Katika hali ya muendelezo wa
madudu katika mahakama yetu ya Tanzania, mwezi June mahakama iliajiri
Mahakimu wakazi wapya 300 wenye degree za sheria(LL.B) na kupitia
lawschool ili wakafanye kazi katika mahakama za mwanzo(kata).
jambo la kushangaza ni kuwa sheria inayoongoza mahakama za chini The
Magistrate Courts Act Cap 11 hairuhusu mahakimu hao (Mahakimu Wakazi)
kufanya kazi katika mahakama za mwanzo. hivyo mahakimu Wakazi hao hadi
leo hii hawana kazi za kufanya, kila siku wanaahidiwa kuwa sheria
itakuwa amended lakini hadi bunge la mwezi october limepita bila sheria
kubadilishwa
jambo la kushangaza ni vile uongozi wa Mahakama ulivyokaa kimya na
kuwasahau hawa vijana wenye moyo wa kuwatumikia wananchi wenzao kwa ari
mpya (!) bila kuwaambia lini sheria itabadilishwa.
.
mahakimu hawa kuendelea kulipwa SALARY bila kufanya kazi ni ufisadi na
mataumizi mabaya ya pesa za walipa kodi wa taifa hili wakati ni dhahiri
kuwa MAHAKIMU HAWA WANARUHUSIWA KISHERIA KABISA KUFANYA KAZI KATIKA
MAHAKAMA ZA WILAYA NA MAHAKAMA ZA HAKIMU MKAZI AMBAZO HAZINA MAHAKIMU WA
KUTOSHA .
TATIZO LINALOJITOKEZA HAPA NI UGONJWA WA KUFANYA MAAMUZI YA MSINGI
UNAOWASUMBUA VIONGOZI WETU.LISSU AKISEMA ETI ANAWADHARAU MAJAJI
KWEELI??????timely justice for all