Madiwani waliofukuzwa Chadema watinga Mahakama Kuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madiwani waliofukuzwa Chadema watinga Mahakama Kuu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Jan 21, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Madiwani wa Chadema waliofukuzwa uanachama wamefungua kesi Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, kupinga hatua iliyochukuliwa na chama chao na wanaiomba mahakama kumzuia Mkuruguenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Estominh ChangÂ’ah, kuitisha uchaguzi mwingine hadi kesi hiyo itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.


  Hata hivyo, kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 27, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Walalamikaji wamefungua kesi hiyo dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema wakipinga hatua ya bodi hiyo kuwafukuza uanachama.

  Chadema kiliwafukuza uanachama madiwani wake watano ambao John Bayo (Elerai), Reuben Ngowi (Themi), Rehema Mohammed (Viti Maalum), Charles Mpanda (Kaloleni) na Estominh Mallah (Kimandolu), kwa madai mbalimbali likiwemo la kukaidi maelekezo ya chama.

  Agosti mwaka jana, Kamati Kuu ya Chadema iliwafukuza uanachama madiwani hao kutokana na utovu wa nidhamu kwa kuingia katika mwafaka na madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kumaliza mgogoro wa uchaguzi wa Meya wa Arusha.

  Mzozo wa umeya uliibuka mwishoni mwa mwaka juzi, baada ya Chadema kupinga matokeo yaliyompa ushindi Gaudence Lyimo (CCM) kikisema kuwa uchaguzi huo ulikiuka kanuni za halmashauri.

  Kabla ya kufungua kesi Mahakama Kuu, walalamikaji hao walifungua kesi kama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Arusha, Hawa Mguruta, Agosti mwaka jana, lakini kesi hiyo ilitupiliwa mbali na mahakama iliagiza walalamikaji wafuate taratibu za kumaliza masuala yao ndani ya chama.

  Walalamikaji wanatetewa na Severine Lawena, wakati Chadema inatetewa na Wakili Method Kimomogoro na Mkurugenzi wa Jiji anatetewa na Wakili Lilian Kassanga.

  Ombi la kesi ya msingi ni namba 11 la mwaka 2011, ambapo walalamikaji wanataka Chadema isiwafukuze uanachama, wakati zuio la muda lipo katika ombi namba 12, la 2011. Wanataka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji asiitishe uchaguzi mwingine na nafasi zao za udiwani ziendelee kuwepo.

  Akipinga kuwepo mashtaka hayo, Wakili Kimomogoro alisema kesi hiyo imefunguliwa kimakosa kwa kuwa sheria inayotawala ufunguaji wa maombi hayo haijafuatwa.

  Pia alisema amri ya Mahakama ya Wilaya ya Arusha, iliyowataka walalamikaji wafuate taratibu za kumaliza masuala yao ndani ya chama bado haijatekelezwa.

  Alisema walalamikaji wanatakiwa kuzingatia amri hiyo ya mahakama kwa mujibu wa taratibu za katiba ya chama chao.

  CHANZO: NIPASHE


   
 2. T

  Topical JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  nitakuwa naangalia double standards za mahakama zetu hapa
   
 3. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  wakishinda italazimu kina Kafulila nao washinde hiii itakuwa aibu ya viongozi wa vyama
   
 4. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hiyo haina kushinda hapo watapigwa dana dana ili muda uende kwa si unajua gamba wanajua kabisa hata kama wakiitisha uchaguzi mwingine hawawezi kushinda na sijaona 7bu ya serikali ktwa kimya mpaka sasa bila kufanya utaratibu wa uchaguzi wakati mahakama tangia mwanzo washatupilia mbali hilo shauri
   
 5. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,110
  Trophy Points: 280
  vyama vimetekeleza wajibu wao, kama mahakama inaona wana haki itakuwa ni maamuzi yao, lakini nadhani ndani ya chama, hata walioshinda hawatakuwa na ujasiri wa kusimama na kutoa mawazo
   
 6. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #6
  Jan 21, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,700
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo mkuu unakiri kuwa mahakama zetu zina double standard?
   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  Jan 21, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  [​IMG] By Topical [​IMG]
  nitakuwa naangalia double standards za mahakama zetu hapa
  Inawezekana kuwa mahakama zetu ni double standard, since it's remotely controlled!
   
 8. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #8
  Jan 21, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Malla kubali matokeo wewe ni msaliti! You are just wast you time.
   
 9. Kinyamagala

  Kinyamagala Senior Member

  #9
  Jan 21, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  CCM WANAJUA HILO NA KUWA WANANCHI WALOKWISHA CHAGUA MABADILIKO HAWARUDI NYUMA,hapa mby ktk kata ninayoishi inayoitwa NZOVWE,tulimchagua diwani toka CHADEMA, mwaka jana akjiuzuru na kutangazwa kujiunga CCM,wakadhani wamepata,viongozi wote wa CCM wilaya za Mby hususani wenyeviti na makatibu wakahamia Nzovwe nyumba kwa nyumba bila kujali hadhi zao wakielezea upupu wao dhidi ya Chadema,Mwisho wa siku wananchi wa Nzovwe hawakujali bali wakatoa onyo kal;i zaidi ya mwanzo,wakamchagua diwani wa Chadema kwa nguvu na ushindi mnono zaidi ya ule wa awali,Jamaa hawakuamini majicho yao wakaennda kulala.
   
Loading...