Madiwani watano wa CHADEMA jiji la Arusha wajivua madaraka

Madiwani watano wa CHADEMA jiji la Arusha wajivua madaraka

digba sowey

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
10,141
Reaction score
22,022
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk Maulid Madeni amesema amepokea barua za kujiuzulu za madiwani watano wa Chadema Jiji la Arusha.

Mbali na barua hizo za kujiuzulu, madiwani hao pia wamemuandikia barua katibu wa CCM Wilaya ya Arusha wakiomba kujiunga na chama hicho tawala nchini Tanzania.
Kutokana na kujiuzulu kwa madiwani hao, Jiji hilo sasa lina madiwani 28 ambapo 20 ni wa Chadema na CCM wanane.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, CCM ilipata diwani mmoja lakini hivi karibuni madiwani saba wa Chadema walijiuzulu na kujiunga na chama hicho tawala.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi Novemba 30, 2019, Dk Madeni amesema Jiji tayari limeanzia mchakato wa kuzifikisha barua hizo katika ngazi nyingine.
"Ni kweli madiwani hawa wamejiuzulu na barua ninazo,” amesema.

Madiwani waliojiuzulu ni George Nditika (Baraa), Veronica Hosea, Glory Kaaya, na Jeni Severe (wote Viti Maalum) na Godfrey Soilel (Simon).

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema alipoulizwa kuhusu madiwani hao amesema alikuwa na taarifa zao kuwa watajiuzulu.

Novemba 19, 2019, meya wa Chadema Jiji la Arusha, Kalist Lazaro alijiuzulu na kuhamia CCM.
 
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk Maulid Madeni amesema amepokea barua za madiwani watano wa Chadema kujiuzulu katika jiji la Arusha

Nb kichaka kinazidi kupukutika,kazi kwenu wanachadema.
Viva ccm
Hata hivyo miaka yao Kitano imebaki miez sita na kwa sababu wamekubali kinunuliwa kwa bei che kama makhaba wa kambi ya fisi waende tu , ila wajue yajayo chadema yanafuhisha, Tundu lisu ndiye atakaye ikomboa chadema dhidi ya hao mbwa mwitu.
 
Hao ni wale wa VITI MAALUMU, wamejua uchaguzi ujao hawatapata maana CCM inachukua kwa nguvu so wameamua kuchukua fedha za kununuliwa kwao mapema, wakijumlisha na pensheni zao watakuwa wamelamba dume, hasara ni kwa CCM.
 
Back
Top Bottom