Maelezo kuhusu kodi ya ardhi na jengo

dominion

Member
Mar 8, 2017
25
13
Habarini wakuu!

Naombeni mnifahamishe kuhusu kozi za majengo na kodi ya ardhi(land tax)
Mfano: Mtu una nusu heka na kanyumba labda ka thamani ya 30 million na upo kwenye eleo la makazi ya watu, kodi hizo mbili zinakuwaje?

Sina uelewa ndiyo maana naomba mchango wenu, naogopa kuibiwa!
 
Habarini wakuu!
Naombeni mnifahamishe kuhusu kozi za majengo na kodi ya ardhi(land tax)
Mfano: mtu una nusu heka na kanyumba labda ka thamani ya 30 million na upo kwenye eleo la makazi ya watu...kodi hizo mbili zinakuwaje,sina uelewa ndiyo maana naomba mchango wenu,naogopa kuibiwa!

kwa mwaka unalipa 10% ya thamani ya nyumba..hii nikwamjibu wa TRA
 
Blaza mbn hapa unanipanikisha,sasa hapa watu si watauza nyumba zao ...duuh!
Inategemea na mkoa na halmashauri uliyopo, kodi ya jengo huwa ni kati ya 5,000 mpaka 20,000 kwa maeneo mengi ya ardhi (ukiondoa wale wenye mahekalu) alafu kodi ya ardhi nayo huwa between 11,000 mpaka 20,000. Kwahiyo kwa mwaka usihofu unaweza ukalipa kiwango kischozidi 50,000 kwa jengo na kiwanja (kiwango cha juu hiki mkuu nilichokupa)
 
Habarini wakuu!
Naombeni mnifahamishe kuhusu kozi za majengo na kodi ya ardhi(land tax)
Mfano: mtu una nusu heka na kanyumba labda ka thamani ya 30 million na upo kwenye eleo la makazi ya watu...kodi hizo mbili zinakuwaje,sina uelewa ndiyo maana naomba mchango wenu,naogopa kuibiwa!
Kodi ya Ardhi (Land Rent) ni ada ya kukodi Ardhi Serikalini. Nchi yetu inatumia mfumo wa lease hold, hivyo wamiliki wote wa Ardhi ni wapangaji mwenye Ardhi ni Serikali.

Kodi ya jengo ni ada ya kumiliki Mali (jengo) anaitwa property tax.

Hizi ni kodi mbili tofauti.
 
Kodi ya ardhi zamani walikuwa wanalipa walioko kwny maeneo yaliyopimwa, kwa sasa sijui kama utaratibu ni ule ule au. Kodi ya nyumba inategemea na aina ya nyumba, thamani, eneo iliyopo na pia matumizi mfano biashara au makazi kama Arusha nimelipa kodi ya mwaka jumla 70,000 kwa nyumba 2 za kupangisha (self ya rm 2 na 3) Nyumba ya kuishi nadhani 25,000(self rm 3)
 
Kodi ya Ardhi (Land Rent) ni ada ya kukodi Ardhi Serikalini. Nchi yetu inatumia mfumo wa lease hold, hivyo wamiliki wote wa Ardhi ni wapangaji mwenye Ardhi ni Serikali.

Kodi ya jengo ni ada ya kumiliki Mali (jengo) anaitwa property tax.

Hizi ni kodi mbili tofauti.

Inategemea na mkoa na halmashauri uliyopo, kodi ya jengo huwa ni kati ya 5,000 mpaka 20,000 kwa maeneo mengi ya ardhi (ukiondoa wale wenye mahekalu) alafu kodi ya ardhi nayo huwa between 11,000 mpaka 20,000. Kwahiyo kwa mwaka usihofu unaweza ukalipa kiwango kischozidi 50,000 kwa jengo na kiwanja (kiwango cha juu hiki mkuu nilichokupa)

Hapana haiwezi kuwa hivyo, haiwezi kuzidi 0.3% ya thamani ya jengo. Maeneo mengi inatozwa kati ya 0.005% hadi 0.1% ya thamani ya jengo.
Mazee shukran sana...nimepata kidogo hope na ujasiri kidogo....also mr. Jodoki eb nielezee kidogo kwa wenye mahekalu.
 
Kodi ya ardhi zamani walikuwa wanalipa walioko kwny maeneo yaliyopimwa, kwa sasa sijui kama utaratibu ni ule ule au. Kodi ya nyumba inategemea na aina ya nyumba, thamani, eneo iliyopo na pia matumizi mfano biashara au makazi kama Arusha nimelipa kodi ya mwaka jumla 70,000 kwa nyumba 2 za kupangisha (self ya rm 2 na 3) Nyumba ya kuishi nadhani 25,000(self rm 3)
Ndo maana Lukuvi ametangaza kufikia June wananchi wakaandikishe ardhi zao ili waweze kupewa hati na serikali ianze kukusanya chake
 
Sawa sawa massaiboi....asante sana....ni vizuri kujua ili tusije tukaibiwa na hawa watu
 
Mazee shukran sana...nimepata kidogo hope na ujasiri kidogo....also mr. Jodoki eb nielezee kidogo kwa wenye mahekalu.
Kimsingi kodi sio kubwa kivile, nilivyosema mahekalu nilimaanisha wakati mwingine kodi inatokana na maeneo uliyopo hasa yale ya wanene but all in all kodi sio kubwa kivile
 
Nimefurahi kufahamu....kwa sababu kuna mtu namfahamu anaplan ya kuuza nyumba kwa sababu ya taarifa za uongo kuhusu hii issue ya kodi
 
Kodi ya ardhi zamani walikuwa wanalipa walioko kwny maeneo yaliyopimwa, kwa sasa sijui kama utaratibu ni ule ule au. Kodi ya nyumba inategemea na aina ya nyumba, thamani, eneo iliyopo na pia matumizi mfano biashara au makazi kama Arusha nimelipa kodi ya mwaka jumla 70,000 kwa nyumba 2 za kupangisha (self ya rm 2 na 3) Nyumba ya kuishi nadhani 25,000(self rm 3)
fano mie nyumba ina fence na ina vyumba 4 vya kulala nalipa 20,000 kwa mwaka sawa tu na mtu aliejenga chumba na sebule, kwa mikoa kama Mwanza, Arusha na Dar ambapo nyumba ni nyingi huwa ni flat rate ila mikoa mingine huwa unalipa kulingana na ukubwa wa nyumba yako na decoration ulizoweka
 
Hapana haiwezi kuwa hivyo, haiwezi kuzidi 0.3% ya thamani ya jengo. Maeneo mengi inatozwa kati ya 0.005% hadi 0.1% ya thamani ya jengo.
Kodi ya nyumba uwa ni 0.15% ya thamani ya nyumba na ndio maana nyumba nyingi za zamani unakuta wanalipa Tshs15,000.
Wanachukulia thamani ya mwisho ya nyumba kwa apa mjini ni Tshs 10,000,000.
Mfano mzuri
Thamani ya nyumba ni
Tshs 10,000,000*0.15%= Tshs15,000.
 
Back
Top Bottom