Maelezo ya Brig. Gen. Al-Adawi kuhusu Dowans Feb 20/02/2011

Na kwa nini aje halafu achague baadhi tu ya vyombo vya habari, pili kwani waandishi wangempiga picha na kuzitoa magazetini kingetokea nini, anasema nia kuja kwake ni kuondoa utata uliogubika taifa kuhushu nani ni mmiliki na kusafisha jina la kampuni yake ambalo anaona linachafuliwa, sasa kama ni hivyo kwa nini atake tufanye atakavyo? na kweli watu wamegwaya mimi sijaona picha yake.

Huwezi mpangia mtu aongee au hasiongee na nani, hakuja mahakamani.
 
Hii habari ni ya kupikwa!! Hakuna mtu kama huyo nchi hii!! Wahariri wamelishwa mlungula wote. Ni uongo ni uzushi, hakuna chombo cha habari makini kinachoweza kutoka na kichwa cha habari juu ya mtu ambaye wanadai hataki kupigwa picha. Huyo wanayemzungumzia ni fiction ambayo imebuniwa na watu kupoteza mwelekeo wa mjadala wa mabomu!

Hakuna mmiliki wa Dowans aliyeko Tanzania sasa hivi, ni stori tuu!
 
Mkuu Mkjj, miye nakuomba usisubiri hao mafisadi walipwe, kama unaweza kuyaweka mahojiano hayo hadharani kabla ya malipo hayo kufanywa basi unaweza kabisa kwa namna moja au nyingine kuinusuru nchi yetu kulipa malipo ya kifisadi ya mabilioni ya shilingi.



Hapana; kwa miaka mitano tumewalilia kuhusu watu hawa hawa na sasa wamekuja na kututhubutisha; sasa watawala wetu wawalipe ili tuwaoneshe jinsi gani utawala wao ulivyo mbovu na Watanzani waliowachagua wajue wametuchagulia madudu gani. Walipeni tu. Nitawekeza dokezo la interview hiyo Jumanne.

MM .... kumekucha ..... tujuze basi angalau kidogo
 
Mnyika hana jipya ndugu zanguni, jamaa hata mwaka hajamaliza ameisha chuja vibaya aisee ! wana ubungo poleni
 
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, RA alipewa Powers of Attorney na Board of Directors wa Dowans SA na sio huyo anayejiita Al dawi. Pia hiyo nguvu ya kisheria ilitolewa Costa Rica na sio UAE.

Nimeamini kuwa RA sio mjanja kama tulivyokuwa tukimfikiria kwa sababu angeweza kujipanga vizuri na sio kama alivyokurupuka.

kama hayo ni kweli the who was that man? Na kwanini adanganye umma? Katumwa na nani kuja kudanganya? I still don't get this man.
 
Ok, what to do?????? tuache kulalamika, tuache porojo, tuache kuwasema sasa hao makupe, ujue sisi tunazidi kuumia huku? washatangaza nauli mpya, tufanyeje? huyo jamaa mmiliki kivuli wa dowans kashaingia, tufanyeje sasa ili astoke na hela zetu lakini kama kweli anatoka huko ughaibuni, kama ni humu humu basi tubanane naye!! :A S 13:aaaahh!!! :A S 13::A S 13: nooooouuuu!!!!

very good puestion. TUANDAMANE kudai serikali ya CCM iondoke madarakani. Nadhani wengi waliochoka hawatasita kutuunga mkono km jeshi, walimu, wauguzi etc. Ajenda iwe kuiondoa serikali ya ccm basi. Tuki win kuanzia Dar mikoa mingine ita support and vice versa is true.
 
Kwani mwizi hapa Tanzania ndio Mwekezaji nchi imejaa mazuzu hii yani sijui tu nani ataokoa hawa
 
Ama kweli Tanzania ni nchi ya majuha!!

Yaani mtu anakuja anabwabwaja anachotaka na kila mtu anamsikiliza na kumheshimu!Anawaamurisha waandishi wa habari wasimpige picha na wanatii amri hiyo. Si unajua kawaambia kuwa yuko karibu sana na Fisadi Rostam Aziz?Gazeti lolote lingethubutu kumpiga picha lingeshughulikiwa kikamilifu.

Hakamatwi wala haguswi na mtu awaye yote. Hii ni nchi ya inayosifika kwa AMANI,UPENDO NA MSHIKAMANO na UHURU WA VYOMBO VYA HABARI. Wewe si umeona yale mabomu ya Mbagala na sasa GMboto na watu wanafurahi tu na kucheka kana kwamba waliokufa ni bahati mbaya maana watazaliwa wengine. Maisha yanaendelea kama kawaida. Rais mwenyewe keshasafiri kwenda zake nje ya nchi maana tatizo la Mabomu ya GMboto ni dogo sana.

Nakumbuka usemi wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mafisadi(CCM) Yusuf Makamba mwaka jana baada ya Uchaguzi Mkuu 2010 wakti akihojiwa na BBC alisema WATANZANIA NI WASAHAULIFU SANA MAANA MWAKA 2015 WATAICHAGUA TENA CCM KWA KISHINDO MAANA WATAKUWA WAMESAHAU MATUKIO YOTE MABAYA YALIYOTOKEA NA KUWASIBU AMBAYO KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE YANGELITOSHA KUWAFANYA WATANZANIA WAIONDOE CCM MADARAKANI!!!!

Yes, Tanzania,Tanzania nchi yangu nakupenda sana.Amani,Upendo na Mshikamano Daima.
 
Colleagues,

Hapa ni ujumbe wangu kwa wafuatao:

1) Kamati/Halmashauri kuu ya CCM: 'Wabadirishe kauli zao juu ya kulipwa kwa DOWANs'-Kumbuka mara baada ya mkutano mwezi jana kwa kauli moja walisema serikali aina uwezo wa kukataa kulipa deni/Tuzo hilo na kwa sababu kesi hipo mahakamani basi serikali isubili kufanya hivyo.

2) Waziri Ngeleja ajitokeze tena ktk vyombo vya habari na kuutangazia umma wa Tanzania kuwa alisema uongo na ajiuzuru mara moja

3) Rais JK akiri mbele ya Watanzania-na zaidi supporters wake wa CCM kuwa kutojua mmiliki wa DOWANS amewasaliti na hakuwatendea haki wa Tanzania- Kwa ujumla ajiuzuru ili na wengine wafuatie. Maana ni wengi (Mwanasheria mkuu....)

4) Wanachama wa CCM na Watanzania wengine wenye ugumu wa kuelewa wajue kuwa hatuwezi kuvulimia ujinga huu (kama si upumbavu) wa kudanganywa kama watoto huku maisha ya Watanzania yakiwa hoi.

5) Wabunge wote (hasa wa chama tawala) waone haibu juu yakinachoendelea kuhusu DOWANs. Wachukue hatua mathubuti za kuiwajibisha serikali haraka iwezekavyo. Kila mtanzania aliyechagua mbunge hatusaidie kuhuriza mbunge huyo/wake nini msimamo wake juu ya DOWANs na nini atakacho fanya bunge lijalo

6) Shimbo/Jeshi ambalo linaipenda sana na kulinda amani ya Tanzania limkamate huyo mmiliki ili maswali yote tulinayo yajibiwe kabla ya kundoka kwake nchini. Nitamshangaa sana Shimbo asipofanya hivyo!

7) Wahariri na vyombo vya habari; Chonde!! chonde!! ninyi ni wadau wakubwa juu ya amani yetu. Ukweli mnatusaliti sana! Uzalendo wenu huko wapi? Iweje mchukue habari za mtu muhimu (aliyeitisha mkutano) msichukue picha yake? Mnajua tunatufuta picha wamiliki wa DOWANs; Rais wetu anataka kujua wamiliki wake-tafadhari msaidie-mplekee picha yake leo



7)
 
Colleagues,

Hapa ni ujumbe wangu kwa wafuatao:

1) Kamati/Halmashauri kuu ya CCM: 'Wabadirishe kauli zao juu ya kulipwa kwa DOWANs'-Kumbuka mara baada ya mkutano mwezi jana kwa kauli moja walisema serikali aina uwezo wa kukataa kulipa deni/Tuzo hilo na kwa sababu kesi hipo mahakamani basi serikali isubili kufanya hivyo.

2) Waziri Ngeleja ajitokeze tena ktk vyombo vya habari na kuutangazia umma wa Tanzania kuwa alisema uongo na ajiuzuru mara moja

3) Rais JK akiri mbele ya Watanzania-na zaidi supporters wake wa CCM kuwa kutojua mmiliki wa DOWANS amewasaliti na hakuwatendea haki wa Tanzania- Kwa ujumla ajiuzuru ili na wengine wafuatie. Maana ni wengi (Mwanasheria mkuu....)

4) Wanachama wa CCM na Watanzania wengine wenye ugumu wa kuelewa wajue kuwa hatuwezi kuvulimia ujinga huu (kama si upumbavu) wa kudanganywa kama watoto huku maisha ya Watanzania yakiwa hoi.

5) Wabunge wote (hasa wa chama tawala) waone haibu juu yakinachoendelea kuhusu DOWANs. Wachukue hatua mathubuti za kuiwajibisha serikali haraka iwezekavyo. Kila mtanzania aliyechagua mbunge hatusaidie kuhuriza mbunge huyo/wake nini msimamo wake juu ya DOWANs na nini atakacho fanya bunge lijalo

6) Shimbo/Jeshi ambalo linaipenda sana na kulinda amani ya Tanzania limkamate huyo mmiliki ili maswali yote tulinayo yajibiwe kabla ya kundoka kwake nchini. Nitamshangaa sana Shimbo asipofanya hivyo!

7) Wahariri na vyombo vya habari; Chonde!! chonde!! ninyi ni wadau wakubwa juu ya amani yetu. Ukweli mnatusaliti sana! Uzalendo wenu huko wapi? Iweje mchukue habari za mtu muhimu (aliyeitisha mkutano) msichukue picha yake? Mnajua tunatutafuta picha wamiliki wa DOWANs; Rais wetu anataka kujua wamiliki wake-tafadhari msaidie (at least kwa kuanzia mpelekee picha ya huyo mtu)
 
Dowans imeingia mkataba na Songas... tuache kulialia.
unapokuwa na njaa usiletee jeuri wenye chakula, utakufa. Sasa hivi tunakula matapishi tuliyoyatapika, ndiyo maana kila wakati nasema sitaki unafiki sitaki mambo ya kiswahili!! kikoapi sasa uwezo hatuna tunaleta kelele!!!!:shut-mouth:
 
jamani mwenye picha ya huyo general aiweke hadharani,usikute aliyekuja si orijino general wa Omani,tunasema mbuzi kirobani....
 
mala DOWANS ina mkataba na serikali, mara inamkataba na wizara ya nishati, mara ina mkataba na Tanesco.....sasa inamkataba na Songas......kwa mwendo huu, sitachelewa kusikia DOWANS inamkataba na mke wa nanihii.
 
Kwa hali ilivyo sasa hivi, hata kanyabwoya yeyote anayeseek attention ya media anaweza kuja na kudai mimi ndiye niliyelipua mabomu ya mle kwenye ghala kule Gongo la Mboto. Ila sitaki mnipige picha! Kesho vichwa vya habari vya magazeti vikajaa habari! Huyu mnayesema kuwa ndo mmiliki wa Dowans, hao wanaodai kuwa walifanya naye mkutano aliwapa ushahidi gani hadi wakakubali kuwa yeye ndiye mwenye hayo majina? Ni nani aliyepeleka habari kwenye vyumba vya habari kuwa atafanya press conference? Hivi vyombo vya habari vya Tanzania haviogopi kuwadanganya watanzania??

Bila kuwapa ushahidi wowote wa Madai yake, iliwezekanaje kesho yake HEADLINES zote zikawa zinazungumzia mmiliki wa Dowans?? Huku wakikili kuwa hawana picha yake? Hivi kama hawa wanaoitwa wahariri walikusanywa na RA/EL wakalipwa chao, wakaambiwa kesho andikeni hivi ni nani atabisha kuwa haikuwa hivyo?

Sasa hivi watu wameshupalia; mmiliki wa Dowans, utafikiri wamemuona na wameona hizo karatasi zinazosema kuwa yeye ndo mwenye dowans! Yaani ukitaka kutengeneza drama hapa bongo, unaweza ukaenda Canada, ukaja na mzungu mmoja wa mtaani akasema "Dowans is my company" siku itakayofuatia vichwa vya habari vyote vitakuwa na headline ya "MMILIKI WA DOWANS HUYU HAPA".

Hii habari ya mmiliki wa Dowans sijui Sheikh gani, mi ntaendelea kuona ni uzushi Mpaka tupate uhakika kuwa kweli kuna mtu huyo mwenye hayo madai, vinginevyo ni madai ya kutengenezwa!
 
Mwizi kaiba nini??
Wameleta mitambo yao, wamezalisha umeme na kuuzia TNSCO na FYI bado wanaidai pesa za huduma zao.
Hili suala la Dowans ni siasa za maji taka na baadhi ya magazeti kutafuta umaarufu.
Hawa jamaa walikuwa wanalipwa kuzalisha KW100 kwa siku, so pesa walizolipwa siyo bure, wamezalisha umeme wakauza. Na tanesco baada ya kuuza huo umeme walipata faida pia lkn hakuna mtu anayeongelea hilo. Na pia ktk wazalishaji binafsi wao ndio wenye bei rahisi. Na kama hili ni tatizo wwataifishe basi na mitambo ya ARTUMAS.
Tatzo waTZ tu mambumbu wa vitu na tunapenda dandia treni kwa mbele, tusiruhusu magazeti na walafi wa kisiasa watuvuruge.

Wewe!!??
 
Ndugu zangu, nilidhani Uhuru tulioupata na elimu tuliyoita vinatusaidia kujitambua sisi ni nani katika Ulimwengu huu. Sitaki kuamini kabisa kwamba sisi bado tuko kama kizazi cha karne zilizopita ambapo mababu zetu walirubuniwa kwa pipi na harua na wakaachia wageni wakafanya kila wanachotaka. Sowezi walaumu sana wazee wetu sababu walikuwa bado hawana elimu dunia. Elimu ya kujua adui wa mbali ana sifa zipi. Hawakujua nini hasa kilikwishatokea kule Ulaya, middle east na Asia. So walijionea sawa. Wakawakaribisha hawa watu na taratibu hawa watu wakatuharibia kila kitu mpaka ikafika wakati hawa wageni wakipenyeza ndani kabisa ya mifumo yetu kabla na hata baada ya uhuru.

Ukiliangalia hili swala kwa umakini utaona ni jinsi gani wa-Tanzania tunavyochukuliwa kama watu tuliopoteza mwelekeo Tangu enzi zile. Sitaki kuamini hili. Naamini hatujapoteza mwelekeo ila viongozi wetu wanatutia aibu wanapotufanya sisi tuonekane tumepoteza mwelekeo. Hata kipindi kile cha mababu zetu enzi za utawala wa kimwinyi waliharibu sana jamii yetu sababu walijirahisisha kwa wageni na walihusika hata kuwauza watu kama watuma. Inawezekana kabisa Kikwete anayo DNA ya kimwinyi na anaweza akatuuza kabisa kwa wageni. Sitaki kuamini kama kweli Kikwete ni mtetezi wa Watanzania.

Sasa nirudi katika swala hili la Dowans, hii inaonekana wazi kabisa kwamba huu ni usanii wa hali ya juu. Kwanza huyu bwana ajiitaye mmiliki wa Dowans anasema ameitwa na Serikari, sasa yafuatayo ni ya kujiuliza:-

1.Ni kweli serikari ilimwita?
2.Kuna uthibitisho wa hili toka kwa Ngeleja?
3.Kama kweli allitwa na Serikari, je kwanini hakutaka kuonana na Waziri ambaye ndo mwakilishi wa Serikari?
4. Kwanini ajitokeze kwa waandishi wa habari wachache ambao hata haijulikani ni akina nani?
5. Kwanini akatae kupigwa picha?
6. Kuna kitu gani anakificha?
7.Kwanini anataka deni lipunguzwe?
8. Je aliweze kuelezea vipi swala la Dowans Holdinss S.A (Costa Rica)?
9.Uko Oman hiyo Dowans iko wapi?

Ndugu zangu tukumbuke ya kwamba Dowans Holdings S.A (Costa Rica) haipo kabisa kulingana na uchunguzi uliofanywa tangu hapo awali na hata pia uchunguzi nilioufanya hivi karibuni kutoka kampuni ya serikari ya Costa Rica (Instituto Costarricense de Electricidad [Costa Rican Institute of Electricity]). Hii ni kampuni ya serikari kama ilivyo TANESCO kwa Tanzania, na inasimamia sekta ya umeme na mawasiliono na kampuni nyingine zozote zinazozalisha umeme uiuzia kampuni hii ya serikari umeme nayo uwauzia wananchi. Kulingana na taarifa toka ndani ya kampuni hii hakuna kampuni ya Dowans Holdings S.A (Costa Rica) katika mkataba na haijawahi hata kuwepo. Hizi ni data za uhakika. Hii inanipa wasiwasi wasi kwamba hata huko Oman hii kitu haipo. Ninafanya uchunguzi juu ya Oman na huyu jamaa na pia kwa wale wamiriki wengine ambao wametajwa tangu hapo nyuma na waziri Ngereja.

Kitu ambacho ninafikiria kama wa-Tanzania inabidi ifike muda sasa tuseme basi. Sisi inabidi kujivunia kwa sasa kwamba uwezo wa kuwa na habari tunao na tunaweza fanya uchunguzi wa kina zaidi hata kuwazidi hao Serikari. Na pia hili jambo linashangaza kweli kwamba serikari inashindwa tanganza wanted warrant ya Dowans owners tangu mwanzo. Ingekuwa nchi nyingine tuseme China, India au Marekani, huyu jamaa angelizuiliwa nchini mpaka uchunguzi utakapomalizika. Na nchi nyingine zimekuwa makini kweli pale inapobidi kulinda maslahi ya nchi na watu wake.

Pia labda niongelee swala lingine ambalo nadhani ni muhimu liangaliwe kwa umakini.

1. Nini kazi ya Usalama wa Taifa?

Nijuavyo na niaminivyo mimi ni kwamba Usalama wa taifa wanatakiwa kuangalia zaidi taifa letu kuwa salama. Sio salama tu kutoka katika vita bali salama kuanzia rasilimali zake. Hii inamaanisha Usalama wa taifa wanao wajibu wa kuhakikisha wanakuwa na Inteligence System thabiti ambayo itaweza fuatilia na kuwatambua watu wote ambao wanatishishia Usalama wa Mtanzania, kuanzia nje na ndani ya nchi. Pia jeshi na Police wote wahusishwe. Viongozi wahusika wawajibishwe. Sidhani kama tunashindwa. India wameweza kumtia ndani waziri aliyehusika na skendo ya ugawaji wa 3G spectrum. Hata sisi ikigundurika waziri fulani au hata rahisi fulani kahusika kwa njia yoyote awajibishwe. Na pia sauti ya m-Tanzania lazima isikike na iheshimike.
 
Mwizi kaiba nini??
Wameleta mitambo yao, wamezalisha umeme na kuuzia TNSCO na FYI bado wanaidai pesa za huduma zao.
Hili suala la Dowans ni siasa za maji taka na baadhi ya magazeti kutafuta umaarufu.
Hawa jamaa walikuwa wanalipwa kuzalisha KW100 kwa siku, so pesa walizolipwa siyo bure, wamezalisha umeme wakauza. Na tanesco baada ya kuuza huo umeme walipata faida pia lkn hakuna mtu anayeongelea hilo. Na pia ktk wazalishaji binafsi wao ndio wenye bei rahisi. Na kama hili ni tatizo wwataifishe basi na mitambo ya ARTUMAS.
Tatzo waTZ tu mambumbu wa vitu na tunapenda dandia treni kwa mbele, tusiruhusu magazeti na walafi wa kisiasa watuvuruge.

Ndugu yangu fanya uchunguzi uijue ARTUMAS, Huwezi linganisha hii na Dowans Ndugu yangu. utakua unachanganya mambo jamaa yangu.
Mimi naomba tujadili la huyu jamaa. aliyegoma kupigwa picha!!
hivi mnakumbuka yule mkristu alikufa akachomwa moto na mwili wake haukuonyeshwa hata kwa ndugu zake?- Sasa tutajuaje kama alikufa kweli?
jaribuni kuangalia hili la huyu mwarabu katika mtazamo huu
 
eti nani akamatwe? yaani Billionea tena mgeni wa RA akamatwe na police wa Mwema? labda awe feki.
 
SIJUIKITU; Isingae pia ukisikia DOWANS ina mkataba na Shekh mkuu Simba pamoja na kardinali Pengo!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom