Madiwani wa CUF na CHADEMA Manispaa ya Kinondoni wasusia kikao

PAMBA1

Member
Sep 13, 2011
55
26
MADIWANI WOTE WA CHADEMA NA CUF WAMETOKA NJE KWA KUPINGA UKIUKWAJI WA KANUNI ZA HALMASHAUL YA KINONDONI,KANUNI YA SITA KIPENGELE C inayosema mkutano wa mwaka ni kuchagua naibu meya na wajumbe wa kamati pamoja na ratiba ya vikao pamoja na kujadili kazi za utekelezaji wa manispaa kwa kipindi cha mwaka mzima.

Cha kushangaza Meya na mkurugenzi wameleta agenda ya uchaguzi tu, pasipo agenda ya kazi za utekelezaji wa mwaka mzima kwakuhofia madudu waliyoyafanya kwenye budget iliyopita.
 
Pamba.. wewe ni diwani wa manispaa hiyo ungeweka uozo hapa wa Meya pamoja na mkurugenzi wake ili watu wajue serikali ya ccm kote wameoza si serikali kuu pee mpaka huku chini.
 
Last edited by a moderator:
Tusiwasemee watoke watuambie kisha tujadili, kutoka nje pekee hakuthibitisha kuwa aliyetoka nje na aliyebaki ndani ni nani kakiuka taratibu.

Sisi tutauunga mkono kwa kila jambo ambalo lina manufaa kwa wengi.
 
Pamba.. wewe ni diwani wa manispaa hiyo ungeweka uozo hapa wa Meya pamoja na mkurugenzi wake ili watu wajue serikali ya ccm kote wameoza si serikali kuu pee mpaka huku chini.

Tuweke pembeni mambo ya vyama kwani wanaoathirika na maamuzi mabaya ya viongozi ni wa vyama vyote.

Ukishaanza kusema serikali ya CCM wakati manispaa ina madiwani wa pande zote tutakuwa hatujadili jambo la kitaifa bali jambo la vyama vya siasa.
 
Kwani halmashauri inaongozwa na Meya wa chama gani? Au mkurugenzi anatoka Chama gani? Pls naomba majibu ili niendelee kujadili
 
Ni kweli manispaa inakuwa na madiwani wa vyama vyote, lakini elewa kuwa utendaji wa serikali katika ngazi zote huratibiwa na kusimamiwa na chama tawala kama sehemu ya kutekeleza ilani ya chama hicho na hii ndio inayopelekea tofauti hizo kwani vyama pinzani havipewi nafasi ndo mana mambo kama haya yanatokea ambayo hu athiri taifa.
 
walizoea kupitisha au maamuzi ya kijinga sasa watu wanataka kanuni zifuatwe japo bado wanaongoza wanajitahidi kutumia mabavu dawa yao ipo jikoni 2015...
hakuna kitu kipo sawa kila kitu sasa wanatumia mabavu sio akili
 
Back
Top Bottom