 2013
  Joined: Dec 16, 2012
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  UFAFANUZI KUHUSU KUPITIWA UPYA KWA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012


  Mnamo tarehe 03 Mei, 2013 Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Wiliam Lukuvi (Mb) ilitoa Kauli ya
  Serikali Bungeni Kuhusu Taarifa ya Awali ya Tume ya Taifa ya Kuchunguza Sababu za kushuka kwa ufaulu wa Mtihani wa Kidato cha
  Nne Mwaka 2012.

  Kauli ya Serikali ilielekeza kuwa matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2012 yafutwe na yaandaliwe upya kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011 ili Wanafunzi hao wawe katika mazingira yanayofanana na ya wenzao wa miaka iliyopita kwa kuwa mfumo uliotumika mwaka 2012 katika kupanga matokeo na madaraja ni tofauti na ule uliotumika mwaka 2011 na miaka
  iliyotangulia.

  Kwa kuzingatia mapendekezo ya Tume na Maelekezo ya Baraza la Mawaziri, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kwar mamlaka
  aliyonayo chini ya Sheria ya Baraza la Mitihani Tanzania, kifungu cha 20, sura 107 ameliagiza Baraza la Mitihani la Taifa kupitia upya
  Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012.

  Aidha, imeagizwa kwamba matokeo hayo yaandaliwe kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011. Serikali haikuagiza kufanyika upya kwa mitihani hiyo na wala haikuagiza kusahihishwa upya. Hivyo, Serikali inapenda kuwahakikishia wananchi kwamba
  hapatakuwa na zoezi la kurudia usahihishaji wa mtihani huo kwa sababu hakuna dosari zilizobainishwa kwenye usahihishaji
  wa mitihani hiyo.

  Alama za watahiniwa ambazo zimehakikiwa zipo tayari, kitakachofanyika ni kwa Baraza la Mitihani kutumia alama hizo kuchakata matokeo upya kwa kutumia viwango vya ufaulu vilivyotumika mwaka 2011. Utaratibu ambao umekuwa ukitumika tangu mwaka 1973
  wakati Baraza lilipoanzishwa, ni wa kuweka viwango vya ufaulu kila mwaka kwa kuzingatia ufaulu wa somo husika na ufaulu katika
  mwaka uliotangulia.

  Kutokana na maelezo hayo, ni dhahiri kuwa zoezi la kupitia upya matokeo ya Kidato cha Nne 2012 litachukua muda mfupi na matokeo yatatangazwa hivi karibuni.

  Selestine Gesimba

  KAIMU KATIBU MKUU
  WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO
  YA UFUNDI
  10/05/2013
   
 2. tunduruboy

  tunduruboy JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2013
  Joined: Mar 16, 2013
  Messages: 389
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  useless people where are we taking this country we need people who are upright to lead this country we are tired of these crooks, Let the go to hell, Politics and education can never walk together, Let the experts do there work Lukuvi is a stdr 7 so he cant know the negative impact this will have of the future generation
   
 3. t

  thatha JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2013
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  mkuu LUKUVI katoa tamko kama serikali, suala la kupitia upya mtokeo ni limekuja baada ya wataalam kukaa ni kufikia muafaka huo, unaweza kujifanya na kiingereza chako, lakini kumbe hujui hata kinachoendelea
   
 4. Ta Kamugisha

  Ta Kamugisha JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2013
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 2,857
  Likes Received: 879
  Trophy Points: 280
  Nchi ya kusadikika a.k.a nchi ya mazuzu
   
 5. N

  Ntuga Senior Member

  #5
  May 10, 2013
  Joined: Apr 20, 2013
  Messages: 168
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi hii wizara ya elimu naibu waziri si ndiye kafoji vyeti, yeye anaona poa tu........, sijui ila inauma....sumu,zemarcopolo..hawa viongozi wenu wa CCM wanatumia makalio kufikiri..........manake majibu mepesi kwa maswali magumu.....tutafika kweli?
   
 6. tunduruboy

  tunduruboy JF-Expert Member

  #6
  May 10, 2013
  Joined: Mar 16, 2013
  Messages: 389
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  You can not know the value of something unless you have being through that, Lukuvi and fellow ministers do not know the extent of damage they are creating to this country or Is it that you are doing that deliberately so that they can create the educated people who will not protect the integrity of this country, The previous results which have been suspended were approved by the same cabinet with president Kikwete chairing the meeting, Are you telling me that they did not see that problem, What am saying is improve the education sector not stardandising them get me correct you hypocrite
   
 7. i

  ilboru1995 JF-Expert Member

  #7
  May 10, 2013
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,331
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Watanzania tunahaki ya kujua kilicho sababisha Baraza la Mitihani kuachana na mfumo uliokuwa unatumika toka 1973... Sababu za kurejea mfumo huo zinajulikana kuwa ni kuongezeka kwa kasi watahiniwa waliofeli! Je nini kilisababisha Baraza kubadili mfumo?...
  Tusifanye mchezo katika elimu hata kidogo, hapa ndipo ambapo Taifa linazalisha madaktari, mainjinia, marubani, manahodha, wapiganaji, wanasiasa, waalimu aitha vipanga ama vilaza!...Kama Taifa, maendeleo yetu yatategemea na uwezo wa Rasilimaliwatu tuliowaandaa...
  Kwa upande wa pili wa shilingi; Tunaweza kuendelea kutawaliwa kiakili na kimwili kwa kukosa maarifa! Kwa kukosa maarifa tunajikuta RASILIMALI zetu hazitusaidii bali zinawanufaisha mabeberu plus makuwadi wachache... nina mashaka na huu mkakati unaoendelea kama kweli unaangalia maslahi mapana ya Taifa letu, na si mbinu za kutufanya duni na kuendelea kutawaliwa kwa miongo mingine mingi ijayo...
   
 8. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #8
  May 10, 2013
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  nchi inaendeshwa na events na ndio maana Dr. Kitila Mkumbo ameuliza kuwa mlijua lini juu ya hili tatizo na hamjamjibu. Aibu yenu maana historia inaandikwa
   
 9. a

  artorius JF-Expert Member

  #9
  May 10, 2013
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 758
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuliko kushiriki kwenye hii dhambi ya kuchakachua matokeo itakayopelekea kuzalisha fake engeneers,fake doctors,fake teachers ni bora uache kazi.
   
 10. Az 89

  Az 89 JF-Expert Member

  #10
  May 10, 2013
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 1,606
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Hivi kwa nini usitumie kiswahili?....kiingereza hiki ndicho ulichotumia kujibu mitihani 2012....? hata Le Mutuz hawez ongea hiv...kibovu sana...pu...mb....a.fu
   
 11. J

  JokaKuu Platinum Member

  #11
  May 10, 2013
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 11,968
  Likes Received: 3,376
  Trophy Points: 280
  @ilboru1995, thatha,

  ..kama mna muda someni article ya Kitila Mkumbo aliyochapishwa na gazeti la raia mwema.

  ..if u dont have time soma key point nilizo-highlight.

  ..kwa mtizamo wangu serikali inachakachua elimu, na huo ni mchezo wa hatari sana kwa future ya taifa letu.  cc:mad:tunduruboy, Kichuguu, NasDaz, ZeMarcopolo, Zitto
   
 12. tunduruboy

  tunduruboy JF-Expert Member

  #12
  May 10, 2013
  Joined: Mar 16, 2013
  Messages: 389
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  It does not matter what language I use tanzania has two official languages if you dont know English go to hell with your Lukuvi
   
 13. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #13
  May 10, 2013
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 42,867
  Likes Received: 11,273
  Trophy Points: 280
  Ni wazi serikali imeona bora iwape marks za bure na ipunguze sifuri aalf watangaze kiwango cha ufaulu kimepanda na watu wazidi kujidanganya alaf walio pata zero ndio watakwenda kwenye vyuo vya ualimu maana wataongezewa marks watapata divion 4 na3
   
 14. n

  nguvukazi mikono JF-Expert Member

  #14
  May 10, 2013
  Joined: Jan 1, 2013
  Messages: 490
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acheni kupiga kalele za kasiasa hapa nyie,nani kawaambia kusoma ni deal hapa Bongo?

  Viigizo vyangu katika maisha ni hawa wafuatao.

  1.Mbowe huyo anapeta na hana elimu hiyo munayoipigia kalele hapa
  2.Sugu huyo anapeta form four failure
  3.Mnyika huyo anapepa na maeshindwa kumalizia degree yake ya jioni
  4.Lema huyo anapeta jambazi ala arusha mstaafu
  5.Maji marefu huyo anapeat mganga wa kienyeji
  6.Selemani Bungala huyo anpeta darasa la saba

  Orodha ni Ndefu jamani naomba tu munisaidie wan jamvi.

  Kama unabisha wewe komaa kupiga shule na ujifanye wewe ni kichwa hao vilaza wa hapo juu watakuja kukupeleka mbio mpaka ukome,chezea Tanzania wewe.

  Bora hayo matokeo yarudiwe tu uenda yatawasaidia hao vijana kupata hata uwezo wa kununua unga na dagaa kwa kufanya certificate za ualimu.

  Ukitaka ufanikiwe Bongo basi kuwa mjanjamjanja wa mjini mambo yako yatakuwa super lakini ukijifanya kichwa sana na mishule yako maisha yatakupiga mpaka mwisho,wananifurahisha sana akina Joti na yule Professa wao,duh ule ndio ualisia wa Bongo.
   
 15. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #15
  May 10, 2013
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Swaga hizi kali kweli.
   
 16. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #16
  May 10, 2013
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,106
  Likes Received: 1,567
  Trophy Points: 280
  Ila hao hao wataalamu walikuwepo pamoja na waziri wao wakati matokeo yakitangazwa kama wangekuwa watu makini wangeshituka kulikoni matokeo 65% ni zero na waliofaulu ni wachache kivile kabla ya hata kuyaweka kwenye public maana haya mambo wanayofanya leo yalishafanyika miaka ya nyuma na matokeo yakitoka yameshatoka, nadhani tuchukue kama changamoto ili siku nyingine waumize vichwa kabla ya kutangaza vitu
   
 17. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #17
  May 10, 2013
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,106
  Likes Received: 1,567
  Trophy Points: 280
  Point hiyo mkuu ila hao wote uliowataja pamoja na elimu zao hizo lakini wengi wao kuna vitu walikuwa wanavifanya ambavyo kwa namna moja ama nyingine vimewaunganisha na watu wengi na ndio maana ukatumia aka ya maji marefu na sugu ambao baada ya kujitambua waliamua kufanya shughuli ambazo mpaka leo wanatambulika kwa majina hayo. Nilichojifunza kwa hao uliowataja ni kwamba elimu ikigoma usikate tamaa wewe komaa na issue zako lakini bado issue ya kupiga shule bado ni muhimu mkuu maana shule ni kuongeza maarifa na si kwa ajiri ya kuajiriwa
   
 18. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #18
  May 10, 2013
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  sina hakika kama serikali ya ccm ina wataalam labda kama ukisema wabaishaji ntakuelewa
   
 19. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #19
  May 10, 2013
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  ipi hiyo? na kiongozi wake ni nani?
   
 20. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #20
  May 10, 2013
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Serikali kupitia Wizara ya Elimu kwa kauli hiyo inasema uthamani wa matokeo ushushwe ili ufaulu uwe na taswira nzuri na si uhalisia wa ubora wa kipimo cha mtihani.


  Si kosa la serikali ni kosa la walioiweka serikali madarakani. Waziri Kawambwa ni mtoto wa nasaba ya Kikwete; tafuta ufaulu wao kwenye mitihani utajiridhisha walioiweka serikali hii madarakani wametuua bila kututazama.


  TAFAKARI CHUKUA HATUA.
   
Loading...