Madua ya kuondosha matatizo ya dunia

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,148

Thread Tools
menu_open.gif
Search this Thread
menu_open.gif
Display Modes
menu_open.gif

#1
post_old.gif
12-16-2006, 09:30 PM
rashid43
user_offline.gif

Super Moderator
Master
Join Date: Dec 2006
Posts: 2,986
Thanks: 0
Thanked 56 Times in 49 Posts


icon1.gif
1.
1.Imamu Ja`afar bin Ssaadiq R.A.A. kasema, “Nashangaa kwa yule mtu aliyefikwa na madhara kisha akaghafilika kuomba dua ya Nabii Ayyuub A.S. inayosema, “
أَنِّي مَسَّنِي الضُّرُّ وَأَنْتَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ
“ANNIY MASSANIYA DHURRU WA-ANTA ARHAMU RRAAHIMIYNA.”
Maana yake, “Mimi yamenipata madhara. Na Wewe Ndiye unaye rehemu kuliko wote wanaorehemu.”
Kwani alipoomba dua hiyo Mola wake akasema, “
فَاسْتَجَبْنَا لَهُ فَكَشَفْنَا مَا بِهِ مِنْ ضُرٍّ
Maana yake, “Basi tukamwitikia, na tukamwondolea madhara aliyo kuwa nayo.”

2.Imamu Ja`afar bin Ssaadiq R.A.A. kasema, “Nashangaa kwa yule mtu aliyefikwa na dhiki kisha akaghafilika kuomba dua ya Nabii Yuunus A.S. inayosema, “
لا إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنتُ مِن الظَّالِمِينَ
“LA ILAAHA ILLA ANTA SUBHAANAKA INNIY KUNTU MINA DHAALIMIYNA.”
Maana yake, “Hapana mungu isipokuwa Wewe Subhaanaka (Uliye takasika). Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu.”
Kwani alipoomba dua hiyo Mola wake akasema, “
فَاسْتَجَبْنَا لَهُ وَنَجَّيْنَاهُ مِنْ الْغَمِّ وَكَذَلِكَ نُنْجِي الْمُؤْمِنِينَ
Maana yake, “Basi tukamwitikia na tukamwokoa kutokana na dhiki. Na hivyo ndivyo tunavyo waokoa Waumini.”

3.Imamu Ja`afar bin Ssaadiq R.A.A. kasema, “Nashangaa kwa yule mtu aliyefikwa na khofu ya kitu kisha akaghafilika kuomba dua ya Nabii Muhammad S.A.W. pamoja na Waislamu inayosema, “
حَسْبُنَا اللَّهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ
“HASBUNA LLAAHU WANA`IMA L-WAKIYLU.”
Maana yake, “Mwenyezi Mungu anatutosha (anatutosheleza).”
Kwani walipoomba dua hiyo Mola wao akasema, “
فَانْقَلَبُوا بِنِعْمَةٍ مِنْ اللَّهِ وَفَضْلٍ لَمْ يَمْسَسْهُمْ سُوءٌ
Maana yake, “Basi wakarudi (vitani) na neema za Mwenyezi Mungu na fadhila (Zake). Hapana baya lililowagusa.”

4.Imamu Ja`afar bin Ssaadiq R.A.A. kasema, “Nashangaa kwa yule mtu aliyefikwa na janga kisha akaghafilika kuomba dua ya Mwislamu wa watu wa Firauni inayosema, “
وَأُفَوِّضُ أَمْرِي إِلَى اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ
“WAUFAWWIDHU AMRIY ILA LLAAHI INNA LLAAHA BASWIYRUN BIL`IYBAADI.”
Maana yake, “Nami namkabidhi Mwenyezi Mungu mambo yangu. Hakika Mwenyezi Mungu anawaona waja Wake.”
Kwani alipoomba dua hiyo Mola wake akasema, “
فَوَقَاهُ اللَّهُ سَيِّئَاتِ مَا مَكَرُوا
Maana yake, “Basi Mwenyezi Mungu akamlinda na ubaya wa hila walizozifanya.”

5.Imamu Ja`afar bin Ssaadiq R.A.A. kasema, “Nashangaa kwa yule mtu aliyeneemeshwa na Mola wake akakhofia isitoweke neema, vipi akaghafilika kuomba dua inayosema, “
وَلَوْلا إِذْ دَخَلْتَ جَنَّتَكَ قُلْتَ مَا شَاءَ اللَّهُ لا قُوَّةَ إِلاَّ بِاللَّهِ
“MA SHAA-A LLAAHU LA QUWWATA ILLA BILLAAHI.”
Maana yake, “Na lau kuwa ulipoingia bustani yako ungelisema, “Mashaallah! Alitakalo Mwenyezi Mungu huwa! Hapana nguvu ila kwa Mwenyezi Mungu.”
Last edited by rashid43; 06-17-2010 at 06:22 PM.

 
jazakallah kheir,M/mungu akuongeze kheri,inawezekana ma mods wakaitoa lkn tushakusoma sheikh
 
umeweka siri kubwa humu...mimi wakati nlikua napita air port na mizigo yangu... Moja ya hizo du3a...nlisoma na watu wa usalama wakawa wamezubaa kabisa. Uushuhuda huo ndio nmeutoa leo!
Shukran.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom