Maelezo binafsi ya Mhe. Zitto Zuberi Kabwe dhidi ya tuhuma za rushwa kwa Umma

Jambo moja tu ambalo ningependa kufahamu kutokana na hii press release hii na ambalo sijapata kulifahamu ni hili;
Ni Taratibu zipi zilizokiukwa na bodi ya wakurugenzi ya Tanesco katika kumsimamisha kazi Mhando ili apishe uchunguzi??
 
Mkuu nimepitia maelezo yake ila still naona too general, hakuna facts za kutosha yeye akiwa kama mwenyekiti wa hiyo kamati ina maana hana clue zozote, mbona amekimbia hoja, yawezekana ni mtazamo wangu ila sioni kipya alichosema zaidi ya siasa tu

Ukiondoa chuki,utamwelewa. Na hana sababu ya kuongea zaidi ya hapo. Amesema aliingilia mgogoro hun kwa kufuata sheria,kanuni na taratibu. Kama wewe unasema ni uwongo,twambie amekosea wapi?
 
Hakuna jipya! Nilitarajia athibitishe kutohusika kwake katika sakata hilo!!!
 
Umetoa maelezo magumu mno hawezi kukuelwa huyu. Usibishane naye
 
zito mimi ni mwana chama wa chadema nanina ipenda sana chadema tena mapenz ya dhati kabisa ya kutoka moyoni lakini kwa taarifa nilizopewa na mtu wa karibu sana na muhando kuwa umekuwa ukionekana nyumbani kwa muhando mikocheni mara kwa mara je huwa unakwenda kufanya nini na hiyo mara ya mwisho kuonekana ni kabla ya habari ya gazeti la RAI kutoka na matokeo yake ndo hilo gazeti likatoa habari ya katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini na hata kabla ya hapo mtu aliyekuwa karibu sana wewe alikuwa akikusikia ukizungumza na simu kutoa maagizo juu ya taarifa itakayo andikwa kwenye gazeti na mengine mengi tu ambayo nikiyaa ndika hapa waweza juta kujiingiza kwenye mambo ya ajabu pasipo kujali kuwa chama chako saizi kina nafasi kubwa sana ya kutwaa dola ushauri wangu kwa zito umejisahau sana umebweteka unahitaji kukaa chini ukaangalia mstakabali wako nin ufanye kujisafisha ni mengi tuna jua kuhusu ww zito ila aitusaidi kuyaweka hapa adhalani tunachokuomba jirekebishe ili wananchi waendelee kuwa na imani na wewe.
 
mimi sijasema Zito hafai .. wala sijui wala siamini kama kuna mkakati wa kumshambulia zito hafai hapa jf ...nasikia kutoka kwako leo mkuu




Mkuu Smile,

Labda wewe ni mgeni humu jf jaribu kupitia threads za zitto zinaanzishwa ngapi? na uisome michango yake utakiona ninachokiona mimi.
 
Kazi yake ni kujichanganya ndio maana hawezi kusema wana jf wamempa ushauri kwakuwa anajua wanamchambua na kumwambia ukweli bila kumficha.
Narudia kusoma maelezo ya Zitto kuna kitu kinachanganya: Maelezo yake ya awali alisema tuhuma hizi ni vita ya URAIS na POSHO, leo naona sababu ni nyingine kabisaaa!
 

Mkuu Mohammed Shossi kwa nini Zitto hanakosa back up ktk chama chake na kwa nn anakua kama mtoto yatima ktk chama chake, pia ni kwa nini wana JF wengi wanampinga humu?
kwa mtazamo wako tu
 
Last edited by a moderator:
Jambo moja tu ambalo ningependa kufahamu kutokana na hii press release hii na ambalo sijapata kulifahamu ni hili;
Ni Taratibu zipi zilizokiukwa na bodi ya wakurugenzi ya Tanesco katika kumsimamisha kazi Mhando ili apishe uchunguzi??

Mkuu Mwita Maranya,majibu amayatoa hapo juu kwamba Kamati iliwaita Bodi, PPRA, na CAG kupata maelezo ya kutosha juu ya hatua iliyochukuliwa na Bodi kumsimamisha kazi CEO wa Tanesco ktk kipindi nyeti kabla ya Bajeti ya Wizara ya Madini na Nishati.
 
Bwata weee uchunguzi ukikamilika tutakwambia, Vp Urais nani alikutuma kupayuka mapema yote hii?
 

Bado ZZK ana maswali ya kujibu.....Kwenye unapaswa kuwataja ili tuweze kuoanisha ushiriki wao kwenye hili sakata na ukisemacho....kwakuwa umeshajipambanua kusema ukweli daima....
Kwenye Naona kama unajitabiria mwenyewe.....angalia usijejikaanga kwa mafuta yako wewe...
Kwenye Tunahitaji kujua ni kanuni ipi ilikiukwa kumsimamisha Mhando??
Kwenye naNi wazi kuwa huna imani na chama chako na hata tulio nje tumeanza kuona kuwa ni kama chama ahako kinapoteza imani na wewe....Hii ni kutokana na utaratibu wako wa kutekeleza sera za chama tawala ukiwa upinzani... amua moja....
 
wakati umefika kila lilifichika linatoka hadharani..ikumbukwe kwamba ni zitto huyuhuyu aliye ungamkono hoja ya kupandishwa kwa bei ya mafuta ya taakwa kisingizio cha kukomesha uchakachuaji, kama hiyo haitoshi ni zitto huyohuyo ndiye aliye piga kelele serekali inunue mitambo iliyo tumika ya ilyokuwa kampuni pacha ya richmond yaani dowans huku akijua fika ni kinyume cha sheria ya manunuzi ya umma..nadhani mmesahau kuwa zitto alishauriwa na watu wengi ikiwemao chama chake asiingie kwenye iliyokuwatume ya uchunguzi wa sakata la dowans kwa walio kwepo pale kona ya mlimani walisikia majibu aliyotoa..alisema hivi 'nimesikia mliyoyasema ila maamuzi juu ya hili suala ni yangu' huku akitahadharishwa kwamba waliokua kwenye kamati wengi ndio wahusika wa tuhuma zenyewe kesho yake tukasika zitto kakubali kuingia kwenye kamati na akahusika kuisafisha dowans,sasa mimi kwa maoni yangu zitto tunae muona leo ndiye zitto halisio mwenye tamaa na mwenye kuweka maslahi yake mbele..haya ni maoni yangu tu.ila zitto kwa sasa ni mtuhumiwa mpaka sheria itakapomtia hatiani nadio tunaweza kausema kuwa ni mwizi au fisadi,au mla rushwa ila mimi simuamini tena.
 
I think Zitto hana haja ya kusema yote haya! Apige kimya tu! Always ukweli huwa unajitenga at the end of the day!

Nashindwa kuelewa ni kwanini ameshindwa kabisa, kabisa kuwa 'calm'.

Hata mimi nashangaa sana kwanini inaonekana kama 'anatapatapa' sana, ooh mara nitaongea na vyombo vya habari, mara sms kwa Maswi, mara nimeomba chama kinichunguze, why all that?!!nadhani hata kama ni kuongea, angeongea kifupi sana, maana kama ukweli upo, upo tu-hata kama utacheleweshwa!
 

hapa atakuwa anamzungumzia mbatia tu hakuna mwingine!!!!!!!!!!!!!
 




Pamoja na hayo uliyoyataja, mimi nimeona haya:



Kwanza nadhani ingekuwa busara kumtaja mwandishi huyo wa habari. Unamuamini kiasi gani? Siku akija kukataa je kuwa hakukuambia hayo? Tuwe na tahadhari na baadhi ya waandishi wa habari.

Pili, nahisi busara hazikutumika kidogo kwa kuamini kwako maneno aliyokuambia huyo mwandishi bila ya kuthibitisha kwanza kama kweli aliambiwa na Waziri na Katibu wake. Hakuna uwezekanao kuwa mwandishi huyo alikuambia uongo?, na kama ni uongo, huoni kama utakuwa umekosea kuwahusisha Mhe. Waziri na Katibu wake na sakata la kuwa wao ndio wanaoshiriki kueneza tuhuma dhidi yako?
 

Jiadharini na tabia iliyojengeka ya CCM ya kumtetea mtu kisa "Huyu ni mwenzetu". Mara zote upofu huu usababishwa na mawazo potofu ya "anasakamwa kwa vile ni mwenzetu!"

Ushauri wangu kwa CDM ni kuakisha uchunguzi huru na wakina unafanyika ili kuondoa mashaka kwa matokeo ya huo uchunguzi. Na baada ya hapo kama Zitto atakuwa "innocent kama wanavyoamini wana-CDM" basi washangilie na kama atakuwa "guilty" basi wamwajibishe.

Mkuu kwa mtindo huo chama cha siasa kitaonekana ni chama mbele ya jamii. And mark my words "Hili ndilo lisilokutikana ndani ya CCM"!
 
Ple sana Mh. Zito, lakini keep up mapambano against Uonevu wa wanyonge. make kwa nchi inayoendeshwa na rais dhaifu na chama dhaifu yote yanawezekana. Tususbiri uchunguzi make si kuna wale waliokutuhumu nao watajieleza kwaninini wamekutuhumu? then kama ni uongo utawachukulia hatua?
 

Jomba uko darasa la ngapi?
Wewe ni fisadi sana eeh?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…