Inawezekana mawazo yako ni sawa, lakini kumbuka kule Meru kata 17 zote madiwani ni CCM mbona walishindwa kuisaidia ikashinda uchaguzi? Hakuna wa kuzuia nguvu ya umma bwana. Kama ni kuwasamehe wanaweza kusamehewa lakini udiwani sijui sheria imekaaje, maana bado kesi iko mahakamani. Wanaojua sheria zetu watujuzeCCM ni wajanja hii ni mbinu ya kuimaliza chadema endapo uchaguzi wa bunge utarudiwa katika jimbo la Arusha mjini. Hawa madiwani wakisamehewa watasimama kama wako chadema lakini watakuwa mamluki wa CCM katika ngazi ya kata zao kuchakachua ushindi wa chadema.
Tukumbuke nguvu ya madiwani katika ngazi ya kata ni kubwa. Chadema kuweni makini na agenda hii.
Pinda alikuwa Arusha kupanga mbinu mpya ya namna ya kuipa ushindi CCM kama uchaguzi utarudiwa endapo Lema atashindwa Rufaa.