Madiwani waliofukuzwa kwenda mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madiwani waliofukuzwa kwenda mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngongo, Aug 8, 2011.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Nimefinywa sikio toka chanzo cha uhakika kwamba madiwani waliotimuliwa na kamati kuu ya CDM watakwenda mahakamani kuomba zuio la mahakama dhidi ya uamuzi wa chama chao.Zuio hilo uenda likazuia pia mkutano wa CDM unaotarajiwa kufanyika alhamisi mjini Arusha kuzungumzia kwa namna yoyote mgogoro wa madiwani hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa na kuamuliwa na mahakama.

  Naomba kuwasilisha.
   
 2. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ni haki yao kabisa ya kikatiba, na hilo lilitarajiwa kutokea kwahiyo si ajabu sana, hata watabiri wengi wa hapa JF "walishaliota".

  Tunasubiri tu hiyo kesi ifunguliwe tujue wanadai nini na mahakama itaamuaje, hususan juu ya huo mkutano wa alhamisi.
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mwita Maranya kwa mtazamo wangu nilifikiri CDM ilitakiwa ijikite zaidi na mapambano ya ufisadi badala ya kushughulika na madiwani ambao wanaweza kukidhalilisha chama.Ndiyo maana muda mwingi nilitaka jambo hili limalizwe kwa namna tofauti na hii ya sasa.
  Unajua mahakama zetu suala hili linaweza kupigwa danadana hadi mwaka 2015 na kukiachia chama makovu yasiyotibika

   
 4. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #4
  Aug 8, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Swali la msingi ambalo nimekuwa nikiwauliza wale msiokubaliana na uamuzi wa kuwatimua madiwani ni moja tu; mnadhani chadema walitakiwa kufanya nini kwa hawa madiwani ambao wamekaidi maagizo na maelekezo ya kamati kuu?na maamuzi hayo yalitakiwa yawe yenye kukiimarisha chama pande zote kiuongozi na kulinda maslahi yake na ya wananchi? hebu tuanzie hapo.

  Lakini pili, suala la mahakama kupiga danadana kesi za namna hiyo si geni miongoni mwa watanzania, na watu wa arusha nao wanalifahamu hilo. Kwahiyo mwisho wa siku chadema hawataweza kubebeshwa mzigo wa kuchelewesha kesi, labda washitaki ndo watakuwa na kazi ya kueleza wananchi ni kwanini walifungua kesi huku wakijua kwamba mahakama itakawia kutoa maamuzi na hivyo kuwaathiri wananchi?
   
 5. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #5
  Aug 8, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Wakuu nimeongea na chanzo cha habari hii kanithibitishia wakili ameshapatikana [jina naliweka kapuni] kesho asubuhi na mapema kesi itafunguliwa mahakama kuu.Viongozi wa CDM makao makuu mnaojiandaa kuja Arusha kwaajili ya mkutano alhamisi mjiandae pia kwaajili ya pingamizi la mahakama.

  Madiwani wote waliofukuzwa CDM watajiunga na chama kingine cha upinzani mkoani Arusha baada ya kumalizana na CDM mahakamani.

  Naomba kuwasilisha.
   
 6. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #6
  Aug 8, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Naomba kukuuliza swali juu ya swali unadhani kuwafukuza ni suluhisho pekee.

   
 7. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #7
  Aug 8, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,056
  Likes Received: 3,980
  Trophy Points: 280
  hao Madiwani wanaumwa maana ni wazi wametofautiana na sera za chama! sasa sijui kwanini hawakuhama chama mpaka wafukuzwe? kama mimi ni Judge natupilia mbali kesi yao!
   
 8. L

  LAT JF-Expert Member

  #8
  Aug 8, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  Kwahiyo kufungua kesi ndiyo suluhisho

  this is what we call left hand thinking capacity
   
 9. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #9
  Aug 8, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hapa si kwamba umeishiwa hoja tu bali hata propaganda imekushinda. Jenga hoja kama unayo sio unalalamika tuuuu kila siku. Ukiulizwa swali jepesi unakimbia je ukiulizwa swali gumu utafanyaje?
   
 10. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Ngongo, Ngongo, Ngongo nakumbuka chuki zako toka kabla na baada ya uchaguzi wa mwaka jana na kweli sasa unaanza hata kuudhi watu ! Hebu tujuze wanaenda mahakamani kuomba zuio la mahakama eti dhidi ya uamuzi gani wa chama chao, chama chao vipi wakati wameshavuliwa uanachama ? Wangeweza kuweka pingamizi wasivuliwe uanachama kama walikuwa na ubavu huo lakini kwa sasa wao si wananchama je wanataka kulazimisha warudishiwe uanachama ? Kumbuka Chadema haijawavua Udiwani, hilo si jukumu la Chadema na kama wanaenda mahakamani kwa hilo, bila shaka watapambana na mamlaka zinazohusika kama Tume ya Uchaguzi n.k. Labda iwe hiyo Tume ina uwezo wa kuvunja utaratibu na kuwaacha wasio na sifa kuendelea kuwa wajumbe wa Halmashauri Arusha kama madiwani wasio na chama, hapo nitaelewa vinginevyo imekula kwao na kwako, get a life !
   
 11. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ngongo bana naona sasa unakuwa driven na wishful thinking, how come umefukuzwa kwenye chama kwa utaratibu halali wa chama husika halafu ukaenda mahakamani???? Hao madiwanni sasa wanatafuta uadui na wananchi, Mahakama itatumia katiba ya CDM kutoa uamuzi and guess what?????? The guyz will alwayz loose unless kama hawafahamu ni maana ya kuwa mwanachama wa chama cha siasa. Lakini pia kumbuka, CDM walichofanya is in the line of:

  "Sometimes losing one battle helps you win the war"
   
 12. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Madiwani waliotimuliwa Chadema wajipanga kwenda mahakamani [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Monday, 08 August 2011 21:28 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]0diggsdigg

  Peter Saramba, Arusha
  KUNA uwezekano wa madiwani watano wa Chadema, waliovuliwa uanachama na kamati kuu ya chama hicho mwishoni mwa wiki iliyopita kwenda mahakamani kupinga uamuzi huo.

  Uwezekano huo ulielezwa na Diwani wa Kata ya Elerai, John Bayo,
  alipozungumza kwa njia ya simu akiwa njiani kutokea Dodoma walipokwenda kuhojiwa kabla ya uamuzi wa kutimuliwa kufikiwa.
  "Binafsi sina kinyongo na chama changu wala viongozi wake. Nimepokea uamuzi huo kwani ndiyo msimamo wa vikao, lakini nakuhakikishia bado nina imani ya kuendelea na nafasi yangu ya udiwani hadi uchaguzi mkuu ujao, kuna njia nyingine ya kupinga uamuzi huo kupitia vikao au mahakamani," alisema Bayo.

  Bayo alisema kabla ya kuchukua uamuzi wowote watazungumza na wapiga kura kwenye kata zao, kuwaeleza yaliyojiri na kuacha nafasi ya uamuzi wa hatua zinazostahili mikononi mwa umma uliowaamini na kuwapa dhamana ya uongozi.
  "Pia, tutawasiliana na wanasheria wetu kuangalia mwanya wa hatua za kisheria kama zipo, ili kulinda na kutetea haki zetu za msingi iwapo zitagundulika kukiukwa katika uamuzi huo," alisema.

  Bayo aliyekuwa Katibu wa Kamati ya Madiwani wa Chadema Manispaa ya Arusha, alitimuliwa kwa kugoma kujiuzulu wadhifa wa uenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Uchumi aliopata kutokana na mwafaka waliofikia kati yao na wenzao wa TLP na CCM.

  Wengine waliotimuliwa na kata zao kwenye mabano ni, Estomih Mallah (Kimandolu), Charles Mpanda (Kaloleni), Reuben Ngowi (Themi) na Rehema Mohamed wa Viti Maalumu. Diwani wa Kata ya Sekei, Chrispine Tarimo, uamuzi wake umewekwa kando baada ya kutohudhuria kikao cha Dodoma kutokana na udhuru.
  Kuhusu iwapo watajiunga na vyama vingine vya siasa kuomba uteuzi wa kutetea udiwani, Bayo alisema wanasubiri uamuzi wa wananchi kufikia hatima yao kisiasa.

  Wakati hayo yakitokea, wananchi 48 kati ya 50 waliohojiwa jana kuhusu uamuzi wa kutimuliwa kwa madiwan hao waliunga mkono wakisisitiza kutochukua hatua hiyo kungefanya chama hicho kukosa nguvu ya kukinyooshea kidole CCM kwamba inashindwa kufanya uamuzi mgumu.
  "Kamati kuu ni kikao cha juu kwa uamuzi katika chama chochote cha siasa, kikitoa agizo na likapuuzwa na mwanachama au kiongozi yeyote, halafu chama kisichukue hatua ingekuwa ni udhaifu. Hata hawa madiwani walijua adhabu yao ni kufukuzwa, hivyo wamepata stahili yao," alisema Karim Abdalah, mkazi wa Kaloleni.

  Karim aliyejitambulisha kuwa mkereketwa wa CCM, alisema uamuzi wa kuwadhibiti wanaokiuka maadili na maelekezo ya vikao vya uamuzi, ni utamaduni uliozoeleka katika chama chake inayowadhibiti wote wanaokiuka maagizo na maelekezo ya vikao halali.

  Kwa upande wake, John Meddah, mkazi wa Sekei na mwanachama wa CCM yeye alipinga uamuzi huo licha ya kukiri kuwa, hata chama chake kiliwahi kuwatimua udiwani madiwani wawili wa Manispaa ya Arusha, Mussa Mkanga (Sombetini) na Mary Kisaka (Viti Maalumu), huku aliyekuwa meya Paul Lota Laizer akivuliwa wadhifa wake.


  Source Mwananchi

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 13. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #13
  Aug 9, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Haya bana nimebandika source gazeti la Mwananchi sijui unataka nini ?.

   
 14. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #14
  Aug 9, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Test 1 2 3
   
 15. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #15
  Aug 9, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280

  wanahangaika kama jamaa aliyepigwa chini na Madam Josephine.

  embe likidondoka halirudi mtini.
   
 16. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #16
  Aug 10, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  An extract from your source:

   
 17. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #17
  Aug 11, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  BAADHI ya madiwani wa Chadema wameendelea kuhudhuria vikao vya madiwani licha ya Kamati Kuu (CC) ya Chama hicho kuzuia madiwani wake wote kufanya hivyo.

  Gazeti hili lilizungumza na madiwani hao jana kwa masharti ya kutoandikwa majina yao gazetini, ambapo walisema wanaendelea kuhudhuria vikao vya halmashauri hiyo kama kawaida.

  Mmoja wa madiwani hao, ambaye amefukuzwa uanachama, alisema jana walihudhuria kikao cha Kamati Ndogo ya Fedha na kwamba hata kesho watahudhuria kikao cha Baraza la Madiwani.

  Diwani huyo alifafanua kuwa kuvuliwa kwao uanachama hakumaanishi wasihudhurie vikao na kwamba wataendelea kuhudhuria vikao hadi Chadema itakapotoa taarifa rasmi kwa halmashauri hiyo.

  Alifafanua kuwa wataacha kuhudhuria vikao hivyo ikiwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda anayehusika na serikali za mitaa, atatangaza nafasi za kata zao kuwa wazi. Aliongeza kuwa wanajiandaa kukata rufaa Baraza Kuu la Chadema, huku wakiendelea kuhudhuria vikao vya halmashauri.

  Mkurugenzi wa Manispaa ya Arusha, Estomiah Chang'ah, alisema barua rasmi ikiwafikia, sheria inamtaka Meya wa Jiji hilo amwandikie Waziri Mkuu.

  Alifafanua kuwa sheria ya Serikali za Mitaa ya Mwaka 1982 inamtaka waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa atamke kuwa nafasi za madiwani hao ziko wazi.

  "Halmashauri ya Jiji la Arusha haijapokea barua rasmi ya madiwani hao kuvuliwa uanachama, hivyo bado wanaendelea kuwa madiwani na kuhudhuria vikao hadi barua hiyo itakapopokewa na kuthibitishwa na waziri mwenye dhamana,” alisema.

  Madiwani waliovuliwa unachama ni Naibu Meya na Diwani wa kata ya Kimandolu, Estomih Mallah; Diwani wa Elirai, John Bayo, Reuben Ngowi (Themi), Charles Mpanda (Kaloleni) na Diwani wa Viti Maalumu, Rehema Mohamed.

  Wakati huo huo, John Mhala anaripoti , kwamba katika mkakati wa kuweka mambo shwari ndani ya Chadema, uongozi wa juu wa chama hicho unatarajia kuhutubia mkutano wa hadhara siku yoyote kuanzia leo katika uwanja wa NMC jijini Arusha.

  Wanaotarajiwa kuwapo katika mkutano huo ni baadhi ya wajumbe wa CC ya Chadema, akiwamo Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa na Naibu Katibu Mkuu, Kabwe Zitto.

  Habari kutoka ndani ya Chadema zinadai kuwa mkutano huo una lengo la kueleza na kutetea uamuzi wa chama hicho wa kuwavua uanachama madiwani watano wa Jiji la Arusha. Mkutano huo utafanyika wakati baadhi ya wanachama na wapenzi wa chama hicho wakiwa na tafsiri tofauti juu ya uamuzi huo.

  Baadhi ya wanachama wamekuwa wakidai kuwa uamuzi huo ni wa kuwaonea madiwani hao na wa kutaka kumridhisha Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema).

  Wanachama wengine wanaunga mkono uamuzi wa Kamati Kuu wa kutimua madiwani hao. Hata hivyo, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samsoni Mwigamba, hakuwa tayari kuelezea msigano huo na kusema kwa ufupi tu kuwa mkutano upo na hakuna mgogoro wowote.
   
 18. Rugas

  Rugas JF-Expert Member

  #18
  Aug 11, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,053
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  kilm,hii inapatikana gazeti gani? Nafikiri madiwani wako sahihi kuwa watatambua kufutwa kwao uanachama baada ya kuwepo kumbukumbu sahihi,na kwa maandishi. Kwa sasa ngoja wachukue posho ya mwishomwisho.
   
 19. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #19
  Aug 11, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ni haki yao kikatiba. Nawapongeza kudai haki yao.
   
Loading...