Maelezo binafsi ya Mhe. Zitto Zuberi Kabwe dhidi ya tuhuma za rushwa kwa Umma

I think Zitto hana haja ya kusema yote haya! Apige kimya tu! Always ukweli huwa unajitenga at the end of the day!

Nashindwa kuelewa ni kwanini ameshindwa kabisa, kabisa kuwa 'calm'.

Ukimya pia unatafsiriwa katika namna nyingi. Atuliaje katika mazingira kama hayo? Nakumbuka Sumaye alipigwa madongo mengi sana lkn akaamua kukaa kimya na umma ukajua yanayosemwa yote ndivyo yalivyo, alikuja kung'amua wakati kishachelewa.

Anna wajibu wa kusema kile anachoamini ni kweli, ikichanganywa na story za upande wa pili umma utang'amua nini kweli nini uongo lkn kukaa kimya si dawa.
 
  1. Nafahamu pia kuwa kuna wanasiasa hasa wa Upinzani ambao wanautaka sana Uenyekiti wa POAC na wanafanya kila njia kutaka kuidhoofisha. Lakini hawajui kuwa anaepanga wajumbe wa Kamati ni Spika wa Bunge.
  2. Msishangae pia kuja baadae kubaini kwamba baadhi ya wanasiasa wenye midomo mikubwa ya kutuhumu wenzao wao ndio vinara wa kupokea rushwa
hapo red sijaelewa zzk....mmmh

.
Humjui Mbatia?
Mimi najiuliza na bado sijapata jibu. Ni nani aliyesema kuwa Zitto kapewa rushwa? Na alisema kwa nani? Hivi kanuni zilizopitishwa na bunge na maneno ya waziri/katibu kujinasua katika tuhuma kwa kutuhumu ni kipi chenye kipaumbela bungeni? Mkakati wa wanasiasa katika vyama vyao kujinasua katika kupoteza nafasi zao ndani ya vikao vya vyama vyao nao ni sehemu ya bunge kwamba spika awekee hayo maazimio ya vyama kinga ya bunge?
Bunge letu limepoteza uadilifu na heshima lililojiwekea toka uhuru ni kwa sababu ya kiti kukaliwa na jinsia inayotiliwa shaka katika jamii kwa kuamini kuwa hakina utashi wake chenyewe ila kile inachowekewa? Mungu lisaidie taifa letu na bunge lanke kurejasha heshima na imani ya wananchi wake ambayo wameipoteza kwalo.
.
 
mimi kwa kweli zitto anazidi kujichanganya na kutuchangaya...hivi mbona haweki wazi ni sheria zipi zilizovunjwa na zimevunjwaje? kweli anataka kutufanya watu wote wajinga hatujui ni maamuzi gani yenye tija kwa taifa?
zitto kukweli naona unazidi kujichafua na kimbelembele chako na ujuaji vitakuponza badilika kaka....kama sheria haina maslahi ya umma ni bora ukaivunja na utaonekana hero.
 
MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE DHIDI YA TUHUMA ZA RUSHWA HUSUSAN KUELEKEA KATIKA KUPITISHA BAJETI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI



Ndugu Waandishi,

Nalazimika kukutana nanyi kutoa maelezo juu ya tuhuma zenye shinikizo la kisiasa zinazoelekezwa kwangu binafsi kwamba hata mimi nimeshiriki katika vitendo vya rushwa, kwa nafasi yangu kama Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma. Taarifa hizo, kama kawaida ya uzushi mwingine wowote zimesambazwa kimkakati na kwa kasi kubwa kiasi cha kuukanganya umma.

Nafahamu nabeba dhamana kubwa ya uongozi, taswira yangu ya uongozi daima imeakisi njozi na matumaini ya wananchi wa Kigoma Kaskazini, wananchi wanyonge na vijana kote nchini bila kujali itikadi zao za kisiasa, jinsia zao, makabila yao na rika zao. Hivyo, nawajibika kupitia kwenu kuwatoa hofu juu ya hisia potofu zinazopandikizwa kwao na wale wasiopenda kuona baadhi yetu tukiwaunganisha na kuwasemea watanzania wasio na sauti, dhidi ya vitendo vya hujuma na vyenye dhamira ovu kwa taifa.

Mkakati huo wa kuniunganisha na baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wanaotuhumiwa kwa kupokea Rushwa unatekelezwa kwa njia zifuatazo:


  1. Kumekuwa na kauli za watendaji wa serikali ambao wamekuwa wakizieneza na hususan kutoa taswira kwamba baadhi ya kauli zangu zinatokana na ushawishi wa rushwa;
  2. Kuna taarifa ambazo zimeandikwa tena katika kurasa za mbele za baadhi ya vyombo vya habari zikidai ’’Zitto kitanzini’’ ama ’’Zitto sawa na popo nundu’’ zikiashiria kwamba na mimi ni mla rushwa; na
  3. Waandishi wa habari na jamii kwa ujumla wamefikia kuaminishwa habari hizi kiasi cha wengine kuuliza kwa nini Mhe. Zitto Kabwe hakutajwa katika orodha iliyotolewa na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani.

Ndugu Waandishi,
Naomba kutoa ufafanuzi wa hicho kinachoelezwa kwamba nina ushiriki katika masuala ya rushwa hususan kwenye masuala yanayohusu sekta ya Nishati na Madini:-


  1. Mara baada ya bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Usambazaji wa Umeme Tanzania (TANESCO) chini ya Uenyekiti wake Meja Jenerali Mstaafu Robert Mboma kutangaza kwamba imemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Nd. William Mhando ili kupisha uchunguzi wa baadhi ya vitendo/mwenendo wake, Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) ambayo mimi ni Mwenyekiti wake ilimuandikia Mhe. Spika kumuomba aridhie ili Kamati iweze kuwaita Bodi ya TANESCO, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali (CAG) na pia Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kujiridhisha na tuhuma zote zinazotajwa zinafanyiwa uchunguzi wa kina na hatua kuchukuliwa;
  2. Kamati ya POAC ninayoiongoza ilimuomba Mhe. Spika kuwaita wahusika tajwa kwa kuwa zilikuwapo tetesi kuwa kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi huyo siku chache kabla ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kulikuwa na lengo la kufunika ’madudu’ makubwa zaidi kwa kulichagiza Bunge na tukio hilo dogo, mkakati ambao naona umefanikiwa sana. Isitoshe, Kamati kutaka kujiridhisha na hatua za Bodi ni sehemu ya msingi ya utekelezaji wa majukumu ya Kamati yaliyowekwa kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge na pia Shirika la TANESCO ni moja kati ya mashirika ambayo yanawajibika kwetu kwa hesabu zake na pia ufanisi wake kwa ujumla. Tumefanya hivyo pia katika mashirika mengine, hili la TANESCO sio tukio la kipekee;
  3. Kitendo hiki cha halali na kwa mujibu wa Kanuni kilichofanywa na Kamati yangu kimetafsiriwa kwa makusudi na baadhi ya watu kwamba ni ishara ya kuwa sisi au zaidi kwamba mimi nina maslahi binafsi na TANESCO na hususan Mkurugenzi wake Injinia Mhando, ndio maana tumetaka maelezo ya Bodi. Ukweli kwamba Kamati ya POAC tumewaita pia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu (CAG) na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kwa jambo hilo hilo umefichwa kwa makusudi!
  4. Baada ya tukio hilo, nikiwa hapa Dodoma, mwandishi wa habari wa gazeti moja alinifuata akiniambia kuwa wamekutana na Mhe. Waziri Mhongo na Katibu Mkuu wake, Nd. Eliachim Maswi hapa hapa Bungeni na wamewaambia kuwa mimi nimepewa rushwa. Hakutaja nimepewa rushwa na nani, kiasi gani na wala kwa lengo gani!
  5. Nimejaribu kumtafuta kwa simu Mhe. Waziri Mhongo na Katibu Mkuu wake ili wanipe ufafanuzi juu ya mimi na Kamati ya POAC kuhusishwa na tuhuma hizi bila mafanikio, hali ambayo inaniondolea mashaka juu ya ushiriki wao katika kueneza au kuthibitisha uvumi huo. Najaribu sana kujizuia kutokuwa na mashaka na ushiriki wao huo ikizingatiwa uzito na taswira ya nafasi zao katika jamii, lakini wameshindwa kunidhihirishia tofauti.

Sasa naomba kutoa ufafanuzi rasmi kuhusu mlolongo wa matukio hayo tajwa ambayo yanatumiwa na baadhi ya wanasiasa kuonesha kwamba eti nimehusika na vitendo vya rushwa.



  • Binafsi sijawahi kuwa na mawasiliano ya aina yeyote na uongozi wa TANESCO kushawishiwa juu ya hatua ambazo POAC ndio imezichukua za kutaka kujiridhisha juu ya utaratibu uliotumika. Ieleweke wazi kabisa kuwa, hakuna wakati wowote, popote ambapo mimi binafsi au Kamati yetu imekataa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO kuchunguzwa kwa tuhuma zozote. Ambacho tumesisitiza wakati wote ni ufuatwaji wa taratibu, kanuni na sheria, hili nitalisimamia iwe masika au kiangazi;
  • Ni kwa sababu hiyo, na kwa kujiamini kabisa nimeunga mkono suala la tuhuma za rushwa zinazotajwa zichunguzwe na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa kina;
  • Nimekwenda mbali zaidi kukiomba chama changu CHADEMA kifanye pia uchunguzi na tathmini yake kwa kina kujiridhisha na tuhuma hizo;
  • Natumia fursa hii pia kuomba vyombo vya Dola vichunguze tuhuma hizo kwa nafasi yake ili kuweza kupata ukweli;
  • Ninaahidi kushiriki kikamilifu iwapo nitatakiwa katika uchunguzi wowote utakaofanywa na niko tayari kuwajibika iwapo nitakutwa na hatia yeyote.

Napenda niwatoe hofu wananchi wa jimbo la Kigoma Kaskazini walionituma kuja kuwawakilisha hapa Bungeni na Watanzania wote kwa ujumla kwamba:-


  1. Mimi Zitto Zuberi Kabwe sina bei, sijawahi kuwa nayo na sitarajii kuwa nayo huko mbeleni. Daima nimesimamia kidete maadili ya uongozi bora katika maisha yangu yote ya siasa, na nawaahidi sitarudi nyuma katika mapambano dhidi ya rushwa katika nchi hii pamoja na mikakati ya aina hii ya kunidhoofisha na kunivunja moyo;
  2. Nafarijika na salam mbali mbali zinazotolewa kunifariji na kusisitiza kuwa nisilegeze kamba katika mapambano haya, nimepokea ujumbe mwingi kwa simu, sms, tweeter na hata facebook na niko pamoja nanyi Watanzania wenzangu kamwe sitarudi nyuma hadi kieleweke. Naamini katika nchi yetu tunazo rasilimali za kutosha mahitaji/haja ya kila mmoja wetu lakini si ‘tamaa/ulafi’ wa baadhi ya watanzania wenzetu;
  3. Napenda kuweka rekodi sawa kwa Watanzania kwamba nimekuwa Mbunge hiki ni kipindi cha pili, Mimi ni Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) huu ni takriban mwaka wa saba sasa, Kamati yangu inasimamia mashirika 259 ya Umma na si TANESCO peke yake. Mchango wa Kamati hii katika Bunge na kwa ustawi wa Mashirika ya Umma ni bayana na haujawahi kutiliwa shaka. Kamati yetu imeokoa upotevu mkubwa wa mali za umma na kuokoa fedha za umma kutokana na umakini wake. Tumefanya hivyo CHC hivi karibuni, Kiwira na kwenye mashirika mengine mengi. Kote huko uadilifu na uzalendo wa Kamati hii haujawahi kuhojiwa. Inatuwia vigumu kuona kuwa tunahojiwa katika suala hili la TANESCO. Hapa pana kitendawili.
  4. Zipo hoja pandikizi za kutaka Kamati ya POAC ivunjwe na haswa zikinilenga mimi binafsi. Nafahamu kiu ya wasioitakia mema nchi yetu kuiona POAC ikivunjwa au sura zikibadilishwa kwa kuwa Kamati hii imekuwa mwiba kwa mikakati yao ya kifisadi. Kwa maoni yangu, Kamati ya POAC isihusishwe na tuhuma hizi kwa vyovyote vile. Niko tayari nihukumiwe mimi kama mimi na sio kuhusisha wajumbe wengine ambao hawatajwi mahala popote katika tuhuma hizi mbaya sana katika historia ya Bunge letu. Nitakuwa tayari kunusuru Kamati ya POAC na maslahi ya taifa letu kwa kujiuzulu Uenyekiti iwapo itathibitika pasipo shaka kuwa nimehongwa. Kamati ya POAC ni muhimu zaidi kuliko mimi.
  5. Nafahamu pia kuwa kuna wanasiasa hasa wa Upinzani ambao wanautaka sana Uenyekiti wa POAC na wanafanya kila njia kutaka kuidhoofisha. Lakini hawajui kuwa anaepanga wajumbe wa Kamati ni Spika wa Bunge.
  6. Msishangae pia kuja baadae kubaini kwamba baadhi ya wanasiasa wenye midomo mikubwa ya kutuhumu wenzao wao ndio vinara wa kupokea rushwa.
  7. Ni lazima tufike mahali kama viongozi kwamba utaratibu unapokiukwa na yeyote yule, au uongo unapotolewa hadharani tuseme bila kuogopa. Hili ndio jukumu letu kama wabunge na viongozi. Kusimamia ufuatiliaji wa utaratibu ni jukumu letu kama Kamati ya POAC na ndio sababu ya msingi ya kuanzishwa kwa mamlaka kama CAG na PPRA. Haiwezekani, tuwe na set ya kanuni kwa kundi fulani na nyingine kwa makundi mengine, au kuhukumu ufuataji wa taratibu kwa kuangalia sura ya mtu usoni

Mwisho

Kumejengeka tabia hivi sasa ya kuwamaliza wanasiasa wenye kudai uwajibikaji na uzalendo. Kumeanzishwa kiwanda kwenye medani ya siasa cha kuzalisha majungu na fitna zenye lengo la kuwachonganisha wanasiasa wa aina hiyo na wananchi kwa kutumia vyombo vya habari na nguvu ya fedha. Naamini mbinu hizi chafu, kama nyingine nyingi zilizojaribiwa kwangu huko nyuma nazo zitashindwa.

Naamini katika kweli na kweli daima huniweka huru. Naamini kuwa mwale mdogo wa mwanga wa mshumaa hufukuza kiza. Kwa imani hiyo, sitasalimu amri mbele ya dhamira zao ovu hata nitakapobaki peke yangu katika mapambano hayo ya kulinda na kutetea rasilimali za taifa zinufaishe watanzania wote.

Daima nitaongozwa na busara ya Hayati Shabaan Robert isemayo, ‘Msema kweli huchukiwa na marafiki zake, nitakapofikwa na ajali hiyo, sitaona wivu juu ya wale wawezao kudumu na marafiki zao siku zote, siwezi kuikana kweli kwa kuchelea upweke wa kitambo, nikajitenga na furaha ya kweli itakayotokea pale uwongo utakapojitenga”.

Ahsanteni sana.


xafi xana JEMBE
 
mohamedi SHOSI naendelea kukueleza kuwa acha kuchangia mada kwa unafiki.Bunge la sasa ni wazi wajumbe wa kamati ya POAC wengi ni CCM ndio wenye kuamua nani awe Mwenyekiti au Makamu mwenyekiti wa Kamati ikifuatiwa na CDM, hivyo ni wazi kuwa wenye kuamua nani awe kiongozi wa kamati ni wajumbe wa CCM maana ni karibu mara mbili ya wajumbe wa CDM.Hivyo si ajabu kuona sasa NCCR yenye mbunge mmoja Mh.Mrema ni Mwenyekiti wa LAAC na hivyo kwa UDP yenye mbunge mmoja Mh.Cheyo ni mwenyekiti wa PAC kwa sababu hao wamewekwa na CCM kwa sababu siyo "Threat" kwa CCM.CCM iliridhia kumpa ZZK uenyekiti wa POAC siyo tu kwamba anauwezo bali baada ya kushauriana wenyewe na kubaini kuwa siyo Threat kwao pia.Kumbukeni wakati huo baada ya uchaguzi jinsi ambavyo kanuni za bunge zilivyochakuliwa katika kutoa maana na tafasri zenye kukidhi malengo binafsi ya ccm.ni maiti tu ataunguna na wewe kwa hoja shallow namna hiyo.
 
Last edited by a moderator:
mimi kwa kweli zitto anazidi kujichanganya na kutuchangaya...hivi mbona haweki wazi ni sheria zipi zilizovunjwa na zimevunjwaje? kweli anataka kutufanya watu wote wajinga hatujui ni maamuzi gani yenye tija kwa taifa?
zitto kukweli naona unazidi kujichafua na kimbelembele chako na ujuaji vitakuponza badilika kaka....kama sheria haina maslahi ya umma ni bora ukaivunja na utaonekana hero.


ni wewe peke yako ndio hujaelewa...
 
Kwa mtazamo wangu wa akili ya kuzaliwa wapo wanene wanao injiania hii kitu kwani tunajua wapo viongozi wetu humu jf umeshawahi kuona wanadhubutu kuwaambia members wanachofanya ni wrong au ni utovu wa nidhamu kwa kiongozi wa kitaifa wa chama?

Na mimi naomba nikuulize wewe unadhani kwanini viongozi jf members wananyamaza? Zitto ni kati ya viongozi walioifanyia makubwa cdm! Zitto alikuwa CDM tangu cdm haijulikani kama inavyojulikana leo! Leo wamekuja watu juzi kati tu wapo juu Zitto amekuwa hafai tena?

Huu ni mtazamo wangu tu ndugu yangu Godlisten Masawe

Ok mkuu Mohammed Shossi, binafsi sina tatizo na kamanda Zitto, nina amini ana udhaifu wake kama binadamu wengine tu, nikiwemo mimi.
Hapo unaposema kwa nn viongoz wa CDM waliopo humu JF hawamtetei Zitto sidhani kama ni wajibu wao kufanya hiyo kazi ya kutetea watu humu, wajibu wa Zitto mwenyewe kujitokeza na kujibu shutuma coz hawa wanaomponda leo walimpenda juzi, so kama leo wanamwona hafai au dhaifu hapo kuna jambo mkuu. Vile vile humu kila mtu ana uhuru wa mawazo si kila mtu atafanya kile kinachokupendeza/kinachonipendeza kukisikia.
 
Last edited by a moderator:
185881_396646290384562_1167489938_n.jpg
 
Zitto alisema kwamba hajawai kushindwa kujisafisha atakama amechafuliwa kiasi gani.
 
Namfahamu Zito tangu Daruso, huwa anamaanisha anachokisema. Tusubiri hizo kamati ili tumalize fitina. Nimewahi kufukuzwa naye migomo ya wanafunzi, pamoja na kubembelezwa na utawala alibaki na msimamo wake. Zito keep fighting, the war is not yet! Plato aliwahi kusema "Only the dead have seen the end of war".

hahahaaaa ww uliandika barua ya komba kurudi nini? nakumbuka bana mlitusevu tukapata 2500/=
lakini b careful msomi mwenzangu kuwa watu hubadilika sana...ni sababu fulani iliyomfanya siku zile aweze kuwa mtetezi na ni sababu vile vile inayoweza kumfanya akawa vinginevyo...na huenda kwa sababu ya uwezo wake huo huo wakugangamala upande wa pili wakaamua kumnunua.
Note: simaanishi zito kanunuliwa au kweli ana husika na rushwa bali nakutahadharisha dhana ya kusema nilimjua fulani kwa muda mrefu kuwa yuko hivi ama vile ....no asili ya mwanadamu ni kubadilika

liwalo na liwe
 
Naanza kuamini lowassa was innocent. Mzee wa watu aliongea kwa uchungu mkuu kumbe alikutwa na hili la zitto na kuweka kumbukumbu sawa
 
Sioni jipya kwa Zitto Kabwe zaidi ya ushuzi mtupu, sana sana anasema anaonewa donge na wabunge wenzake wa upinzani yeye kuwa mwenyeki wa POC. ( Kumbe kuna ulaji mpaka mtu aonewe donge? )
Nashukuru tu hakusema anaonewa kwa sababu yeye ni Mwislamu kama ilivyo sababu dhaifu ambazo uzitumia vibaraka wake hapa JF kumtetea.
 
Zito badilika, wabunge wa upinzani wakipanga kususia jambo wewe unaliunga mkono, sasa na wanaona si mwenzao uko upande wa chama tawala, na CCM nao wamekugeuka uko alone.

P/s fanya move zako ukikiusisha chama, nenda pamoja na msimamo wa chama chako sio kufanya unayoona ni sahihi.

hata kama wanasusua ujinga yaani unataka zitto aungane na wakina selasini kudai posho ziongezwe
 
Sioni jipya kwa Zitto Kabwe zaidi ya ushuzi mtupu, sana sana anasema anaonewa donge na wabunge wenzake wa upinzani yeye kuwa mwenyeki wa POC. ( Kumbe kuna ulaji mpaka mtu aonewe donge? )
Nashukuru tu hakusema anaonewa kwa sababu yeye ni Mwislamu kama ilivyo sababu dhaifu ambazo uzitumia vibaraka wake hapa JF kumtetea.

anaonewa wivu na wakaskazini kama mbatia na selasini
 
mohamedi shosi acha ushabiki wa kinafiki.Ni wazi kuwa hakuna mbunge wa upinzani aliye makini anayetamani au kutafuta uenyekiti wa kamati ya POAC.Uenyekiti wa kamati haupewi na Spika bali wajumbe wa kamati ndiyo wanapiga kura.Kumbukeni ZZK kupata uenyekiti huo ni baada ya JK na Pinda kushauriana na kuamua kumwacha kuendelea kwa sababu yeye kama kiongozi wa CDM hakuwa na madhara kwa CCM.Leo hii endapo ZZK atatolewa kwenye nafasi ni CCM hawako tayari kumpatia nafsi hiyo mbunge wa CDM kwa haina yye ile ni bora apewe NCCR au CUF ,mbona CCM walimpa CHEYO nafsi ya uenyekiti PAC wakati UDP ina mbunge mmoja kwenye Bunge.
Wenzio wanaangalia kwanza huyu ni dini yetu? stuka mkuu....hakuna kitu hapo
 
Sioni jipya kwa Zitto Kabwe zaidi ya ushuzi mtupu, sana sana anasema anaonewa donge na wabunge wenzake wa upinzani yeye kuwa mwenyeki wa POC. ( Kumbe kuna ulaji mpaka mtu aonewe donge? )
Nashukuru tu hakusema anaonewa kwa sababu yeye ni Mwislamu kama ilivyo sababu dhaifu ambazo uzitumia vibaraka wake hapa JF kumtetea.
hapo ndo kaniacha na question mark kichwani..anatufanya tuungane na wale wanaoamini kuwa ni msaliti wa hicho chama chao...kumbe chake ni chake ....hawakilishi upinzani sio ..so who is he then?
 
Back
Top Bottom