Madiwani wa Moshi wagomea mafunzo kisa posho ya Tsh 100,000

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
33,346
2,000
Hili tukio halikuwai kutokea kwa kipindi chote ambacho Ndesamburo alikuwa mbunge na manispaa ya Moshi kuwa chini ya Chadema.

Ni aibu kwa madiwani kutoka chama kinachojiita cha mabadiliko kulilia posho badala ya mafunzo ya kuibua miradi na kuisaidia jamii.

Yaani madiwani hawa wako pale kwa maslahi ya matumbo yao tu.

Madiwani wa Rombo na Arusha pia waliwahi kugomea posho lakini baada ya wakurugenzi kuwa ngangari hatimaye walitulia.

Madiwani Rombo walilia posho
MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wamegoma kupewa mafunzo ya utaratibu ulioboreshwa wa uendeshaji wa Miradi ya Maendeleo kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGDG), wakishinikiza kupewa posho ya Sh 100,000 kwa siku.

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), yalitakiwa kufanyika jana katika ofisi za Halmashauri hiyo na kuwahusisha madiwani pamoja na wakuu wa idara.

Hata hivyo madiwani wote waligoma na kutoka nje, jambo lililosababisha wakufunzi kutoka Tamisemi kutoa mafunzo hayo kwa wakuu wa idara peke yao. Kabla mafunzo kuanza Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Michael Kilawila aliwaeleza madiwani hao kuwa, kwa sababu mafunzo hayo hayapo kisheria, halmashauri inatakiwa kutoa posho zao kutoka makusanyo ya ndani.

Alisema, kutokana na mapato ya halmashauri kuwa madogo, kila diwani atalipwa Sh 60,000 kama posho ya siku, hivyo kwa siku mbili za mafunzo hayo kila diwani angelipwa Sh 120,000.

Baada ya tamko hilo madiwani walionesha kutoridhishwa na kiwango hicho cha posho na kuanza kugonga meza wakishinikiza kulipwa Sh 100,000 kwa siku kama wanavyolipwa katika vikao vingine vinavyotambulika.

Kilawila aliwasihi madiwani hao wakubali posho hiyo, lakini waliendelea kugoma, na kuamua kutoka nje, wakiwaacha wakuu wa idara ndani ya ukumbi. Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Butamo Ndalahwa alisema, madiwani hao wamegoma kwa sababu ya kutaka posho kubwa bila kujali kuwa mafunzo hayo yangewanufaisha wananchi ambao ndio waliwachagua.

Alisema mafunzo hayo yanatolewa katika halmashauri zote nchini kwa lengo la kuhakikisha madiwani wanashirikiana na wananchi kuibua miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo halmashauri itawasaidia kuiendeleza.

Ndalahwa alisema, kitendo cha madiwani kugomea mafunzo hayo kitasababisha maendeleo ya halmashauri hiyo kurudi nyuma kwa sababu ya kukosa elimu ya uibuaji wa miradi ambayo inakubalika.

Alisema amesikitika sana kuona madiwani wanaweka maslahi mbele badala ya kuwatumikia wananchi ambao waliwachagua “tumewaelimisha sana sababu ya kuwapa posho ya Sh 60,000 lakini hawakutaka kuelewa badala yake walianza kugonga meza ovyo na kutoka nje.”

Gazeti hili liliwatafuta baadhi ya madiwani lakini hawakuwa tayari kuzungumza lolote kwa madai kuwa msemaji wao ni Mwenyekiti wa Halmashauri, Kilawila ambaye alisema hawezi kuzungumzia jambo lolote mpaka kikao cha madiwani kitakapokaa na kutoa maazimio.


Source:

Madiwani wagomea mafunzo, kisa posho ya 100,000/
 

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
9,176
2,000
Wasikilizwe kwanza yawezekana walijibiwa mbovu. Mbona mbadala umepatikana haraka namna hiyo ? Itakuwa walipewa majibu yasiyo na staha yakawakasirisha
 

MZEE MSASAMBEGU

JF-Expert Member
Apr 19, 2013
2,782
2,000
Kila mara wanatusema kwanini tunaipenda serikali ya JPM

Ila tukisema wao ni matumbo mbele hawana jipya la kuisaidia nchi yetu, wanatutukana

Haya hilo wanalofanya halinishangazi kabisaaaaaa
Mkuu ebu tupige hesabu...kwa mfano diwani anatoka eneo la mbali karibu na halmashauri..hiyo ebu tuongee ukweli hiyo 120,000 kwa siku zote mbili inatosha Chumba+chakula+nauli???ebu tuongee ukweli??
 

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
33,346
2,000
Madiwani siyo vichaa kutakuwa na tatizo na itakuwa wamegundua kiasi ambacho kilitakiwa kilipwe kimekwapuliwa na magamba wapiga rambirambi.
Umeisoma hiyo habari vizuri?Hela itakwapuliwaje wakati inatoka halmashauri ambapo signatory ni mwenyekiti wa halmashauri?
 

fablo can

JF-Expert Member
May 25, 2016
1,223
2,000
Mkuu ebu tupige hesabu...kwa mfano diwani anatoka eneo la mbali karibu na halmashauri..hiyo ebu tuongee ukweli hiyo 120,000 kwa siku zote mbili inatosha Chumba+chakula+nauli???ebu tuongee ukweli??
Huwa unafikiri kabla ya kuandika. Ama kweli naamini hakuna wazalendo katka nchi yetu. Ebu niambie kama kuna kata ya mbali amabayo unaweza kutumia nauli hata ya elfu kumi. Hawa ndo wanataka madaraka wakijiita wazalendo. Siasa za Tanzania imejaaa ubinafsi.
 

chabusalu

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
7,872
2,000
Hili tukio halikuwai kutokea kwa kipindi chote ambacho Ndesamburo alikuwa mbunge na manispaa ya Moshi kuwa chini ya Chadema.

Ni aibu kwa madiwani kutoka chama kinachojiita cha mabadiliko kulilia posho badala ya mafunzo ya kuibua miradi na kuisaidia jamii.

Yaani madiwani hawa wako pale kwa maslahi ya matumbo yao tu.
Kama wewe ulivyo hapa kwa maslahi ya tumbo lako! Utakimbiziaje hapa "unbalanced story"? Nenda kawatafute madiwani uwahoji ni kwanini wamegomea hiyo posho. Tuletee na package ya semina yenyewe tuone kama ilikuwa na maslahi gani, kafanye pia na investigative journalism ili kubaini exactly mkurugenzi alikuwa ameandaa bajeti ya kiasi gani kwa washiriki wa semina maana isije kuwa madiwani walikuwa wamenusa upigaji kama ambavyo mara kadhaa inafanyika!
 

NAKWEDE

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
27,900
2,000
Mkuu ebu tupige hesabu...kwa mfano diwani anatoka eneo la mbali karibu na halmashauri..hiyo ebu tuongee ukweli hiyo 120,000 kwa siku zote mbili inatosha Chumba+chakula+nauli???ebu tuongee ukweli??
Mkoa wa Kilimanjaro ni mkoa mdogo sana hapa Tanzania!!! unaweza kuuzunguka kwa masaa ma tano tu ukawa umeumaliza.
sasa kwa kesi ya madiwani wa Moshi hakuna anayesafiri umbali mrefu kufika eneo la mkutano.
 

mbikagani

JF-Expert Member
Dec 5, 2014
3,049
2,000
Tunatarajia kutakuwa na maelezo ya ziada why do they reject to accept!.
Kama sivyo, watakuwa hawakuonyesha mfano mzuri.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom