Maelezo binafsi ya Mhe. Zitto Zuberi Kabwe dhidi ya tuhuma za rushwa kwa Umma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maelezo binafsi ya Mhe. Zitto Zuberi Kabwe dhidi ya tuhuma za rushwa kwa Umma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Maganga Mkweli, Aug 1, 2012.

 1. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #1
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,097
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE DHIDI YA TUHUMA ZA RUSHWA HUSUSAN KUELEKEA KATIKA KUPITISHA BAJETI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI  Ndugu Waandishi,

  Nalazimika kukutana nanyi kutoa maelezo juu ya tuhuma zenye shinikizo la kisiasa zinazoelekezwa kwangu binafsi kwamba hata mimi nimeshiriki katika vitendo vya rushwa, kwa nafasi yangu kama Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma. Taarifa hizo, kama kawaida ya uzushi mwingine wowote zimesambazwa kimkakati na kwa kasi kubwa kiasi cha kuukanganya umma.

  Nafahamu nabeba dhamana kubwa ya uongozi, taswira yangu ya uongozi daima imeakisi njozi na matumaini ya wananchi wa Kigoma Kaskazini, wananchi wanyonge na vijana kote nchini bila kujali itikadi zao za kisiasa, jinsia zao, makabila yao na rika zao. Hivyo, nawajibika kupitia kwenu kuwatoa hofu juu ya hisia potofu zinazopandikizwa kwao na wale wasiopenda kuona baadhi yetu tukiwaunganisha na kuwasemea watanzania wasio na sauti, dhidi ya vitendo vya hujuma na vyenye dhamira ovu kwa taifa.

  Mkakati huo wa kuniunganisha na baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wanaotuhumiwa kwa kupokea Rushwa unatekelezwa kwa njia zifuatazo:


  1. Kumekuwa na kauli za watendaji wa serikali ambao wamekuwa wakizieneza na hususan kutoa taswira kwamba baadhi ya kauli zangu zinatokana na ushawishi wa rushwa;
  2. Kuna taarifa ambazo zimeandikwa tena katika kurasa za mbele za baadhi ya vyombo vya habari zikidai ''Zitto kitanzini'' ama ''Zitto sawa na popo nundu'' zikiashiria kwamba na mimi ni mla rushwa; na
  3. Waandishi wa habari na jamii kwa ujumla wamefikia kuaminishwa habari hizi kiasi cha wengine kuuliza kwa nini Mhe. Zitto Kabwe hakutajwa katika orodha iliyotolewa na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani.

  Ndugu Waandishi,
  Naomba kutoa ufafanuzi wa hicho kinachoelezwa kwamba nina ushiriki katika masuala ya rushwa hususan kwenye masuala yanayohusu sekta ya Nishati na Madini:-


  1. Mara baada ya bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Usambazaji wa Umeme Tanzania (TANESCO) chini ya Uenyekiti wake Meja Jenerali Mstaafu Robert Mboma kutangaza kwamba imemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Nd. William Mhando ili kupisha uchunguzi wa baadhi ya vitendo/mwenendo wake, Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) ambayo mimi ni Mwenyekiti wake ilimuandikia Mhe. Spika kumuomba aridhie ili Kamati iweze kuwaita Bodi ya TANESCO, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali (CAG) na pia Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kujiridhisha na tuhuma zote zinazotajwa zinafanyiwa uchunguzi wa kina na hatua kuchukuliwa;
  2. Kamati ya POAC ninayoiongoza ilimuomba Mhe. Spika kuwaita wahusika tajwa kwa kuwa zilikuwapo tetesi kuwa kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi huyo siku chache kabla ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kulikuwa na lengo la kufunika 'madudu' makubwa zaidi kwa kulichagiza Bunge na tukio hilo dogo, mkakati ambao naona umefanikiwa sana. Isitoshe, Kamati kutaka kujiridhisha na hatua za Bodi ni sehemu ya msingi ya utekelezaji wa majukumu ya Kamati yaliyowekwa kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge na pia Shirika la TANESCO ni moja kati ya mashirika ambayo yanawajibika kwetu kwa hesabu zake na pia ufanisi wake kwa ujumla. Tumefanya hivyo pia katika mashirika mengine, hili la TANESCO sio tukio la kipekee;
  3. Kitendo hiki cha halali na kwa mujibu wa Kanuni kilichofanywa na Kamati yangu kimetafsiriwa kwa makusudi na baadhi ya watu kwamba ni ishara ya kuwa sisi au zaidi kwamba mimi nina maslahi binafsi na TANESCO na hususan Mkurugenzi wake Injinia Mhando, ndio maana tumetaka maelezo ya Bodi. Ukweli kwamba Kamati ya POAC tumewaita pia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu (CAG) na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kwa jambo hilo hilo umefichwa kwa makusudi!
  4. Baada ya tukio hilo, nikiwa hapa Dodoma, mwandishi wa habari wa gazeti moja alinifuata akiniambia kuwa wamekutana na Mhe. Waziri Mhongo na Katibu Mkuu wake, Nd. Eliachim Maswi hapa hapa Bungeni na wamewaambia kuwa mimi nimepewa rushwa. Hakutaja nimepewa rushwa na nani, kiasi gani na wala kwa lengo gani!
  5. Nimejaribu kumtafuta kwa simu Mhe. Waziri Mhongo na Katibu Mkuu wake ili wanipe ufafanuzi juu ya mimi na Kamati ya POAC kuhusishwa na tuhuma hizi bila mafanikio, hali ambayo inaniondolea mashaka juu ya ushiriki wao katika kueneza au kuthibitisha uvumi huo. Najaribu sana kujizuia kutokuwa na mashaka na ushiriki wao huo ikizingatiwa uzito na taswira ya nafasi zao katika jamii, lakini wameshindwa kunidhihirishia tofauti.

  Sasa naomba kutoa ufafanuzi rasmi kuhusu mlolongo wa matukio hayo tajwa ambayo yanatumiwa na baadhi ya wanasiasa kuonesha kwamba eti nimehusika na vitendo vya rushwa.  • Binafsi sijawahi kuwa na mawasiliano ya aina yeyote na uongozi wa TANESCO kushawishiwa juu ya hatua ambazo POAC ndio imezichukua za kutaka kujiridhisha juu ya utaratibu uliotumika. Ieleweke wazi kabisa kuwa, hakuna wakati wowote, popote ambapo mimi binafsi au Kamati yetu imekataa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO kuchunguzwa kwa tuhuma zozote. Ambacho tumesisitiza wakati wote ni ufuatwaji wa taratibu, kanuni na sheria, hili nitalisimamia iwe masika au kiangazi;
  • Ni kwa sababu hiyo, na kwa kujiamini kabisa nimeunga mkono suala la tuhuma za rushwa zinazotajwa zichunguzwe na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa kina;
  • Nimekwenda mbali zaidi kukiomba chama changu CHADEMA kifanye pia uchunguzi na tathmini yake kwa kina kujiridhisha na tuhuma hizo;
  • Natumia fursa hii pia kuomba vyombo vya Dola vichunguze tuhuma hizo kwa nafasi yake ili kuweza kupata ukweli;
  • Ninaahidi kushiriki kikamilifu iwapo nitatakiwa katika uchunguzi wowote utakaofanywa na niko tayari kuwajibika iwapo nitakutwa na hatia yeyote.

  Napenda niwatoe hofu wananchi wa jimbo la Kigoma Kaskazini walionituma kuja kuwawakilisha hapa Bungeni na Watanzania wote kwa ujumla kwamba:-


  1. Mimi Zitto Zuberi Kabwe sina bei, sijawahi kuwa nayo na sitarajii kuwa nayo huko mbeleni. Daima nimesimamia kidete maadili ya uongozi bora katika maisha yangu yote ya siasa, na nawaahidi sitarudi nyuma katika mapambano dhidi ya rushwa katika nchi hii pamoja na mikakati ya aina hii ya kunidhoofisha na kunivunja moyo;
  2. Nafarijika na salam mbali mbali zinazotolewa kunifariji na kusisitiza kuwa nisilegeze kamba katika mapambano haya, nimepokea ujumbe mwingi kwa simu, sms, tweeter na hata facebook na niko pamoja nanyi Watanzania wenzangu kamwe sitarudi nyuma hadi kieleweke. Naamini katika nchi yetu tunazo rasilimali za kutosha mahitaji/haja ya kila mmoja wetu lakini si ‘tamaa/ulafi' wa baadhi ya watanzania wenzetu;
  3. Napenda kuweka rekodi sawa kwa Watanzania kwamba nimekuwa Mbunge hiki ni kipindi cha pili, Mimi ni Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) huu ni takriban mwaka wa saba sasa, Kamati yangu inasimamia mashirika 259 ya Umma na si TANESCO peke yake. Mchango wa Kamati hii katika Bunge na kwa ustawi wa Mashirika ya Umma ni bayana na haujawahi kutiliwa shaka. Kamati yetu imeokoa upotevu mkubwa wa mali za umma na kuokoa fedha za umma kutokana na umakini wake. Tumefanya hivyo CHC hivi karibuni, Kiwira na kwenye mashirika mengine mengi. Kote huko uadilifu na uzalendo wa Kamati hii haujawahi kuhojiwa. Inatuwia vigumu kuona kuwa tunahojiwa katika suala hili la TANESCO. Hapa pana kitendawili.
  4. Zipo hoja pandikizi za kutaka Kamati ya POAC ivunjwe na haswa zikinilenga mimi binafsi. Nafahamu kiu ya wasioitakia mema nchi yetu kuiona POAC ikivunjwa au sura zikibadilishwa kwa kuwa Kamati hii imekuwa mwiba kwa mikakati yao ya kifisadi. Kwa maoni yangu, Kamati ya POAC isihusishwe na tuhuma hizi kwa vyovyote vile. Niko tayari nihukumiwe mimi kama mimi na sio kuhusisha wajumbe wengine ambao hawatajwi mahala popote katika tuhuma hizi mbaya sana katika historia ya Bunge letu. Nitakuwa tayari kunusuru Kamati ya POAC na maslahi ya taifa letu kwa kujiuzulu Uenyekiti iwapo itathibitika pasipo shaka kuwa nimehongwa. Kamati ya POAC ni muhimu zaidi kuliko mimi.
  5. Nafahamu pia kuwa kuna wanasiasa hasa wa Upinzani ambao wanautaka sana Uenyekiti wa POAC na wanafanya kila njia kutaka kuidhoofisha. Lakini hawajui kuwa anaepanga wajumbe wa Kamati ni Spika wa Bunge.
  6. Msishangae pia kuja baadae kubaini kwamba baadhi ya wanasiasa wenye midomo mikubwa ya kutuhumu wenzao wao ndio vinara wa kupokea rushwa.
  7. Ni lazima tufike mahali kama viongozi kwamba utaratibu unapokiukwa na yeyote yule, au uongo unapotolewa hadharani tuseme bila kuogopa. Hili ndio jukumu letu kama wabunge na viongozi. Kusimamia ufuatiliaji wa utaratibu ni jukumu letu kama Kamati ya POAC na ndio sababu ya msingi ya kuanzishwa kwa mamlaka kama CAG na PPRA. Haiwezekani, tuwe na set ya kanuni kwa kundi fulani na nyingine kwa makundi mengine, au kuhukumu ufuataji wa taratibu kwa kuangalia sura ya mtu usoni

  Mwisho

  Kumejengeka tabia hivi sasa ya kuwamaliza wanasiasa wenye kudai uwajibikaji na uzalendo. Kumeanzishwa kiwanda kwenye medani ya siasa cha kuzalisha majungu na fitna zenye lengo la kuwachonganisha wanasiasa wa aina hiyo na wananchi kwa kutumia vyombo vya habari na nguvu ya fedha. Naamini mbinu hizi chafu, kama nyingine nyingi zilizojaribiwa kwangu huko nyuma nazo zitashindwa.

  Naamini katika kweli na kweli daima huniweka huru. Naamini kuwa mwale mdogo wa mwanga wa mshumaa hufukuza kiza. Kwa imani hiyo, sitasalimu amri mbele ya dhamira zao ovu hata nitakapobaki peke yangu katika mapambano hayo ya kulinda na kutetea rasilimali za taifa zinufaishe watanzania wote.

  Daima nitaongozwa na busara ya Hayati Shabaan Robert isemayo, ‘Msema kweli huchukiwa na marafiki zake, nitakapofikwa na ajali hiyo, sitaona wivu juu ya wale wawezao kudumu na marafiki zao siku zote, siwezi kuikana kweli kwa kuchelea upweke wa kitambo, nikajitenga na furaha ya kweli itakayotokea pale uwongo utakapojitenga".

  Ahsanteni sana.
   
 2. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Well said,

  Ila kama ulivyosema tuiachie kamati ya kinga na maadili ya Bunge ichunguze kila kitu na wale walio wasafi na wachafu pumba na mchele utaonekana.

  Mapambano yapo Mhe Zitto na sio madogo ila unapokuwa mpambanaji kubali yote.

  Kuna kuanikwa mpaka siri zako za ndani ili kuwadhoofisha wale ambao wanapambana ili tuu kukuvunja moyo usipambane ila kama unaamini katika Mungu yote ni mapito wanasema utashinda na mnafiki mwishowe atajionyesha
   
 3. n

  ngozimbili JF-Expert Member

  #3
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 823
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 60
  Loud n clear
   
 4. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #4
  Aug 1, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Swali kwa ZITTO. sababu hii kimati inaonekana kuwa uchochoro wa kukuchafua, ukizingatia kwamba watanzania wote wanajua kwamba serikali yetu haisikilizi ushauri wa kamati yako, ama kwa sababu pia watanzania hawawezi kuona impact ya kamati yako katika uboreshaji wa uendeshaji wa mashirika yetu ya uma, wewe binafsi umeishaanza kufikiria kuachana na hiyo kamati ili ujikite kwenye siasa zenye tija zaidi kwa taifa letu, hasa zile zinazojielekeza katika kuhahakikisha kwamba mwaka 2015 ndio mwisho wa CCM kuwa na mamlaka ya kuongoza serikali yetu?

  Nakuuliza swali hili kwa sababu, kwa wingi zaidi, watanzania wanaona kama style ya siasa zako, hasa jinsi unavyoambatana na mambo ya utawala wetu katika siku za karibuni zinakinzana na njia wanayoelekea wanasiasa wengine ndani ya chama chako, of course na watanzania wengi kwa ujumla.
   
 5. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #5
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  mgangaukweli hamna jipya hapo bado ni ngonjera tu.Mnyumbuliko wa wa maneno ni kutafuta huruma ya umma.Naona maswali ni mengi kuliko majibu mazito.Kwa nini asitoe facts za ukweli?.

  Mwandishi gani alimwambia kuwa Maswi Kamtaja ZZK kupokea hongo?kwa nini asimtaje?.Tatizo la kufanya uswahiba na makanjanja hadi unawandikia habari kama yule wa Mwananchi."Shemtawa" ndiyo madhara yake.

  Mwanzoni watu walilia nafasi ya Uwaziri Mkuu sakata la Lowasa sasa ni nafasi ya Uenyekiti wa POAC na sakata la ZZK.Kwa ujumla ZZK taarifa yako imejaa unafiki na hila zaidi.

  Rejea "Nitamtetea Mhando sana arejeshwe maana najua namimi (ZZK) mhathirika wa uonevu".Naishia hapo naona kuchambua taarifa hiyo inaweza kujaza page kama tano hivi.
   
 6. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #6
  Aug 1, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu zitto ,usiwe na wacwac,mwisho wa siku ukweli utajitenga na uongo
   
 7. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #7
  Aug 1, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Nimependa sana hitimisho.
   
 8. n

  nsanu Member

  #8
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 26, 2012
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ngoja ntarudi tena kuisoma vizuri, now mishe mishe mingi, si mjaua tena kutafuta cha'paaaa
   
 9. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #9
  Aug 1, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Nataka kujiaminisha kuwa Prof Muhongo si mwanasiasa ila ni mtu anayelenga kulinda mali na rasilimali za Taifa! Kitu cha kuhoji hapa ni je sheria ya manunuzi inaweza kutumika kuhujumu nchi? Na kama ndiyo basi inabidi ifanyiwe marekebisho fasta ili isiendelee kuwanufaisha wajanja wachache!
   
 10. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #10
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  1. Nafahamu pia kuwa kuna wanasiasa hasa wa Upinzani ambao wanautaka sana Uenyekiti wa POAC na wanafanya kila njia kutaka kuidhoofisha. Lakini hawajui kuwa anaepanga wajumbe wa Kamati ni Spika wa Bunge.
  2. Msishangae pia kuja baadae kubaini kwamba baadhi ya wanasiasa wenye midomo mikubwa ya kutuhumu wenzao wao ndio vinara wa kupokea rushwa
  hapo red sijaelewa zzk....mmmh
   
 11. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #11
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  He is confident maybe hizo tuhuma ndio ziile "gutter politics" zilizobobea CCM it's time for CDM now to stand with him.. Ili waendelee kuwaumbua hawa mabaradhuli, eti naskia na Ole Sendeka ndani! Kweli Mungu hamfichi mnafki.
   
 12. S

  Sessy Senior Member

  #12
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tusubiri uchunguzi tu ukweli na uongo utajulikana
   
 13. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #13
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Ngoja nikale kwanza chakula cha mchana
   
 14. Asabaya

  Asabaya JF-Expert Member

  #14
  Aug 1, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 1,317
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  ukweli haujifichi.
   
 15. Ngongoseke

  Ngongoseke JF-Expert Member

  #15
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 3,212
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Umeongea vizuri sana mwenye ushahidi wake wakuwa umepokea rushwa atoe sio kuleta majungu tu,
   
 16. t

  thatha JF-Expert Member

  #16
  Aug 1, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  hamna jipya hapo, dogo umekula mlungula!
   
 17. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #17
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Kuna vitu vingine hata hakutakiwa kuongea bwana ..zaidi anazidi kuharibu cheki hiki kipengele
  1. Nafahamu pia kuwa kuna wanasiasa hasa wa Upinzani ambao wanautaka sana Uenyekiti wa POAC na wanafanya kila njia kutaka kuidhoofisha. Lakini hawajui kuwa anaepanga wajumbe wa Kamati ni Spika wa Bunge.
  2. Msishangae pia kuja baadae kubaini kwamba baadhi ya wanasiasa wenye midomo mikubwa ya kutuhumu wenzao wao ndio vinara wa kupokea rushwa.....

   
 18. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #18
  Aug 1, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 925
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Umesomeka Mkuu Zitto Kabwe.Mungu atakukinga na fitna mbaya za wasiokupenda wote.
   
 19. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #19
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Maneno mazito hayo ZZK

  Naona umeachana na maneno ya kukataa mkurugenzi asisimamishwe kazi kwani ni sehemu ya uchunguzi

  Ufafanuzi wako haujaweka jipya lolote umeibua maswali zaidi
   
 20. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #20
  Aug 1, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  haya sasa
   
Loading...