Maelezo ya Serikali ujenzi wa Chalinze-Segera utata-Spika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maelezo ya Serikali ujenzi wa Chalinze-Segera utata-Spika

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ng'wanza Madaso, Jun 19, 2009.

 1. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Maelezo ya Serikali ujenzi wa Chalinze-Segera utata-Spika
  Na Muhibu Said
  19th June 2009B-pepeChapaMaoni
  Spika wa Bunge Samuel Sitta.
  Spika wa Bunge Samuel Sitta, amesema amepokea maelezo ya serikali yanayofafanua kuhusu tuhuma zilizotolewa bungeni na Mbunge wa Nzega (CCM), Lucas Selelii, kwamba fedha za ujenzi wa barabara ya Chalinze-Segera ni za bajeti ya mwaka 2009/10, ambayo haijaidhinishwa na Bunge yamejaa utata.

  Kauli hiyo ya Spika inazidi kuonyesha jinsi sakata hilo lilivyo tete, kutokana na ukweli kwamba, iwapo serikali itakuwa imefanya hivyo itakuwa imevunja katiba na iwapo si kweli Selelii anaweza kuwa katika wakati mgumu kama akitakiwa athibitishe.

  Sitta alisema bungeni mjini hapa jana kuwa alipokea maelezo hayo ya ufafanuzi juzi jioni, lakini baada ya kuyapitia aligundua yana utata katika kitabu cha makadirio.

  Jumatatu wiki hii, akichangia hotuba ya bajeti ya Waziri wa Fedha na Uchumi, Selelii alitoa hoja akitaka mwongozo wa Spika kuhusiana na maamuzi hayo mazito ya serikali.

  Baada ya kutoa tuhuma hizo, Spika Sitta aliitaka serikali itoe maelezo juzi ili jana aweze kutoa mwongozo kuhusiana na suala ambalo ameliita ni zito.

  “Waheshimiwa wabunge, juzi Mheshimiwa Selelii aliomba mwongozo kuhusu maelezo kwamba ujenzi wa barabara ya Chalinze Segera Tanga, umekuwa ukitumia fedha za bajeti ambayo haijapitishwa na bunge,” alisema Spika jana na kuongeza:

  ”Sasa, juzi jioni serikali ilileta maelezo yake mazuri tu , lakini nilivyopitia nilibaini kuna utata kuhusu kitabu cha makadirio, nimekabidhi maelezo hayo kwa Katibu wa Bunge, ikiwa kama fedha hizo zilikuwa katika kitabu cha bajeti ya mwaka 2007/08 hakutakuwa na matatizo, lakini endapo fedha hizo zitakuwa mpya ambazo zimeainishwa katika bajeti hii ambayo tunaipitisha leo (jana) hapo itakuwa ni tatizo kubwa la Katiba,” alisema Sitta.

  Selelii ambaye alihoji nafasi ya mbunge iko wapi, alisema Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein, hivi karibuni aliweka jiwe la msingi wakati pesa zake zimeombewa katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2009/010. Hoja hiyo ilimfanya Spika Sitta kusimama na kutolea ufafanuzi ambapo alisema, Suala hilo ni zito sana kama kuna matumizi yanaendelea wakati bajeti haijajadiliwa na kupitishwa hiyo ni ukiukwaji wa taratibu.

  “Mheshimiwa Spika hii ni dharau, nafasi ya Bunge hapa ipo wapi? baadhi ya miradi imeanza hata kabla haijapitishwa, kwa mfano barabara ya Segera-Chalinze na ile ya Korogwe-Same iliyogharimu Sh. 44 bilioni,”alihoji Selelii.


  CHANZO: NIPASHE

  My take: Je hili linaweza kutokea kuanza ujenzi kabla ya bajeti?
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Mmmm wanajenga barabara kwa mh jk akistaafu asipate shida tena kuja dar.....nilifikiria kuwa wangejenga barabara morogoro toka kimara hadi chalinze kwa level 4 ways...ila si chal segera...sijui sababu haswa naona kama politik zaidi orofessional
   
Loading...