Maduka ya Shoprite-Naomba maoni

Johnsecond

JF-Expert Member
May 4, 2010
1,076
211
Jamani mwenzenu mara tatu nimenunua kuku wameoza shoprite ni wale ambao wanakuwa wamekaangwa. Pia majuzi nimeenda kununua Keki zile kama za sherehe za watoto nikashangaa yule mama ananifungia keki kwenye box la azam juice ambalo limeshamaliza juice actuaaly alishaandika na jina pale juu nikakataa kuchukua ile keki. Anayedhani uongo aende kesho aagize keki aone kinachotokea ni pale kamata. Sasa hivi hapo usafi uko wapi ? Wenzangu hamjakumbana na mambo ya hivyo ni mimi tu?

Nawasilisha.
 
Yaani umepata mkasa mara ya kwanza ukarudia tena, ukapata mkasa na bado ukarudia tena... inaelekea unaiamini sana hiyo supermarket
 
ya kamata? Zamani sana nilinunua kuku walopikwa walikua wameharibika. Kama miaka yote hii hawajajirekebisha wana walakini!
 
Nyie mnaojipa tabu na makuku yenu ya supermarket sie wengine twaenda beba kule stirio sokoni wale bado wamoto moto au pale njia panda kigogo kuku saaafi
 
Wavivu wa kupika utawajua tu. Mke mzima anaenda kununua chakula ambacho kimeshapikwa na wenzie, badala ya kupika mwenyewe nyumbani ili vinukie na mmewe apate hamu ya kula. Kila siku Shoprite-shoprite-shoprite mpaka ugali unanunua shopwrite!!!! mnaniudhi sana.
 
Wale ni wahuni tu. Hata kwenye shelves kuna vitu kibao vime expire. Angalia sana lebo wakati wa kununua. Mi pale nanunua pombe kali na wine tu, sigusi kitu ingine, hata dog food sinunui
 
kuna vitu vya kununua supermarket!kwa nini usipate kuku fresh kwenye masoko yetu yaleee?
 
Wale ni wahuni tu. Hata kwenye shelves kuna vitu kibao vime expire. Angalia sana lebo wakati wa kununua. Mi pale nanunua pombe kali na wine tu, sigusi kitu ingine, hata dog food sinunui
tangu lini kibuku unayokunywa imekuwa pombe kali? we sema unapita pale ubungo stendi ya mkoa unajichukulia ka creti kako kamoja wakati wa foleni unachapa mwendo
 
Shoprite hamna kitu sijui taasisi za Tanzania ni za ofisini tu au wapi? maana kuna TBS kuna TFDA na makolokolo kibao utakuta wanabobea sehemu za machinga kuwaibia pesa zao tu. Huko huwa hawaendi ila ni uchafu mtupu Shoprite najisikia kinyaaaaaaaa
 
aise kuku fresh mtaani unaenda kwa mfugaji unamwambia namtaka yule jogoo pale anawaita watoto wa jirani waanze mbio kumkimbiza na kumkamata
hata ukimpika mpaka majirani wanahisi harufu yake maana yule anakula wadudu wa mashambani
 
aise kuku fresh mtaani unaenda kwa mfugaji unamwambia namtaka yule jogoo pale anawaita watoto wa jirani waanze mbio kumkimbiza na kumkamata
hata ukimpika mpaka majirani wanahisi harufu yake maana yule anakula wadudu wa mashambani

Kweli mkuu
anakuwa fresh kabisa
 
Kweli mkuu
anakuwa fresh kabisa

Hata siku moja usilogwe kununua kuku wa supermarket au hata samaki maana ukiuliza wamekaa siku ngapi au ukijua muda waliokaa kwenye hizo fridge zao unaweza tapika
 
Hivi kweli, mtu na akili zako timamu, na jinsi masoko ya kuku yalivyojaa hapa Tanzania, unaweza kwenda kununua "vibudu" pale shoprite? Misifa itawaletea matatizo!!
 
Sio kuku tu wakuu ila bidhaa nyingi za shoprite ni mbovu na wanavutia watu kwa kupunguza bei. Kwa nini wahusika wasiwatembeleee kwa kustukiza siku moja waone uozo huuo. Mtoa mada alisema wanafunga keki kwenye box la azm ambalo limemaliza juice na hapo si crap hili genge wala sio supermarket
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom