Madudu Mengine ya MAHAKAMA YA TANZANIA

review

New Member
Nov 19, 2012
4
0
Katika hali ya muendelezo wa madudu katika mahakama yetu ya Tanzania, mwezi June mahakama iliajiri Mahakimu wakazi wapya 300 wenye degree za sheria(LL.B) na kupitia lawschool ili wakafanye kazi katika mahakama za mwanzo(kata).
jambo la kushangaza ni kuwa sheria inayoongoza mahakama za chini The Magistrate Courts Act Cap 11 hairuhusu mahakimu hao (Mahakimu Wakazi) kufanya kazi katika mahakama za mwanzo. hivyo mahakimu Wakazi hao hadi leo hii hawana kazi za kufanya, kila siku wanaahidiwa kuwa sheria itakuwa amended lakini hadi bunge la mwezi october limepita bila sheria kubadilishwa

jambo la kushangaza ni vile uongozi wa Mahakama ulivyokaa kimya na kuwasahau hawa vijana wenye moyo wa kuwatumikia wananchi wenzao kwa ari mpya (!) bila kuwaambia lini sheria itabadilishwa.
.
mahakimu hawa kuendelea kulipwa SALARY bila kufanya kazi ni ufisadi na mataumizi mabaya ya pesa za walipa kodi wa taifa hili wakati ni dhahiri kuwa MAHAKIMU HAWA WANARUHUSIWA KISHERIA KABISA KUFANYA KAZI KATIKA MAHAKAMA ZA WILAYA NA MAHAKAMA ZA HAKIMU MKAZI AMBAZO HAZINA MAHAKIMU WA KUTOSHA .

TATIZO LINALOJITOKEZA HAPA NI UGONJWA WA KUFANYA MAAMUZI YA MSINGI UNAOWASUMBUA VIONGOZI WETU.LISSU AKISEMA ETI ANAWADHARAU MAJAJI KWEELI??????timely justice for all
 

Nyalotsi

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
6,411
2,000
Kuna dada yangu kapelekwa huko sitimbi, sasa hivi anasimamia mashamba aliyonunua. Mungu saidia wasahau kubadili sheria ili na sie tuvune hayo mazao. Maana tumechoka kuwakumbusha hata basic things. Ukiwaambia wanasema unatafuta umaarufu wa kisiasa kumbe kuna kodi zetu zinapotea bure.
 

Bob G

JF-Expert Member
Oct 5, 2011
2,353
1,195
haiwezekani serikali dhaifu, bunge Dhaifu ukawa na mahakama yenye kutimiza wajibu, Tanzania nahisi ina laana wake
Katika hali ya muendelezo wa
madudu katika mahakama yetu ya Tanzania, mwezi June mahakama iliajiri
Mahakimu wakazi wapya 300 wenye degree za sheria(LL.B) na kupitia
lawschool ili wakafanye kazi katika mahakama za mwanzo(kata).
jambo la kushangaza ni kuwa sheria inayoongoza mahakama za chini The
Magistrate Courts Act Cap 11 hairuhusu mahakimu hao (Mahakimu Wakazi)
kufanya kazi katika mahakama za mwanzo. hivyo mahakimu Wakazi hao hadi
leo hii hawana kazi za kufanya, kila siku wanaahidiwa kuwa sheria
itakuwa amended lakini hadi bunge la mwezi october limepita bila sheria
kubadilishwa

jambo la kushangaza ni vile uongozi wa Mahakama ulivyokaa kimya na
kuwasahau hawa vijana wenye moyo wa kuwatumikia wananchi wenzao kwa ari
mpya (!) bila kuwaambia lini sheria itabadilishwa.
.
mahakimu hawa kuendelea kulipwa SALARY bila kufanya kazi ni ufisadi na
mataumizi mabaya ya pesa za walipa kodi wa taifa hili wakati ni dhahiri
kuwa MAHAKIMU HAWA WANARUHUSIWA KISHERIA KABISA KUFANYA KAZI KATIKA
MAHAKAMA ZA WILAYA NA MAHAKAMA ZA HAKIMU MKAZI AMBAZO HAZINA MAHAKIMU WA
KUTOSHA .

TATIZO LINALOJITOKEZA HAPA NI UGONJWA WA KUFANYA MAAMUZI YA MSINGI
UNAOWASUMBUA VIONGOZI WETU.LISSU AKISEMA ETI ANAWADHARAU MAJAJI
KWEELI??????timely justice for all
 

Lokissa

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
7,446
2,000
mtoa mada kasema kweli
mahakimu wakazi mahakama za mwanzo
ikitokea rufaa kesi zitasikilizwa na mahakimu wakazi wa wilaya au mkoa?
hiki ni kituko
Advocate Ordinance haiwaruhusu mawakili kwenda mahakama za mwanzo
nadhani kwa hili wamekurupuka
 

CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
12,369
2,000
Tundu lissu akiongea wapuuzi watasema anatafuta umaarufu.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
Mheshimiwa JK, sasa hapa Tundu Lisu akisema mnavunja katiba/mnakiuka sheria utasema TL anatafuta umaarufu wa kisiasa na kuwaomba majaji wawasamehe! CJ alikuwa wapi wakati wanawapeleka mahakimu hawa mahakama za mwanzo bila kuingilia kati. Au na yeye hajui kuwa hawaruhusiwi kufanya kazi ya uhakimu huko kisheria. Ulevi wa madaraka, bara liende!!!!!
 

Naibili

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,225
unategemea nini kuweka watu wasiojua kitu ndo wafanye maamuzi, lazima wasinzie sinzie
 
Top Bottom