Maelezo toka kwa Meya Jerry Silaa

Maelezo toka kwa Meya Jerry Silaa

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Posts
5,564
Reaction score
847
[h=5]TAARIFA YA KUPOROMOKA KWA JENGO LA GHOROFA JIJINI DAR- ES – SALAAM MTAA WA INDIRA GANDHI NA BARABARA YA MOROGORO
KIWANJA NA.
1. UTANGULIZI.
Sheria zinazosimamia masuala ya ujenzi mijini zilitungwa kwa mara ya kwanza mwaka 1920 wakati wa utawala wa Mwingereza. Sheria hizo zilijukana kama Kanuni za Miji (Township Rules, Cap.101) ambapo Kanuni za Ujenzi Mjini (Township (Building Rules) Cap. 101 zilikuwa sehemu ya Kanuni hizo. Sheria hizo pamoja na mambo mengine zililenga kusimamia shughuli zote za majenzi mjini.

Aidha, Msimamizi wa sheria hizi zilikuwa Mamlaka za Miji, Manispaa na jiji ( kwa wakati huo) kwa sasa ni Majiji, Manispaa na Miji). Hata hivyo sheria hizi hazikuwa zinafanya kazi peke yake kwani mwaka 1968 Serikali ya Tanzania ilitunga sheria ya Wahandisi ( yaani the Engineers (Registration) Act,No.49/1968) na mwaka 1972 ilitungwa Sheria ya kusimamia Wasanifu Majengo ,Wakadriaji Majengo na Wakandarasi, Na.35/1972. Sheria zote hizo kwa pamoja zilikuwa zikisimamia shughuli zote za ujenzi mjini.

Kutokana na taratibu zilizokuwa zimezoeleka tangu huko nyuma usimamizi wa shughuli za ujenzi mjini zimeonekana kuwa mamlaka ya usimamizi ni Halmashauri ya Mji,Manispaa au Jiji husika na siyo wadau wengine. Kwa ujumla dhana hii sio sahihi hata kidogo. Kama tulivyoona hapo juu wadau katika sekta hii ni wengi ambao wanapaswa kusimamia shughuli zote za ujenzi pamoja na ubora wa kazi zinazofanywa na wakandarasi, watalaamu washauri kwa maana ya wahandisi na wasanifu majengo.Taarifa hii inakusudia kutoa ufafanuzi juu ya jengo la ghorofa kumi na sita lililokuwa linajengwa katika kiwanja Na……………………barabara ya Morogoro na mtaa wa Indira Gandhi jijini Dar es salaam kuporomoka siku ya tarehe 29/03/2013.

2. Nini msimamo wa Sheria zinazosimamia Ujenzi Mjini.
Kama ilivyooneshwa hapo juu historia ya sheria zinazosimamia ujenzi mjini zilivyoanza na baadaye mabadiliko ya uchumi yalisababishwa kutungwa kwa sheria ya kusajili Wahandisi mwaka 1968 na baadaye sheria ya Wasanifu majengo ,Wakandarasi na Wakadriaji majengo.

Hivi leo sheria zote hizo hapo juu zilifutwa na kutungwa upya na kutoa majukumu ya msingi kwa kila mamlaka ( Mdau).
Tukianza na Kanuni za Ujenzi Mijini Sura, 101 ilifutwa Mwaka 1994 kwa Sheria Na.8 /1994 (yaani the Law Revision Act, No.8/1994). Baada ya kufutwa sheria hii Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Nchini kote zilikaa kwa kipindi cha miaka 14 bila kuwa na sheria ya kusimamia ujenzi mijini mpaka zilipotungwa Kanuni za Miji chini ya Tangazo la serikali Na.242/2008 (the Local Government (Urban Authourities) (Development Control) Regulations, GN.No.242/2008).

Kanuni hizi zinaweka wajibu kwa Halmashauri kutoa kibali kwa mujibu wa Kanuni Na.124 kulingana na mchoro uliowasilishwa.

Vilevile, kanuni hizi zinaweka wajibu Mhandisi au Msanifu majengo kuandaa hesabu ya uzito wa vyuma vitakavyotumika kujenga jengo husika hii ni kwa mujibu wa Kanuni Na.143.

Kwa mantiki hiyo Halmashauri si Mamlaka pekee ya usimamizi wa majengo makubwa ya umma na /au binafsi ambayo matumizi yake ni kwa ajili ya biashara au shughuli nyinginezo za kibinadamu.Taasisi zifuatazo ni mamlaka za usimamizi ambazo zimeanzishwa na sheria ya Bunge:-

1. Bodi ya Wasanifu Majengo ,Wakadriaji Majengo ni mamlaka iliyoanzishwa na Sheria Na.16/1997( the Architects and Quantity Surveyors (Registration) Act [cap.269 R.E 2002] na mwaka 2010 sheria hii ilifanyiwa marekebisho ambayo kimsingi hayakuathiri majukumu yake. Fungu la 4 la sheria hii linaweka majukumu kwa chombo hiki kufanya yafuatayo;-

• Kusimamia shughuli na utendaji kazi wa wasanifu majengo ,wakadriaji majengo pamoja na kampuni zinazofanya kazi ya utalaamu ushauri katika kusimamia miradi ya ujenzi;

• Kuingia na kukagua shughuli zote za ujenzi unaofanyika hapa nchini kwa madhumuni ya kujiridhisha na kuhakikiksha kama kazi ya ujenzi inayofanyika inafanywa na mtu ambaye amesajiliwa na bodi na anazingatia taratibu,kanuni na sheria zote zinazosimamia ujenzi mijini; na

• Kuhakikisha kuwa maeneo yote ambako ujenzi unafanyika kumewekwa mabango yenye kuonyesha jina na anwani ya mradi, jina la mteja (mmiliki) , watalaamu washauri kwa maana wasanifu majengo na wahandisi pamoja na mkandarasi endapo atakuwa hakufanya hayo atachukuliwa hatua za kisheria.

2. Bodi ya Usajili wa Wahandisi ni mamlaka iliyoanzishwa na sheria Na.15/1997(the Engineers Registration, Act [Cap.63 R.E 2002]. Fungu la 4 la sheria hii linaweka majukumu kwa chombo hiki kufanya yafuatayo;-

• Kufuatilia na kusimamia shughuli na utendaji kazi wa wahandisi ikiwa ni pamoja na kampuni zinazofanya kazi ya utalaamu ushauri wa usimamizi wa miradi ya majenzi mijini;

3. Bodi ya Wakandarasi [CRB] ni mamlaka iliyoanzishwa na sheria Na.17/1997( the Contractors Registration Act, [Cap.235 R.E 2002] Fungu la 4 la Sheria hii linaweka majukumu kwa chombo hiki kufanya yafuatayo;-

• Kusimamia shughuli na utendaji kazi wa Wakandarasi katika kujenga majengo imara na yenye kufuata viwango kwa mujibu wa michoro ya majengo hayo;

• Kuhakikisha kuwa maeneo yote ambako ujenzi unafanyika kumewekwa mabango yenye kuonyesha Jina na anwani ya mradi, jina la mteja (mmiliki) , Watalaamu washauri kwa maana wasanifu majengo na wahandisi pamoja na mkandarasi endapo atakuwa hakufanya hayo atachukuliwa hatua za kisheria.

4. Mamlaka nyingine ya usimamizi ni usalama mahali pa kazi (Occupational, Safety and Health Agency). Hiki ni chombo ambacho kinashiriki pia kusimamia miradi ya ujenzi mijini. Mamlaka hii hutoa kibali na kusajili mradi kama ambavyo mamlaka nyingine ambavyo zinafanya kwa kutoa “sticker”.

5. Hitimisho.
Kama ilivyoonyeshwa hapo juu tumeona kwamba zipo sheria mbalimbali zenye kubainisha wadau wote wanaohusika na usimamizi wa majenzi mijini. Hivyo tunaomba ieleweke kwa umma kwamba Halmashauri ya Manispaa ya Ilala si mamlaka pekee ya usimamizi. Hii ni kwasababu muombaji wa kibali anapoomba na kukubaliwa baada ya kupitia michoro yake ambayo mara nyingi huwa imeandaliwa na Wasanifu na Wakadriaji majengo pamoja na “Structural Engineer” ambao wanasimamiwa na mamlaka zilizobainishwa hapo juu. Halmashauri huwa haina nafasi zaidi ya kitalaamu ya kusimamia katika masuala makubwa hasa ya vyuma na kiwango cha “material” yanayotumika katika ujenzi ; isipokuwa kufuatilia kama muombaji (mmiliki) anajenga kama ambavyo alionyesha katika michoro iliyopitishwa kwa mujibu wa mpango wa uendelezaji wa eneo husika.

________________________________
Imetolewa Na:
Mstahiki Meya
katika kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani (1/04/2013),
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
Dar- es - salaam.
[/h]
 
  • Thanks
Reactions: SQL
Ndo nini sasa, mnasubiri tufe ndo mje na maandiko mareeefu kama haya,it's of no use to us..
 
Mkuu nakubaliana na wewe. Mimi nimeshare tu report. "Don't shoot the messenger".
 
mpaka matatizo ya tokee ndo wananchi kama mimi ndo tunajua kumbe kunasheria za ujenzi tupeni elimu sio mnakaa maofisini yakitokea ya kutokea ndo mnatoa maelezo kama haya.
 
amesema kweli, halmashauri haziwezi kuwa msimamizi wa majengo wakati kuna washauri wanaolipwa kaw ajili hiyo. hili la kuwakamata na kuwasweka ndani wanahdisi na wasanifu wa majengo kila jengo linapodondoka ni uenevu
 
Bado yupo kwa ofisi?Nilitegemea kaishawajibika.
 
Mstahiki meya hadithi yako inatufundisha nini???utakuwepo kwenye dinner magogoni????
 
Mchoro umeaonyesha ghorofa 10 na zilizojengwa ni 16, anazungumziaje hilo?
 
Ndo nini sasa, mnasubiri tufe ndo mje na maandiko mareeefu kama haya,it's of no use to us..
Na afadhali maelezo yenyewe yangekuwa na maana. Lakini nilichokiona hapo ni kuwa Silaa na wenzake wanataka kujivua lawama. Sawa, Manispaa si msimamizi pekee, na wameonyesha wengine wanaohusika, Je, katika ile sehemu ambayo Manispaa inahusika, ilifanya nini ili kuepusha balaa hili? Hicho ndicho Silaa anapaswa kutueleza, si kutupia lawama taasisi nyingine.
Hizo taasisi nyingine tunazifahamu nazo tutazihoji zitoe maelezo kulingana na wajibu wake katika kusimamia ujenzi mijini.
Tafadhali Bwana Silaa, njoo na maenelezo ya kuonyesha Manispaa ilifanya nini kuepusha kadhia hii?
 
Huyu meya asituletee hadhisi hapa na historia, kilichotokea ni misconduct by players kwenye best practice atutajie boldly ni nani wawajibishwe.Na kama ingetokea jambo zuri limejotokeza ktk ujenzi ule angekubali kuwa excluded ktk rewards.Haya mambo matokeo yake huwa ni Carrots and sticks for whatever outcome.Jerry must go
 
Kila mtu atakula kwa mkono wake, hivyo meya chukua lawama zako. Hizo sheria tunazijua
 
Meya ya wa Ilala ambaye ni Slaa haweziu kukwepa lawama na ikibidi alitakiwa awe tayari amejumuishwa katika wa waliokamtwa kama wapo hadi sasa. Hapa suala siyokuangalia kuna wasimamizi wangapi, eleza ramani ya jnego ilibadilishwaje kutoka gorofa 10 hadi 16? kuna siku alichukua jukumu kukaa na wadau wote anaojaribu kuwaorodhesha hapo juu kujadili taarifa mbalimbali kufuati majanga kama hayo huko nyuma? je taarifa hii ni kutaka kujitete kuwa manispaa iliachiwa kufanya kazi ambayo hawana uwezo nayo na wakaendelea kuifanya pamoja na kutambua kuwa hawana uwezo nayo, ni kweli kuwa madiwani wakuwa hawajui utaratibu hadi leo aweze kutoa historia ya usimamizi wa majengo? injekuwa jambo la busara kwama angefikia hitimisho kwa kusema anajiuzulu kwa kusababisho vifo visivyikuwa vya lazima kuliko kuleta porojo hizi sasa ambazo hazima maana. Inasikitisha viongozi wetu wamekuwa mbele kwenye sherehe na kupata ufadhili kwa shughuli zao za kisiasa na kuweka maisha ya watanzania rehani. Mani
TAARIFA YA KUPOROMOKA KWA JENGO LA GHOROFA JIJINI DAR- ES – SALAAM MTAA WA INDIRA GANDHI NA BARABARA YA MOROGORO
KIWANJA NA.
1. UTANGULIZI.
Sheria zinazosimamia masuala ya ujenzi mijini zilitungwa kwa mara ya kwanza mwaka 1920 wakati wa utawala wa Mwingereza. Sheria hizo zilijukana kama Kanuni za Miji (Township Rules, Cap.101) ambapo Kanuni za Ujenzi Mjini (Township (Building Rules) Cap. 101 zilikuwa sehemu ya Kanuni hizo. Sheria hizo pamoja na mambo mengine zililenga kusimamia shughuli zote za majenzi mjini.

Aidha, Msimamizi wa sheria hizi zilikuwa Mamlaka za Miji, Manispaa na jiji ( kwa wakati huo) kwa sasa ni Majiji, Manispaa na Miji). Hata hivyo sheria hizi hazikuwa zinafanya kazi peke yake kwani mwaka 1968 Serikali ya Tanzania ilitunga sheria ya Wahandisi ( yaani the Engineers (Registration) Act,No.49/1968) na mwaka 1972 ilitungwa Sheria ya kusimamia Wasanifu Majengo ,Wakadriaji Majengo na Wakandarasi, Na.35/1972. Sheria zote hizo kwa pamoja zilikuwa zikisimamia shughuli zote za ujenzi mjini.

Kutokana na taratibu zilizokuwa zimezoeleka tangu huko nyuma usimamizi wa shughuli za ujenzi mjini zimeonekana kuwa mamlaka ya usimamizi ni Halmashauri ya Mji,Manispaa au Jiji husika na siyo wadau wengine. Kwa ujumla dhana hii sio sahihi hata kidogo. Kama tulivyoona hapo juu wadau katika sekta hii ni wengi ambao wanapaswa kusimamia shughuli zote za ujenzi pamoja na ubora wa kazi zinazofanywa na wakandarasi, watalaamu washauri kwa maana ya wahandisi na wasanifu majengo.Taarifa hii inakusudia kutoa ufafanuzi juu ya jengo la ghorofa kumi na sita lililokuwa linajengwa katika kiwanja Na……………………barabara ya Morogoro na mtaa wa Indira Gandhi jijini Dar es salaam kuporomoka siku ya tarehe 29/03/2013.

2. Nini msimamo wa Sheria zinazosimamia Ujenzi Mjini.
Kama ilivyooneshwa hapo juu historia ya sheria zinazosimamia ujenzi mjini zilivyoanza na baadaye mabadiliko ya uchumi yalisababishwa kutungwa kwa sheria ya kusajili Wahandisi mwaka 1968 na baadaye sheria ya Wasanifu majengo ,Wakandarasi na Wakadriaji majengo.

Hivi leo sheria zote hizo hapo juu zilifutwa na kutungwa upya na kutoa majukumu ya msingi kwa kila mamlaka ( Mdau).
Tukianza na Kanuni za Ujenzi Mijini Sura, 101 ilifutwa Mwaka 1994 kwa Sheria Na.8 /1994 (yaani the Law Revision Act, No.8/1994). Baada ya kufutwa sheria hii Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Nchini kote zilikaa kwa kipindi cha miaka 14 bila kuwa na sheria ya kusimamia ujenzi mijini mpaka zilipotungwa Kanuni za Miji chini ya Tangazo la serikali Na.242/2008 (the Local Government (Urban Authourities) (Development Control) Regulations, GN.No.242/2008).

Kanuni hizi zinaweka wajibu kwa Halmashauri kutoa kibali kwa mujibu wa Kanuni Na.124 kulingana na mchoro uliowasilishwa.

Vilevile, kanuni hizi zinaweka wajibu Mhandisi au Msanifu majengo kuandaa hesabu ya uzito wa vyuma vitakavyotumika kujenga jengo husika hii ni kwa mujibu wa Kanuni Na.143.

Kwa mantiki hiyo Halmashauri si Mamlaka pekee ya usimamizi wa majengo makubwa ya umma na /au binafsi ambayo matumizi yake ni kwa ajili ya biashara au shughuli nyinginezo za kibinadamu.Taasisi zifuatazo ni mamlaka za usimamizi ambazo zimeanzishwa na sheria ya Bunge:-

1. Bodi ya Wasanifu Majengo ,Wakadriaji Majengo ni mamlaka iliyoanzishwa na Sheria Na.16/1997( the Architects and Quantity Surveyors (Registration) Act [cap.269 R.E 2002] na mwaka 2010 sheria hii ilifanyiwa marekebisho ambayo kimsingi hayakuathiri majukumu yake. Fungu la 4 la sheria hii linaweka majukumu kwa chombo hiki kufanya yafuatayo;-

• Kusimamia shughuli na utendaji kazi wa wasanifu majengo ,wakadriaji majengo pamoja na kampuni zinazofanya kazi ya utalaamu ushauri katika kusimamia miradi ya ujenzi;

• Kuingia na kukagua shughuli zote za ujenzi unaofanyika hapa nchini kwa madhumuni ya kujiridhisha na kuhakikiksha kama kazi ya ujenzi inayofanyika inafanywa na mtu ambaye amesajiliwa na bodi na anazingatia taratibu,kanuni na sheria zote zinazosimamia ujenzi mijini; na

• Kuhakikisha kuwa maeneo yote ambako ujenzi unafanyika kumewekwa mabango yenye kuonyesha jina na anwani ya mradi, jina la mteja (mmiliki) , watalaamu washauri kwa maana wasanifu majengo na wahandisi pamoja na mkandarasi endapo atakuwa hakufanya hayo atachukuliwa hatua za kisheria.

2. Bodi ya Usajili wa Wahandisi ni mamlaka iliyoanzishwa na sheria Na.15/1997(the Engineers Registration, Act [Cap.63 R.E 2002]. Fungu la 4 la sheria hii linaweka majukumu kwa chombo hiki kufanya yafuatayo;-

• Kufuatilia na kusimamia shughuli na utendaji kazi wa wahandisi ikiwa ni pamoja na kampuni zinazofanya kazi ya utalaamu ushauri wa usimamizi wa miradi ya majenzi mijini;

• Kuingia na kukagua shughuli zote za ujenzi unaofanyika hapa nchini kwa madhumuni ya kujiridhisha na kuhakikiksha kama kazi ya ujenzi inayofanyika inafanywa na mtu ambaye amesajiliwa na bodi na anazingatia taratibu,kanuni na sheria zote zinazosimamia ujenzi mijini; na

• Kuhakikisha kuwa maeneo yote ambako ujenzi unafanyika kumewekwa mabango yenye kuonyesha jina na anwani ya mradi, jina la mteja (mmiliki) , watalaamu washauri kwa maana wasanifu majengo na wahandisi pamoja na mkandarasi endapo atakuwa hakufanya hayo atachukuliwa hatua za kisheria.

3. Bodi ya Wakandarasi [CRB] ni mamlaka iliyoanzishwa na sheria Na.17/1997( the Contractors Registration Act, [Cap.235 R.E 2002] Fungu la 4 la Sheria hii linaweka majukumu kwa chombo hiki kufanya yafuatayo;-

• Kusimamia shughuli na utendaji kazi wa Wakandarasi katika kujenga majengo imara na yenye kufuata viwango kwa mujibu wa michoro ya majengo hayo;

• Kuingia na kukagua shughuli zote za ujenzi unaofanyika hapa nchini kwa madhumuni ya kujiridhisha na kuhakikiksha kama kazi ya ujenzi inayofanyika inafanywa na mtu ambaye amesajiliwa na bodi na anazingatia taratibu,kanuni na sheria zote zinazosimamia ujenzi mijini; na

• Kuhakikisha kuwa maeneo yote ambako ujenzi unafanyika kumewekwa mabango yenye kuonyesha Jina na anwani ya mradi, jina la mteja (mmiliki) , Watalaamu washauri kwa maana wasanifu majengo na wahandisi pamoja na mkandarasi endapo atakuwa hakufanya hayo atachukuliwa hatua za kisheria.

4. Mamlaka nyingine ya usimamizi ni usalama mahali pa kazi (Occupational, Safety and Health Agency). Hiki ni chombo ambacho kinashiriki pia kusimamia miradi ya ujenzi mijini. Mamlaka hii hutoa kibali na kusajili mradi kama ambavyo mamlaka nyingine ambavyo zinafanya kwa kutoa "sticker".

5. Hitimisho.
Kama ilivyoonyeshwa hapo juu tumeona kwamba zipo sheria mbalimbali zenye kubainisha wadau wote wanaohusika na usimamizi wa majenzi mijini. Hivyo tunaomba ieleweke kwa umma kwamba Halmashauri ya Manispaa ya Ilala si mamlaka pekee ya usimamizi. Hii ni kwasababu muombaji wa kibali anapoomba na kukubaliwa baada ya kupitia michoro yake ambayo mara nyingi huwa imeandaliwa na Wasanifu na Wakadriaji majengo pamoja na "Structural Engineer" ambao wanasimamiwa na mamlaka zilizobainishwa hapo juu. Halmashauri huwa haina nafasi zaidi ya kitalaamu ya kusimamia katika masuala makubwa hasa ya vyuma na kiwango cha "material" yanayotumika katika ujenzi ; isipokuwa kufuatilia kama muombaji (mmiliki) anajenga kama ambavyo alionyesha katika michoro iliyopitishwa kwa mujibu wa mpango wa uendelezaji wa eneo husika.

________________________________
Imetolewa Na:
Mstahiki Meya
katika kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani (1/04/2013),
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
Dar- es - salaam.
 
Na afadhali maelezo yenyewe yangekuwa na maana. Lakini nilichokiona hapo ni kuwa Silaa na wenzake wanataka kujivua lawama. Sawa, Manispaa si msimamizi pekee, na wameonyesha wengine wanaohusika, Je, katika ile sehemu ambayo Manispaa inahusika, ilifanya nini ili kuepusha balaa hili? Hicho ndicho Silaa anapaswa kutueleza, si kutupia lawama taasisi nyingine.
Hizo taasisi nyingine tunazifahamu nazo tutazihoji zitoe maelezo kulingana na wajibu wake katika kusimamia ujenzi mijini.
Tafadhali Bwana Silaa, njoo na maenelezo ya kuonyesha Manispaa ilifanya nini kuepusha kadhia hii?

Huu utetezi mwingine ni kuzidi kutuongezea machungu tu.

Mtu ushaboronga halafu unazidisha kuboronga na boilerplate obscurantism.
 
5. Hitimisho.
Kama ilivyoonyeshwa hapo juu tumeona kwamba zipo sheria mbalimbali zenye kubainisha wadau wote wanaohusika na usimamizi wa majenzi mijini. Hivyo tunaomba ieleweke kwa umma kwamba Halmashauri ya Manispaa ya Ilala si mamlaka pekee ya usimamizi. Hii ni kwasababu muombaji wa kibali anapoomba na kukubaliwa baada ya kupitia michoro yake ambayo mara nyingi huwa imeandaliwa na Wasanifu na Wakadriaji majengo pamoja na "Structural Engineer" ambao wanasimamiwa na mamlaka zilizobainishwa hapo juu.
Halmashauri huwa haina nafasi zaidi ya kitalaamu ya kusimamia katika masuala makubwa hasa ya vyuma na kiwango cha "material" yanayotumika katika ujenzi ; isipokuwa kufuatilia kama muombaji (mmiliki) anajenga kama ambavyo alionyesha katika michoro iliyopitishwa kwa mujibu wa mpango wa uendelezaji wa eneo husika.

________________________________
Imetolewa Na:
Mstahiki Meya
katika kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani (1/04/2013),
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
Dar- es - salaam.

Sasa muheshimiwa mstahiki hapo mbona twachanganywa tena? Kama Halmashauri inafuatilia kile kichopo kwenye mchoro, iweje mchoro uelekeze ghorofa tisa kisha ujenzi uwe wa ghorofa 16?
Tatizo mnatufanya sisi waTZ machizi wote. Ila muda utafika tu.
 
Nikipenda hizo board zingine zituletee matamko yao..nashukuru baraza la madiwani la ilala kutuelimisha...
Ilala inabadilika sasa hata mji umeanza kupendeza..
 
Kwanza taarifa yenyewe ilivyoandikwa ni kama imeandikwa na wale watu wa kisomo cha watu wazima wa enzi za Nyerere. Halafu kama alivyosema mchangiaji mmoja, bado hajaonyesha kama alifanya kazi yake, sana sana amefanya kama mchezo wa mtoto mdogo anaposhikwa na kosa ankakimbilia kusema sio mimi peke yangu na fulani na fulani walikuwepo. Hawa ndio wasthiki meya wetu.
 
Nilichoelewa ni kwamba Meya anakili kosa la Manispaa ila inawataarifu watanzania kwamba sio wao peke yao.

Hitimisho.
Kama ilivyoonyeshwa hapo juu tumeona kwamba zipo sheria mbalimbali zenye
kubainisha wadau wote wanaohusika na usimamizi wa majenzi mijini. Hivyo tunaomba ieleweke kwa umma kwamba Halmashauri ya Manispaa ya Ilala si mamlaka pekee ya usimamizi. Hii ni kwasababu muombaji wa kibali anapoomba na kukubaliwa baada ya kupitia michoro yake ambayo mara nyingi huwa imeandaliwa na Wasanifu na Wakadriaji majengo pamoja na "Structural Engineer" ambao wanasimamiwa na mamlaka zilizobainishwa hapo juu. Halmashauri huwa haina nafasi zaidi ya kitalaamu ya kusimamia katika masuala makubwa hasa ya vyuma na kiwango cha "material" yanayotumika katika ujenzi ; isipokuwa kufuatilia kama muombaji (mmiliki) anajenga kama ambavyo alionyesha katika michoro iliyopitishwa kwa mujibu wa mpango wa uendelezaji wa eneo husika.
 
Back
Top Bottom