Madiwani wapya

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,793
12,238
Katika kata ya Chang'ombe Manispaa ya Dodoma CCM wameshinda, je katika kata zingine zilizofanya uchaguzi jana matokeo yako vipi?

Tafadhali wenye taarifa watujuze.
 
Katika kata ya Chang'ombe Manispaa ya Dodoma CCM wameshinda, je katika kata zingine zilizofanya uchaguzi jana matokeo yako vipi?

Tafadhali wenye taarifa watujuze.
duh! hawa wagogo sijui wataamka lini maana wamelala usingizi wa pono na watabaki ombaomba mpaka yesu arudi
 
mgogo kumbadilisha aelewe kuwa ccm ndo wanaleta tabu hizi hapa tz ni ngumu kweli..

Hata nchi mbili zinapoingia kwenye vita...zile sehemu muhimu ndio hupigwa kwanza ili kudhohofisha....ndio kitu CDM inafanya...zamu yao itafika tu!!..
 
Hata nchi mbili zinapoingia kwenye vita...zile sehemu muhimu ndio hupigwa kwanza ili kudhohofisha....ndio kitu CDM inafanya...zamu yao itafika tu!!..

wagogo wamezoea BAJAJI na TINGATINGA tu, ngoja walale sisi haoooo
 
duh! hawa wagogo sijui wataamka lini maana wamelala usingizi wa pono na watabaki ombaomba mpaka yesu arudi

Njaa ikizidi inafedhehesha mkuu, Dodoma kuna njaa kali kiasi kwamba Magamba yakigawa vijizawadi kidogo, wagogo wanauwaona wakombozi kumbe ndo wanawachimbia kaburi la UAMSIKINI.
 
mbio za kuelekea 2015 ndo kwanza zimeshika kasi,ombwe la uongozi limejidhihirisha wa magamba wamechoka watuachie nchi wenye uwezo wa kuongoza na wenye kujua matatizo ya wananchi.Viva CDM viva
 
Wadau, endeleeni kutujuza, hivi ni kata sita tu ndo zilizokuwa na chaguzi? kama zipo nyingine, matokea yakoje huko kwingineko? Tunapoipongeza CDM kwa huu ushindi mnono wa Arumeru, hebu tuone pia kwenye hizi kata imefanyaje. Viva CHADEMA, viva mabadiliko!!!
 
tusiwalaumu wala kuwatukana wagogo bali tuwaelimishe ili wawe na chachu ya mabadiliko

Wajumbe wa nyumba kumi Dodoma ni watu wenye dhiki kubwa! Wanakubali zawadi na ahadi ndogo ndogo kwa urahisi sana. Aidha bado wananchi wengi na hasa vijijini wanawategemea sana hawa kwa kuwa misaada yote inayotolewa na serikali inapitia kwao.

Hivyo endapo Wagogo watapata elimu ya kutosha na nguvu za kiuchumi kwa maana ya fedha za kujikimu wanaweza kubadilika!
 
kwa hiyo mnataka kuwasadikisha watu kua kila ccm inaposhinda kuna dhiki,Temeke nako kuna wagogo,ilala kwa zungu?acheni kua myopic halafu mnajifanya great thinkers,kwenye msafara wa mamba na kenge wapo ndio maana sio kila anae login jamii forum ni great thinker
 
Back
Top Bottom